PostGE2025 Askofu Mihali awaasa Wakatoliki waliofanya Udanganyifu kwenye Uchaguzi wakatubu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Juuchini

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2018
Posts
1,968
Reaction score
2,832
Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa, Mhashamu Romanus Mihali, amewataka Wakristo, hususan waumini wa Kanisa Katoliki, kutimiza wajibu wao wa kusimamia haki, amani na uadilifu, hasa katika masuala ya uchaguzi, wakisisitiza kuwa kutotenda haki ni dhambi kubwa.

Askofu Mihali alitoa wito huo wakati wa homilia ya Misa ya Sikukuu ya Krismasi (Noeli) iliyoadhimishwa katika Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, Kihesa, jimboni Iringa.

Akizungumza na waumini, Askofu Mihali alisema Mkristo Mkatoliki amepewa dhamana ya kusimamia taratibu za uchaguzi kwa haki na kwa kuzingatia dhamiri safi, bila kuyumbishwa na shinikizo au maelekezo yanayokiuka misingi ya haki.

“Wewe Mkristo Mkatoliki umepewa wajibu wa kusimamia uchaguzi. Je, unasimamia uchaguzi vizuri? Ukielekezwa kufanya kinyume cha haki, unapaswa kusimama imara kama Mkristo na kusema hili si la haki, sitafanya,” alisema Askofu Mihali.

Aliongeza kuwa Mkristo anayeshiriki au kunyamazia vitendo vya udhalilishaji wa haki anapaswa kutambua kuwa anafanya dhambi, akisisitiza kuwa kuchezea dhamiri za watu bila kutubu ni kosa kubwa mbele ya Mungu.

Katika ujumbe wake wa Krismasi, Askofu Mihali aliwakumbusha waumini kuwa maadhimisho ya Noeli yanapaswa kwenda sambamba na kuishi maisha ya haki, unyenyekevu na amani, kama kielelezo cha kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

“Tukiwa tunaadhimisha sikukuu ya Noeli, tunapaswa kuwa watu wa haki, watu wa unyenyekevu na watu wa amani,” alisisitiza Askofu Mihali.

Aliwahimiza waumini kuishi mafundisho ya imani yao kwa vitendo, wakichangia kujenga jamii yenye misingi ya haki, ukweli na upendo, hususan katika kipindi hiki cha sikukuu.

#SAUTDIGITAL l #HABARI l #sautdigitalupdates l #RadioSAUTFm
 
Wanajisumbua tu na agenda za Padre Kitima. Yaani Kitima amewateka nyara maaskofu wengi, wameacha kazi ya kuhubiri neno la Mungu wamejikita kwenye siasa.
 
Wauaji lazima mkemewe
 
Kimbesa,Luca,Stunex karibuni kwa tafakuri wakaribisheni na washirika wenu wote kwenye timu yenu ya wimbo wa amani bila haki.
 
Wanajisumbua tu na agenda za Padre Kitima. Yaani Kitima amewateka nyara maaskofu wengi, wameacha kazi ya kuhubiri neno la Mungu wamejikita kwenye siasa.
Umezipata za ndani kuwa Fr.Kitima kawateka ili wamfuate?

Maana Maaskofu ndio wenye Baraza lao Kwahiyo Fr.Kitima ni mtendaji na kuna wakubwa wake.
 
Nape alishasema wakishaiba wanatubu ila ujumbe uwafikir wale wanajiita wakiristu au rc wakati tabia na mienendo Yao hazifanani
 
Umezipata za ndani kuwa Fr.Kitima kawateka ili wamfuate?

Maana Maaskofu ndio wenye Baraza lao Kwahiyo Fr.Kitima ni mtendaji na kuna wakubwa wake.
Yap!! Kabla ya Fr Kitima kuwa Katibu wa TEC, unamkumbuka nani alikuwa kwenye hiyo desk? Na je alikuwa ana trend kwenye mitandao kama huyu Kitima?
 
" Mimi kwa mfano kwenye kituo changu mpaka kufikia saa nane mchana ni wapiga kura 30 pekee ndiyo walijitokeza (na hapa ni kijijini eti!!) kati ya wapiga kura 450 waliojiandikisha! Msimamizi alipofika kukagua akaniachia maagizo ya kuhakikisha kitabu chote kinajaa! Yaani niache nafasi mbili tu! Hivyo mpaka wakati wa kufunga, mgombea wa chama tawala alikuwa amepata kuru 420!" Mwisho wa kunukuu.

Huu ujinga hauvimiliki. Karibia maeneo yote ya nchi kulifanyika uhuni.
 
Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa, Mhashamu Romanus Mihali, amewataka Wakristo, hususan waumini wa Kanisa Katoliki, kutimiza wajibu wao wa kusimamia haki, amani na uadilifu, hasa katika masuala ya uchaguzi, wakisisitiza kuwa kutotenda haki ni dhambi kubwa.

Askofu Mihali alitoa wito huo wakati wa homilia ya Misa ya Sikukuu ya Krismasi (Noeli) iliyoadhimishwa katika Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, Kihesa, jimboni Iringa.

Akizungumza na waumini, Askofu Mihali alisema Mkristo Mkatoliki amepewa dhamana ya kusimamia taratibu za uchaguzi kwa haki na kwa kuzingatia dhamiri safi, bila kuyumbishwa na shinikizo au maelekezo yanayokiuka misingi ya haki.

“Wewe Mkristo Mkatoliki umepewa wajibu wa kusimamia uchaguzi. Je, unasimamia uchaguzi vizuri? Ukielekezwa kufanya kinyume cha haki, unapaswa kusimama imara kama Mkristo na kusema hili si la haki, sitafanya,” alisema Askofu Mihali.

Aliongeza kuwa Mkristo anayeshiriki au kunyamazia vitendo vya udhalilishaji wa haki anapaswa kutambua kuwa anafanya dhambi, akisisitiza kuwa kuchezea dhamiri za watu bila kutubu ni kosa kubwa mbele ya Mungu.

Katika ujumbe wake wa Krismasi, Askofu Mihali aliwakumbusha waumini kuwa maadhimisho ya Noeli yanapaswa kwenda sambamba na kuishi maisha ya haki, unyenyekevu na amani, kama kielelezo cha kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

“Tukiwa tunaadhimisha sikukuu ya Noeli, tunapaswa kuwa watu wa haki, watu wa unyenyekevu na watu wa amani,” alisisitiza Askofu Mihali.

Aliwahimiza waumini kuishi mafundisho ya imani yao kwa vitendo, wakichangia kujenga jamii yenye misingi ya haki, ukweli na upendo, hususan katika kipindi hiki cha sikukuu.

#SAUTDIGITAL l #HABARI l #sautdigitalupdates l #RadioSAUTFm
Ye mwenyewe ameshatubu kukaa kwake kimya kwenye uchaguzi wa 2019 na 2020 kisa aliyekuwa anapigiwa kura ni mkatoliki?!!!! Atubu unafiki wao kwanza Kisha ndo aje na mahubiri yake.
 
Back
Top Bottom