Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula: Haki katika hukumu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
FB_IMG_1583831301921.jpg

Leo tarehe 10 Machi 2020 ni siku ambayo Mahakama ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam itatoa hukumu katika Kesi ya Uchochezi inayowakabili Viongozi Waadamizi wa CHADEMA akiwemo Mbunge wa Hai ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho na Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mheshimiwa Freeman Mbowe.

Hii itakuwa ni 'Hukumu ya Kihistoria' katika nchi yetu na kwa vyo vyote itakavyokuwa, hukumu hii italeta msisimko mpya katika Sheria za Tanzania na Siasa za Tanzania kwa ujumla. Hii ni kesi iliyobeba maslahi mapana kwa taifa hasa ikizingatiwa kuwa inawahusu Viongozi Wakuu wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini na ikitolewa katika mwaka ambao nchi inafanya Uchaguzi Mkuu.

Kwa vyo vyote vile, hukumu hii itaweza kujibu swali muhimu kuhusu 'Uhuru wa Mahakama' za Tanzania kwa upande mmoja na 'Ukomavu wa Demokrasia' kwa upande mwingine. Uhuru wa Mahakama utaweza kupimwa katika maeneo mawili. Je, uamuzi wa hakimu utaathiriwa na hisia za wafuasi wa CHADEMA pamoja na Watanzania wengine wanaofikiri kuwa hiyo ni kesi ya kisiasa? Au, Je! 'Uhuru wa Mahakama' utaathiriwa na 'mashinikizo kutoka juu'? Je, Mahakama itaweza kutenda haki pasipo kuathiriwa na mashinikizo kutoka katika pande hizo zote mbili?

Kwa vyo vyote vile, huu ni mtihani mgumu sana katika nchi yetu! Ni mtihani kwa Hakimu aliyesikiliza kesi, ni mhithani kwa Sheria zetu, ni mtihani kwa Katiba yetu, ni mtihani kwa Mahakama kwa ujumla wake, ni mtihani kwa CHADEMA, ni mtihani kwa Upinzani nchini, ni mtihani kwa Serikali, ni mtihani kwa CCM ambayo hivi karibuni Katibu Mkuu wake amesikika akisema kuhusu kutumia dola ili kubaki madarakani, ni mtihani kwa umoja na mshikamano nchini, na mtihani kwa wanasiasa wote.

Mimi kama Askofu nimemuomba sana Mungu kuhusiana na jambo hili. Nimemuombea Hakimu pamoja na jopo lake ili watende haki pasipo hofu, huba, woga wala upendeleo. Nimewaombea watuhumiwa ili wawe na utulivu katika mioyo yao. Nimewaombea wafuasi wa CHADEMA ili wawe na utulivu. Pia, nimemuomba Mungu ili hila isipate kutia mkono wake katika hukumu hii.

Kwa vyo vyote itakavyokuwa, kinachotolewa hukumu siku ya leo sio shauri au mashauri yaliyoko mbele ya Mahakama, bali haki ndiyo itakayotolewa hukumu. Kwa maneno mengine, 'Haki iko katika Hukumu' ('Justice is on Trial')! Watanzania wanaisubiri sana hukumu hii. Jumuiya ya Kimataifa nayo inaisubiri sana hukumu hii. Waombaji wanasubiri jibu kutoka kwa Mungu!

Tunapoendelea kusubiri kusomwa kwa hukumu hii, hebu tuimbe sote 'Pambio ya Haki na Hukumu' kama ilivyotungwa na kuimbwa na Mfalme na Nabii Daudi katika Zaburi 101.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani.
 
View attachment 1382878

hata Pompeo anafuatilia kwa karibu sana hii hukumu.
 
Tafadhali mliyoko mahakamani kisutu mtupe yanayojiri mana wengine sisi tupo huku alikokuwa akong'ang'ania joyce banda tunawategemea wa huko.
 
Hukumu kwa vyovyote vile itakavyotoka,lazima itazua mjadala mkubwa!Hapa ndipo serikali itakapojiona walikurupuka bila kuangalia athari zake mbeleni!Wakikutwa na hatia itazua taharuki,wasipokutwa na hatia pia itazua mjadala!Vyovyote vile naiona serikali ikivuliwa nguo hadharani!
 
View attachment 1382878

Leo tarehe 10 Machi 2020 ni siku ambayo Mahakama ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam itatoa hukumu katika Kesi ya Uchochezi inayowakabili Viongozi Waadamizi wa CHADEMA akiwemo Mbunge wa Hai ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho na Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mheshimiwa Freeman Mbowe.

Hii itakuwa ni 'Hukumu ya Kihistoria' katika nchi yetu na kwa vyo vyote itakavyokuwa, hukumu hii italeta msisimko mpya katika Sheria za Tanzania na Siasa za Tanzania kwa ujumla. Hii ni kesi iliyobeba maslahi mapana kwa taifa hasa ikizingatiwa kuwa inawahusu Viongozi Wakuu wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini na ikitolewa katika mwaka ambao nchi inafanya Uchaguzi Mkuu.

