Askofu Mwamakula amtaja Gerald Hando shujaa wa maoni 2022

saidoo25

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
624
Reaction score
1,456
GERALD HANDO ATAJWA NA ASKOFU KUWA SHUJAA WA UHURU WA MAONI WA 2022.

Wamiliki wa vyombo vya habari vya Tanzania na wahariri wamewekwa mfukoni na serikali, wanajikomba na wanajipendekeza kwa serikali.

Mtangazaji wa EFM na TVE, Gerald Hando ameadhibiwa na mmiliki wake kwa kauli yake ya kukosoa tabia ya serikali ya kukopa fedha. EFM inataka watangazaji wake wawe wanasifia serikali wasiwe wanakosoa. EFM haijui wajibu wa wanahabari kwa umma. Ni aibu kubwa sana kuwa na vyombo vya habari vinavyojikomba na kujipendekeza serikalini.

Ndugu Gerald Hando anatajwa na Askofu Mwamakula kuwa shujaa wa 31 Desemba 2022 kwa kutoa maoni yake bila kuogopa na kukosoa serikali bila hofu!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

21314597_863902927097614_141664816224741445_n.jpg
 
Askofu anaishi kwa sadaka, Gerald Hando unategemea mshahara, kila chombo cha habari kina policy zake na malengo. Askofu asijaze watu ujinga.
 
Tatizo la nchi zetu za kiafrika mnamuita mwenzenu shujaa kule kazini kwake anafukuzwa kwa mkono wa serikali na kukosesha wanae mkate wa siagi.
Majizo alikuwa Dj tu kama kina Dj Nelly tu, Sasa mtu mwenye akili ni lazima ujiulize amepata wapi ghafla pesa ya kumiliki media house yake?

Unapokiona kinyago kwenye display ujuwe kuna Wamakonde wamekichonga.
 
Maisha yetu yanazidi kuwa magumu pale ambapo tunalazimishwa tuishi kama mazezeta, tuende kinyume na fikra zetu kwa kuogopa kushughulikiwa na ofisi zetu pale tutapotoa maoni yatakayowakera watawala.

Hali hii inaonesha bado kama taifa tunaishi kwenye utumwa wa kifikra, na wakoloni wetu ni CCM na viongozi wao, hapa ndipo walipotufikisha, wameshindwa kumpiga vita adui ujinga miaka zaidi ya sitini, sasa kwa nguvu wameamua sote kwa pamoja kama taifa tujiunge nae, kazi kwetu kuanzisha mapambano mapya ya kumuondoa mkoloni mweusi.
 
Tatizo la nchi zetu za kiafrika mnamuita mwenzenu shujaa kule kazini kwake anafukuzwa kwa mkono wa serikali na kukosesha wanae mkate wa siagi.
Halafu wala hatumchangii ili watoto wake waendelee kwenda shule.

Sasa nachukua fursa hii kuwaomba watanzania wote tumchangie mwenzetu Gerad Hando aliyefukuzwa kazi kwa uonevu baada ya kutoa maoni yake.

Mnasemaje?????
 
Kanisa lake liko wapi? Sio mtu wa Mbeya huyo Askofu? Mbeya ndio kunaongoza kwa upumbavu wa makanisa ya kisasa. Kila nyumba Askofu, mwili hana, amevaa sijui nn kichwani huyo kichaa.
 
Asiishie hapo tu, amweke kwenye orodha ya wanufaika wa sadaka Kanisani kwake.
 
GERALD HANDO ATAJWA NA ASKOFU KUWA SHUJAA WA UHURU WA MAONI WA 2022.

Wamiliki wa vyombo vya habari vya Tanzania na wahariri wamewekwa mfukoni na serikali, wanajikomba na wanajipendekeza kwa serikali.

Mtangazaji wa EFM na TVE, Gerald Hando ameadhibiwa na mmiliki wake kwa kauli yake ya kukosoa tabia ya serikali ya kukopa fedha. EFM inataka watangazaji wake wawe wanasifia serikali wasiwe wanakosoa. EFM haijui wajibu wa wanahabari kwa umma. Ni aibu kubwa sana kuwa na vyombo vya habari vinavyojikomba na kujipendekeza serikalini.

Ndugu Gerald Hando anatajwa na Askofu Mwamakula kuwa shujaa wa 31 Desemba 2022 kwa kutoa maoni yake bila kuogopa na kukosoa serikali bila hofu!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

View attachment 2465873
Gerald Hando ni form IV leaver hana elimu yeyoye kwenye sekta ya habari au kwenye uchumi. Hajui vigezo vya kukopa ni vipi katika level ya nchi. Tanzania mpaka sasa haipo kwenye nchi 20 zenye mikopo mibaya. Wataalamu huangalia mikopo kwa kutumia index inaitwa debt/equity ratio au debt/ gdp ratio. Jedwali lifuatalo linaonyesha nchi za Afrika zenye ratio mbaya:
Screenshot_20230101-204529.png
Screenshot_20230101-204514.png
 
Halafu wala hatumchangii ili watoto wake waendelee kwenda shule.

Sasa nachukua fursa hii kuwaomba watanzania wote tumchangie mwenzetu Gerad Hando aliyefukuzwa kazi kwa uonevu baada ya kutoa maoni yake.

Mnasemaje?????
Ila nasi tumchangie kwa siri tusipoteze ugali huku kwetu akakosa wa kumchangia.
 
Tatizo la nchi zetu za kiafrika mnamuita mwenzenu shujaa kule kazini kwake anafukuzwa kwa mkono wa serikali na kukosesha wanae mkate wa siagi.
Maisha yetu yanazidi kuwa magumu pale ambapo tunalazimishwa tuishi kama mazezeta, tuende kinyume na fikra zetu kwa kuogopa kushughulikiwa na ofisi zetu pale tutapotoa maoni yatakayowakera watawala.

Hali hii inaonesha bado kama taifa tunaishi kwenye utumwa wa kifikra, na wakoloni wetu ni CCM na viongozi wao, hapa ndipo walipotufikisha, wameshindwa kumpiga vita adui ujinga miaka zaidi ya sitini, sasa kwa nguvu wameamua sote kwa pamoja kama taifa tujiunge nae, kazi kwetu kuanzisha mapambano mapya ya kumuondoa mkoloni mweusi.
The best way kwa Gerald Hando kama mtangazaji wa kipindi angemualika mtaalamu wa uchumi na fedha kutoka kwenye vyuo bobezi kama UDSM, IFM au Mzumbe halafu yeye awe anauliza maswali then mtaalamu ndiyo a make opinion. Ila yeye kuongea mambo ya kijiweni kwenye ulevi ni kutomtendea haki mwajiri wake.

Mwamakula naye amepinda tu kama mateja yanayovuta unga. Yeye Hana kanisa wala waumini popote japo anaitwa Askofu wa Moravian Uamsho
 
Ila mwamakula amekonda jamani, na Ile kofia ya uaskofu sijui huwa anaigundisha na gundi pale kichwani
 
Tatizo la nchi zetu za kiafrika mnamuita mwenzenu shujaa kule kazini kwake anafukuzwa kwa mkono wa serikali na kukosesha wanae mkate wa siagi.
Ni shujaa lkn!..mkate unaodhani wewe ni upofu wa fikra tu.
 
GERALD HANDO ATAJWA NA ASKOFU KUWA SHUJAA WA UHURU WA MAONI WA 2022.

Wamiliki wa vyombo vya habari vya Tanzania na wahariri wamewekwa mfukoni na serikali, wanajikomba na wanajipendekeza kwa serikali.

Mtangazaji wa EFM na TVE, Gerald Hando ameadhibiwa na mmiliki wake kwa kauli yake ya kukosoa tabia ya serikali ya kukopa fedha. EFM inataka watangazaji wake wawe wanasifia serikali wasiwe wanakosoa. EFM haijui wajibu wa wanahabari kwa umma. Ni aibu kubwa sana kuwa na vyombo vya habari vinavyojikomba na kujipendekeza serikalini.

Ndugu Gerald Hando anatajwa na Askofu Mwamakula kuwa shujaa wa 31 Desemba 2022 kwa kutoa maoni yake bila kuogopa na kukosoa serikali bila hofu!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

View attachment 2465873
Ushujaa wake aufanye akiwa na ofisi yake hizo ni biashara za watu
 
Back
Top Bottom