Askofu Lusekelo (Mzee wa Upako): Kesi ya Mbowe inakera sana na inaniumiza moyo

Mzee wa Upako anapata taabu sana kutambua kama kweli Mh Mbowe ni Gaidi au Sio Gaidi.
Atueleze ni kwanini anapata taabu kuamini ? Nadhani hakupata taabu UAMSHO walipoitwa magaidi ?. I see a pattern here.

Siamini kama Mbowe ni gaidi by the way, profile yake tuu haifit na izo tuhuma. Nadhani viongozi wengi wa CCM wana tatizo la kujiamini, personally si mwanachama wa chama chochote cha siasa. Na sijawahi kuomba uanachama hadi sasa, nasimama na haki tuu na jamii ilipo. Samia anaweza shinda uchaguzi bila ya hila wa ghilba yoyote katika uchaguzi, hamna haja ya kuwa na pressure yoyote jikiteni zaidi katika kuleta maendeleo na kuchapa kazi.

Wekeni maslahi ya taifa mbele kuliko ushindani usio na tija kwa jamii. Si lazima kushinda kwa kishindo kila uchaguzi, sheria zibadilishwe zinadumana hatua za maendeleo katika taifa.

Maasalaam.
 
Kuna watu wanaitwa kina malaria sugu, mti mkavu, riz 1 nk enzi za JK wapo humu, wote hao walikua wanakula hizo buku 7. Fatilia tu vizuri historia ya JF utaona hilo mkuu
Hao wote hawakua na athari Kama hivyo virusi vya Pole pole.
Watu walitekwa, waliuliwa walifungwa lakini wao walitetea tu.
 
Najua hilo, tukubaliane sasa kwamba unabadiri topic. Nilicho jadiri ni muasisi wa Lumumba buku 7 sports club kwamba sio utawala wa Magufuli/Polepole, ni utawala wa Kikwete/Nape Nnauye. Hilo la kutekwa kuuawa nk sote tunajua kwamba lilishamiri sana enzi za mwendazake
 
Waliopata kufahamika ni wa kipindi Cha MAGUFULI.
Wengi tulikuwa hatujui Mambo ya LUMUMBA BUKU 7
 
ndio maana yupo mahakamani, sasa kwa nini mnasema sio Gaidi wakati ushahidi haujakamilika na mahakama haija toa hukumu?!
Mahakama ndio yenye mamlaka ya kusema kama alikuwa anafanya vitendo vya kigaidi au la, tuache mahakama ifanye majukumu yake ya kikatiba.
sio mara leo unamsikia mzee Mbatia oohh kesi ya Mbowe ifutwe!! ohhh Mbowe sio gaidi!! huko ni kuingilia uhuru wa mahakama
pale unaona kuna ushahidi au uhuni tu? Hata Std 7 leaver anaelewa mchezo wao
 
Atueleze ni kwanini anapata taabu kuamini ? Nadhani hakupata taabu UAMSHO walipoitwa magaidi ?. I see a pattern here.

Siamini kama Mbowe ni gaidi by the way, profile yake tuu haifit na izo tuhuma. Nadhani viongozi wengi wa CCM wana tatizo la kujiamini, personally si mwanachama wa chama chochote cha siasa. Na sijawahi kuomba uanachama hadi sasa, nasimama na haki tuu na jamii ilipo. Samia anaweza shinda uchaguzi bila ya hila wa ghilba yoyote katika uchaguzi, hamna haja ya kuwa na pressure yoyote jikiteni zaidi katika kuleta maendeleo na kuchapa kazi.

Wekeni maslahi ya taifa mbele kuliko ushindani usio na tija kwa jamii. Si lazima kushinda kwa kishindo kila uchaguzi, sheria zibadilishwe zinadumana hatua za maendeleo katika taifa.

Maasalaam.
Mkuu sasa unataka mtu akipata taabu kuamini ndio apate tabu kwa kila jambo?
 
Hakutueza ni kwanini isiwezekane, wakati wa UAMSHO walipoitwa magaidi nadhani alijiridhisha na kuona ni sawia...that will be guess. Kama nilivyosema awali, I see a pattern.
 
Ni siku ya tatu sasa akihutubia ktk moja ya safu ya mafundisho yake katika jamii. Askofu wa Kanisa la TAG hapa Ubungo Kibangu Maarufu kama Mzee wa Upako ametoa maoni yake juu ya kesi anayohisi huenda ni ya kuzingizia ya Ugaidi dhidi ya Mbowe.