Kwa vyo vyote vile, hukumu hii itaweza kujibu swali muhimu kuhusu 'Uhuru wa Mahakama' za Tanzania kwa upande mmoja na 'Ukomavu wa Demokrasia' kwa upande mwingine. Uhuru wa Mahakama utaweza kupimwa katika maeneo mawili. Je, uamuzi wa hakimu utaathiriwa na hisia za wafuasi wa CHADEMA pamoja na Watanzania wengine wanaofikiri kuwa hiyo ni kesi ya kisiasa? Au, Je! 'Uhuru wa Mahakama' utaathiriwa na 'mashinikizo kutoka juu'? Je, Mahakama itaweza kutenda haki pasipo kuathiriwa na mashinikizo kutoka katika pande hizo zote mbili?

Kwa vyo vyote vile, huu ni mtihani mgumu sana katika nchi yetu! Ni mtihani kwa Hakimu aliyesikiliza kesi, ni mhithani kwa Sheria zetu, ni mtihani kwa Katiba yetu, ni mtihani kwa Mahakama kwa ujumla wake, ni mtihani kwa CHADEMA, ni mtihani kwa Upinzani nchini, ni mtihani kwa Serikali, ni mtihani kwa CCM ambayo hivi karibuni Katibu Mkuu wake amesikika akisema kuhusu kutumia dola ili kubaki madarakani, ni mtihani kwa umoja na mshikamano nchini, na mtihani kwa wanasiasa wote.

Mimi kama Askofu nimemuomba sana Mungu kuhusiana na jambo hili. Nimemuombea Hakimu pamoja na jopo lake ili watende haki pasipo hofu, huba, woga wala upendeleo. Nimewaombea watuhumiwa ili wawe na utulivu katika mioyo yao. Nimewaombea wafuasi wa CHADEMA ili wawe na utulivu. Pia, nimemuomba Mungu ili hila isipate kutia mkono wake katika hukumu hii.

Kwa vyo vyote itakavyokuwa, kinachotolewa hukumu siku ya leo sio shauri au mashauri yaliyoko mbele ya Mahakama, bali haki ndiyo itakayotolewa hukumu. Kwa maneno mengine, 'Haki iko katika Hukumu' ('Justice is on Trial')! Watanzania wanaisubiri sana hukumu hii. Jumuiya ya Kimataifa nayo inaisubiri sana hukumu hii. Waombaji wanasubiri jibu kutoka kwa Mungu!

Tunapoendelea kusubiri kusomwa kwa hukumu hii, hebu tuimbe sote 'Pambio ya Haki na Hukumu' kama ilivyotungwa na kuimbwa na Mfalme na Nabii Daudi katika Zaburi 101.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani.
Huyu Askofu kwa unafiki yuko vizuri,anamtaja Bashiru na kumpa sifa ya kutamka CCM inalindwa na dola kubaki madarakani lakini hamtaji Mbowe kwa sifa yake ya kuwatahadharisha wagombea Uenyekiti wa Chadema Taifa kwamba,' Sumu haionjwi kwa Ulimi'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu mbariki Baba Askofu
 
Kwanini umpangie cha kuongea, kama na wewe unaona mbowe alikosea kwanini usitamke?
 
Mimi CCM damudamu, ila MBOWE ni jembe na kiongozi mstahimilivu.

Wanalumumba tumezoea kumuita DJ, but huyu DJ ni genious haswaa kuzidi PhD kadhaa tulizo nazo hapa Lumumba
 
Barikiwa na Bwana! Sote tuseme Ameni
 
Huyu Askofu kwa unafiki yuko vizuri,anamtaja Bashiru na kumpa sifa ya kutamka CCM inalindwa na dola kubaki madarakani lakini hamtaji Mbowe kwa sifa yake ya kuwatahadharisha wagombea Uenyekiti wa Chadema Taifa kwamba,' Sumu haionjwi kwa Ulimi'

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa hilo la Mbowe ndio lilikuwa fumbo ambalo vichwa maji wengi wa lumumba hamkulielewa, sio ile kauli ya Bashiru mnalindwa na dola, tena akatoa mpaka mifano ya vyama vya nchi nyingine vilivyofanya uzembe vikashindwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Askofu kwa unafiki yuko vizuri,anamtaja Bashiru na kumpa sifa ya kutamka CCM inalindwa na dola kubaki madarakani lakini hamtaji Mbowe kwa sifa yake ya kuwatahadharisha wagombea Uenyekiti wa Chadema Taifa kwamba,' Sumu haionjwi kwa Ulimi'

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu utakuwa ni ugoro wa moto, harufu yake inatia kinyaa!

Kama huna cha kuandika wewe potezea tu mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom