Askofu Munga: Mkataba wa Bandari umetusaidia kuwajua Viongozi zaidi

B5B26A7A-8CF3-4A45-8953-8F51DE0D3E22.jpeg
FB3CD0D6-2440-41F4-B040-1161ACFBD183.jpeg
9199D8B0-B7E6-43D6-AD0E-6CA3CCD66E4B.jpeg
 
Mzee Wasira anasemaje? Mzee Malecela is fully supporting the move ya mama. Ila ikumbukwe alifanyiwa ikhisani sana kwenye msiba wa mwanaye.
Duh...nakumbuka kuna siku Ndugai alisema malecela alimwita akamwambia mdogo wangu jiuzulu tuu uspika na Ndugai akatii Bila kuuliza swali..

Pia nikiwa mdogo nilisikia Mzee alipewa ndefu ili tuingie OIC Naye akataka kubadili Imani yake kabisa..Yaani TZ ukiwa makini wa kufuatilia matukio ni episodes zimenyooka...hakuna kinachotokea kwa bahati mbaya Tanzania ... Everything is well calculated.
 
Muhimu kutafakari kabla ya Kuchangia.
[emoji4][emoji4]
Utafakarije utumbo ambao uko fully one sided? Hakuna mkataba mbovu kuliko ule wa kanisa na serikali juu makanisa kuchotewa kodi zetu kifisadi. Utaisha lini?
 
Mzee wangu Munga Mungu akubariki kwa ujumbe mzito
Wiki ijayo tukionana ile njia ya mtoni ukifanya mazoezi ntakupa mkono
 
Ujumbe mzito na wenye kueleweka kwa wenye akili, kutoka kwa Askofu Dr. Munga
 
yule mama ni mshenzi sana, hao waarabu sijajua wamempa nini hadi ameanza kufanya mambo ya ajabu katika nchi kiasi hiki..!!
Ameonekana kwenye burj Khalifa na sikia picha yako kuonekana hapo sio mchezo
 
Alianza na Ngorongoro Taratibu kila mtu ataguswa.v
 
Hii kitu inajisimamia bila kuingiza michanyato ya IMANI; nashauri isimame yenyewe kama yenyewe.....; sababu mustakabali wa Taifa haijalishi wewe kama ni shetani au malaika kwa macho ya huyu au yule...
 
Nimekuelewa vizuri kabisa Kiongozi wangu. Tupo pamoja mpaka mwisho.
 
Ameandika Baba Askofu Stephen Munga

MKATABA WA BANDARI UMETUSAIDIA KUJUANA ZAIDI

"Na hivi ndivyo tunavyoweza kutambua wazi kati ya walio watoto wa Mungu na walio watoto wa shetani. Mtu ye yote asiyetenda lililo haki si wa Mungu; wala asiyempenda ndugu yake si wa Mungu."
(1 Yohana 3:10)

Kwanza, Nimekubali kuwa ndugu hujuana vizuri wakati wa matatizo na migogoro. Hata uliodhani wanakuheshimu utawasikia wakikutukana. Wasiostahil8 kutukana walijaribu kumvunjia heshima Profesa Shivji wakisahau kwamba wapo watu heshima zao hazivunjwi kirahisi.

Pili, Mgogoro wa bandari umetufanya tujuane vizuri Watanzania. Baadhi ya watu walitiwa kiza fahamu na adabu zao wakabaki kama waliosimama uchi hadharani. Tukumbuke kuwa kujaribu kufunika ukweli na kufukia haki ni kama kuzima moto kwa petroli.

Tatu, Uzalendo na maadili mema tuliyojidai tunataka kuyajenga katika jamii yetu juhudi hizo tumezimwagia matope. Hata viongozi wa dini wenye dhamana ya kuadibisha jamii wametumika kwa uongo na majungu. Utamwambiaje mtoto asitukane wakati mwenyewe ni mtukanaji. Tusiwaharibie watoto maisha kwa ajili ya ulafi wa leo.

Nne, Tumedhalilishana kwa hoja zisizo na ufahamu wa kina. Wapo watu ambao akipewa kipande cha mkate aweza kutukana kijiji kizima. Hekima ni pamoja na kujua la kuzungumza kwa wakati ufaao na kwa kiasi kifaacho.

Hitimisho, hivi ni vita vikubwa kwani ni mvutano baina ya kweli na uongo; haki na dhuluma; wema na uovu; giza na nuru; na uzalendo na usaliti. Mpaka tutakapofika mwisho tutakuwa tumejuana vizuri. Kwamba asiyetenda lililo haki si wa Mungu; wala asiyempenda ndugu yake si wa Mungu.
 
Brother huwezi kupewa Majibu. Tuliambiwa mama anaupiga Mwingi ila sasa baada ya kukosa majibu ya kuuza bandari zetu zote wamekuja na slogan mpya mama Mtulivu ila ukweli ni kwamba hana majibu baada ya uotopolo aliotufanyia watanganyika
 
Back
Top Bottom