Askofu huyo licha ya kudai kuwa wafuasi wa chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema wamekuwa wakimtukana mitandao kwa kumhisi yeye na CCM ni maswahiba ametanabaisha kuwe yeye ni rafiki wa watanzania wote na vyama vyote na hata waio na vyama.

Ktk safu hiyo ambapo aligusia maswala ya Amani, Upendo na Haki ktk nchi amelalamikia kitendo cha mamlaka kumtubumu Mh Freeman Mbowe kwa makosa makubwa ya Ugaidi baada ya kuanza harakati za Kudai Katiba Mpya.

" Naamini Mbowe ni Mtu Muungwana, wangeweza kumuita na kumweleza kuwa Mzee Hii kasi yako ni kubwa punguza kidogo na angeweza kuelewa kuliko kumwita Gaidi" sehemu ya kauli zake.

Mzee wa Upako anapata taabu sana kutambua kama kweli Mh Mbowe ni Gaidi au Sio Gaidi. Huku akitanabaisha kuwa kesi hii itakuwa na Impact kubwa ndani na nje ya Taifa letu la Tanzania.

Amewashauri wenye mamalaka kuwa badala ya kumtweza Mbowe wamemfanya kuwa maarufu zaidi na kwamba Mambo kama haya yanawapa maadui zetu sababu za kuingilia Mambo Yetu kama Taifa.

Link ya video inapatikana ktk PTVTazanzania online Tv.

Nadhani sasa tumeona kinachoenelea.
 
Atueleze ni kwanini anapata taabu kuamini ? Nadhani hakupata taabu UAMSHO walipoitwa magaidi ?. I see a pattern here.

Siamini kama Mbowe ni gaidi by the way, profile yake tuu haifit na izo tuhuma. Nadhani viongozi wengi wa CCM wana tatizo la kujiamini, personally si mwanachama wa chama chochote cha siasa. Na sijawahi kuomba uanachama hadi sasa, nasimama na haki tuu na jamii ilipo. Samia anaweza shinda uchaguzi bila ya hila wa ghilba yoyote katika uchaguzi, hamna haja ya kuwa na pressure yoyote jikiteni zaidi katika kuleta maendeleo na kuchapa kazi.

Wekeni maslahi ya taifa mbele kuliko ushindani usio na tija kwa jamii. Si lazima kushinda kwa kishindo kila uchaguzi, sheria zibadilishwe zinadumana hatua za maendeleo katika taifa.

Maasalaam.
Anapata tabu kwa sababu Kesi ya Mbowe hakuna shaka kuwa imepikwa
 
Ni siku ya tatu sasa akihutubia ktk moja ya safu ya mafundisho yake katika jamii. Askofu wa Kanisa la TAG hapa Ubungo Kibangu Maarufu kama Mzee wa Upako ametoa maoni yake juu ya kesi anayohisi huenda ni ya kuzingizia ya Ugaidi dhidi ya Mbowe.

Askofu huyo licha ya kudai kuwa wafuasi wa chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema wamekuwa wakimtukana mitandao kwa kumhisi yeye na CCM ni maswahiba ametanabaisha kuwe yeye ni rafiki wa watanzania wote na vyama vyote na hata waio na vyama.

Ktk safu hiyo ambapo aligusia maswala ya Amani, Upendo na Haki ktk nchi amelalamikia kitendo cha mamlaka kumtubumu Mh Freeman Mbowe kwa makosa makubwa ya Ugaidi baada ya kuanza harakati za Kudai Katiba Mpya.

" Naamini Mbowe ni Mtu Muungwana, wangeweza kumuita na kumweleza kuwa Mzee Hii kasi yako ni kubwa punguza kidogo na angeweza kuelewa kuliko kumwita Gaidi" sehemu ya kauli zake.

Mzee wa Upako anapata taabu sana kutambua kama kweli Mh Mbowe ni Gaidi au Sio Gaidi. Huku akitanabaisha kuwa kesi hii itakuwa na Impact kubwa ndani na nje ya Taifa letu la Tanzania.

Amewashauri wenye mamalaka kuwa badala ya kumtweza Mbowe wamemfanya kuwa maarufu zaidi na kwamba Mambo kama haya yanawapa maadui zetu sababu za kuingilia Mambo Yetu kama Taifa.

View attachment 2123456
Yametimia
 
Back
Top Bottom