Askofu Lusekelo (Mzee wa Upako): Kesi ya Mbowe inakera sana na inaniumiza moyo

Askofu Lusekelo (Mzee wa Upako): Kesi ya Mbowe inakera sana na inaniumiza moyo

Wewe kwenda zako. Hatujawahi kukalia kimuya vitendo vya uminyaji haki. Sisi tumekuwa mstari wa mbele. Historia itatuhukumu kwa Haki.

Uliwateteta wapi mbona hatujawasikia kuwatetea hao waislamu waliobaki ndani zaidi ya kumtetea Mbowe ??
 
Huyu ni mnafiki. Rejea matamko yake ya huko siku za nyuma. Ni Chato Gang huyo, ana hasira na utawala uliopo madarakani, anatafuta huruma upande wa pili. Anafahamu fika kuwa "akiongea maneno matamu" hawatokosekana wa kumshabikia. Same trick Polepole is using. Tell them what they like to hear, and you are an instant hero!
Kumbe wanatuchora tu.
Asante Jasusi kwa comment yako.
 
Walipofungwa wale wengine miaka 9 na kuambiwa Magaidi bila ya uthibitisho mbona hakusema kitu au kisa mb*w ni Wa imani yke?
Lakini kama una kumbu kumbu nzuri kelele zilipigwa sana na kila mpenda amani na haki. Madai siku zote yalikuwa kama ni Magaidi mbona kesi haipelekwi mahakamani ili wahukumiwe kwa haki?

Hatimaye Kama Mungu tu wakaachiwa.
 
Mzee wa upako subiri mahakana itoe jibu. Endelea na mambo yako ya Biblia.
 
Ni siku ya tatu sasa akihutubia ktk moja ya safu ya mafundisho yake katika jamii. Askofu wa Kanisa la TAG hapa Ubungo Kibangu Maarufu kama Mzee wa Upako ametoa maoni yake juu ya kesi anayohisi huenda ni ya kuzingizia ya Ugaidi dhidi ya Mbowe.

Askofu huyo licha ya kudai kuwa wafuasi wa chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema wamekuwa wakimtukana mitandao kwa kumhisi yeye na CCM ni maswahiba ametanabaisha kuwe yeye ni rafiki wa watanzania wote na vyama vyote na hata waio na vyama.

Ktk safu hiyo ambapo aligusia maswala ya Amani, Upendo na Haki ktk nchi amelalamikia kitendo cha mamlaka kumtubumu Mh Freeman Mbowe kwa makosa makubwa ya Ugaidi baada ya kuanza harakati za Kudai Katiba Mpya.

" Naamini Mbowe ni Mtu Muungwana, wangeweza kumuita na kumweleza kuwa Mzee Hii kasi yako ni kubwa punguza kidogo na angeweza kuelewa kuliko kumwita Gaidi" sehemu ya kauli zake.

Mzee wa Upako anapata taabu sana kutambua kama kweli Mh Mbowe ni Gaidi au Sio Gaidi. Huku akitanabaisha kuwa kesi hii itakuwa na Impact kubwa ndani na nje ya Taifa letu la Tanzania.

Amewashauri wenye mamalaka kuwa badala ya kumtweza Mbowe wamemfanya kuwa maarufu zaidi na kwamba Mambo kama haya yanawapa maadui zetu sababu za kuingilia Mambo Yetu kama Taifa.

Link ya video inapatikana ktk PTVTazanzania online Tv.


HAA KUMBE NAWE UMO?
 
AMANI ya NCHI ni ya MUHIMU zaidi kuliko Mbowe au mwanasiasa yeyote yule.

Funzo kwa wanasiasa kwa hiki anacho pitia Mbowe kwa sasa ni;

Mtu yeyote yule au mwanasiasa yeyote atakaye jaribu kuchezea/kucheza na Amani ya Nchi atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria bila kujali wadhifa wake, awe CCM, NCCR, CDM, CUF, n.k atashughulikiwa kikamilifu.

Amani yetu ni kitu muhimu zaidi kuliko mtu yeyote au chama chochote kile.
Kwa akili zako chache aliyekwambia amani ya nchi inalindwa kwa njia hiyo ni nani,maana wote mlikutana wajinga.Omba Mungu akupe siku zakuishiili uje ushuhidie nchi inakapokuja kuingia kwenye matatizo uko mbele ambayo chanzo chake ni hawa hawa viongozi zalimu.
 
Hakunaga funzo kwenye uonevu,kesi ni ya kijinga,uonevu,ufujaji wa kodi zetu bure...actually mtu mwenye takataka kichwani tu ndio anaweza sema hii ni kesi halali.

Kesi ni ya kubumba na uzushi,ni suala la muda tu wataumbuka..Mbowe sio gaidi.
Mbowe sio Malaika.
 
AMANI ya NCHI ni ya MUHIMU zaidi kuliko Mbowe au mwanasiasa yeyote yule.

Funzo kwa wanasiasa kwa hiki anacho pitia Mbowe kwa sasa ni;

Mtu yeyote yule au mwanasiasa yeyote atakaye jaribu kuchezea/kucheza na Amani ya Nchi atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria bila kujali wadhifa wake, awe CCM, NCCR, CDM, CUF, n.k atashughulikiwa kikamilifu.

Amani yetu ni kitu muhimu zaidi kuliko mtu yeyote au chama chochote kile.
Usitudanganye hapa, CCM wamechezea amani ya nchi yetu kwa maneno na kwa vitendo, na HAKUNA kitu wamefanywa!

Watu wametamka hadharani,kuwa "watakaompinga Magufuli hawastahili kuishi" wakaenda mbali zaidi, wakaua wengi walioonyesha kutokubaliana na style ya uongozi ya JPM, wapo walionusurika vifo kwa kudra za Mwenyezi Mungu tu, mf.Mdude na Lissu, ingekuwa nchi zingine pangekuwa pamechafuka haswa...lakini kwa upole wa raia wa nchi yetu basi CCM wanaona wote hatujielewi kabisa!
 
Mpaka Leo siamini vyema nguvu wafuasi mwendazake kumchomekea Mama hili gari bovu! Hope leo Shauri litafutwa
Mnajaribu kumpa huyu mtu mnayemuita mama utakatifu ambao hana. Huyu ni muovu kama waovu wengine ndani ya chama chake. Mnataka mpaka afanye jambo gani la hovyo zaidi ndiyo muelewe kuwa naye hafai?
 
Back
Top Bottom