Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,917
Leo tarehe 10 Machi 2020 ni siku ambayo Mahakama ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam itatoa hukumu katika Kesi ya Uchochezi inayowakabili Viongozi Waadamizi wa CHADEMA akiwemo Mbunge wa Hai ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho na Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mheshimiwa Freeman Mbowe.
Hii itakuwa ni 'Hukumu ya Kihistoria' katika nchi yetu na kwa vyo vyote itakavyokuwa, hukumu hii italeta msisimko mpya katika Sheria za Tanzania na Siasa za Tanzania kwa ujumla. Hii ni kesi iliyobeba maslahi mapana kwa taifa hasa ikizingatiwa kuwa inawahusu Viongozi Wakuu wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini na ikitolewa katika mwaka ambao nchi inafanya Uchaguzi Mkuu.
Kwa vyo vyote vile, hukumu hii itaweza kujibu swali muhimu kuhusu 'Uhuru wa Mahakama' za Tanzania kwa upande mmoja na 'Ukomavu wa Demokrasia' kwa upande mwingine. Uhuru wa Mahakama utaweza kupimwa katika maeneo mawili. Je, uamuzi wa hakimu utaathiriwa na hisia za wafuasi wa CHADEMA pamoja na Watanzania wengine wanaofikiri kuwa hiyo ni kesi ya kisiasa? Au, Je! 'Uhuru wa Mahakama' utaathiriwa na 'mashinikizo kutoka juu'? Je, Mahakama itaweza kutenda haki pasipo kuathiriwa na mashinikizo kutoka katika pande hizo zote mbili?
Kwa vyo vyote vile, huu ni mtihani mgumu sana katika nchi yetu! Ni mtihani kwa Hakimu aliyesikiliza kesi, ni mhithani kwa Sheria zetu, ni mtihani kwa Katiba yetu, ni mtihani kwa Mahakama kwa ujumla wake, ni mtihani kwa CHADEMA, ni mtihani kwa Upinzani nchini, ni mtihani kwa Serikali, ni mtihani kwa CCM ambayo hivi karibuni Katibu Mkuu wake amesikika akisema kuhusu kutumia dola ili kubaki madarakani, ni mtihani kwa umoja na mshikamano nchini, na mtihani kwa wanasiasa wote.
Mimi kama Askofu nimemuomba sana Mungu kuhusiana na jambo hili. Nimemuombea Hakimu pamoja na jopo lake ili watende haki pasipo hofu, huba, woga wala upendeleo. Nimewaombea watuhumiwa ili wawe na utulivu katika mioyo yao. Nimewaombea wafuasi wa CHADEMA ili wawe na utulivu. Pia, nimemuomba Mungu ili hila isipate kutia mkono wake katika hukumu hii.
Kwa vyo vyote itakavyokuwa, kinachotolewa hukumu siku ya leo sio shauri au mashauri yaliyoko mbele ya Mahakama, bali haki ndiyo itakayotolewa hukumu. Kwa maneno mengine, 'Haki iko katika Hukumu' ('Justice is on Trial')! Watanzania wanaisubiri sana hukumu hii. Jumuiya ya Kimataifa nayo inaisubiri sana hukumu hii. Waombaji wanasubiri jibu kutoka kwa Mungu!
Tunapoendelea kusubiri kusomwa kwa hukumu hii, hebu tuimbe sote 'Pambio ya Haki na Hukumu' kama ilivyotungwa na kuimbwa na Mfalme na Nabii Daudi katika Zaburi 101.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani.