Askofu Mwamakula amtaja Gerald Hando shujaa wa maoni 2022

Askofu Mwamakula amtaja Gerald Hando shujaa wa maoni 2022

Halafu wala hatumchangii ili watoto wake waendelee kwenda shule.

Sasa nachukua fursa hii kuwaomba watanzania wote tumchangie mwenzetu Gerad Hando aliyefukuzwa kazi kwa uonevu baada ya kutoa maoni yake.

Mnasemaje?????
Weka account No. au tafuta namba yake ya simu tumdondoshee mpunga.
 
The best way kwa Gerald Hando kama mtangazaji wa kipindi angemualika mtaalamu wa uchumi na fedha kutoka kwenye vyuo bobezi kama UDSM, IFM au Mzumbe halafu yeye awe anauliza maswali then mtaalamu ndiyo a make opinion. Ila yeye kuongea mambo ya kijiweni kwenye ulevi ni kutomtendea haki mwajiri wake.

Mwamakula naye amepinda tu kama mateja yanayovuta unga. Yeye Hana kanisa wala waumini popote japo anaitwa Askofu wa Moravian Uamsho
Mkuu kila kitu mtaalam, tutaitendeaje haki katiba inayotupa uhuru kujadiri issue tofauti?
 
Majizo alikuwa Dj tu kama kina Dj Nelly tu, Sasa mtu mwenye akili ni lazima ujiulize amepata wapi ghafla pesa ya kumiliki media house yake?

Unapokiona kinyago kwenye display ujuwe kuna Wamakonde wamekichonga.
Fikra za kimaskini.
 
Umeingia chaka jingine. Aliyekuwa askofu wa Jimbo la Mbulu ni Babu yake ambaye alikufa about 15 years ago. All in all utajuri wa askofu hauingii kwenye familia
Unaingia, kwa hiyo aliondoka na mali zake akazikwa nazo?
 
GERALD HANDO ATAJWA NA ASKOFU KUWA SHUJAA WA UHURU WA MAONI WA 2022.

Wamiliki wa vyombo vya habari vya Tanzania na wahariri wamewekwa mfukoni na serikali, wanajikomba na wanajipendekeza kwa serikali.

Mtangazaji wa EFM na TVE, Gerald Hando ameadhibiwa na mmiliki wake kwa kauli yake ya kukosoa tabia ya serikali ya kukopa fedha. EFM inataka watangazaji wake wawe wanasifia serikali wasiwe wanakosoa. EFM haijui wajibu wa wanahabari kwa umma. Ni aibu kubwa sana kuwa na vyombo vya habari vinavyojikomba na kujipendekeza serikalini.

Ndugu Gerald Hando anatajwa na Askofu Mwamakula kuwa shujaa wa 31 Desemba 2022 kwa kutoa maoni yake bila kuogopa na kukosoa serikali bila hofu!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula



View attachment 2465873
Unadai uhuru wa vyombo vya habari wakati ndani ya chombo cha habari hakuna uhuru. Vyombo vya habari vimebakia kujikomba kwa serikali, kusifiasifia tu ili wapate teuzi. Hakuna weledi kabisa wa uandishi
 
Kuna MOAT ya enzi hizo iko chini ya Mzee Mengi na kuna hii ya akina Kusaga, Majizo na Diamond.
 
Back
Top Bottom