Askofu Mwamakula amtaja Gerald Hando shujaa wa maoni 2022

GERALD HANDO ATAJWA NA ASKOFU KUWA SHUJAA WA UHURU WA MAONI WA 2022.

Wamiliki wa vyombo vya habari vya Tanzania na wahariri wamewekwa mfukoni na serikali, wanajikomba na wanajipendekeza kwa serikali.

Mtangazaji wa EFM na TVE, Gerald Hando ameadhibiwa na mmiliki wake kwa kauli yake ya kukosoa tabia ya serikali ya kukopa fedha. EFM inataka watangazaji wake wawe wanasifia serikali wasiwe wanakosoa. EFM haijui wajibu wa wanahabari kwa umma. Ni aibu kubwa sana kuwa na vyombo vya habari vinavyojikomba na kujipendekeza serikalini.

Ndugu Gerald Hando anatajwa na Askofu Mwamakula kuwa shujaa wa 31 Desemba 2022 kwa kutoa maoni yake bila kuogopa na kukosoa serikali bila hofu!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

View attachment 2465873
Opinion ya Hando ni nzuri sana na ndio kipimo cha upumbavu wa Tanzania, kama ishu Ina majibu kuna haja gani hofu na kuchukia, wanavyokopa na kukopeshwa wanavigezo na sababu zao hofu na wasiwasi wa nini hii nchi Ina upumbavu mwingi sana
 
Ila nasi tumchangie kwa siri tusipoteze ugali huku kwetu akakosa wa kumchangia.
Yaah! Ni kweli. Misisiemu haikawii Kuna kubomoa banda lako la biashara ama kukufukuza kazi kwasab ya kumchangia Hando
 
Gerald Hando ni form IV leaver hana elimu yeyoye kwenye sekta ya habari au kwenye uchumi. Hajui vigezo vya kukopa ni vipi katika level ya nchi. Tanzania mpaka sasa haipo kwenye nchi 20 zenye mikopo mibaya. Wataalamu huangalia mikopo kwa kutumia index inaitwa debt/equity ratio au debt/ gdp ratio. Jedwali lifuatalo linaonyesha nchi za Afrika zenye ratio mbaya:
View attachment 2465980View attachment 2465981
Jibuni hoja yake badala ya kulialia
 
Tatizo la nchi zetu za kiafrika mnamuita mwenzenu shujaa kule kazini kwake anafukuzwa kwa mkono wa serikali na kukosesha wanae mkate wa siagi.
Hivi mnavyo viona ni vita vya kidini ila vipo katika hatua ya vita baridi kuelekea vita ya moto
 
The best way kwa Gerald Hando kama mtangazaji wa kipindi angemualika mtaalamu wa uchumi na fedha kutoka kwenye vyuo bobezi kama UDSM, IFM au Mzumbe halafu yeye awe anauliza maswali then mtaalamu ndiyo a make opinion. Ila yeye kuongea mambo ya kijiweni kwenye ulevi ni kutomtendea haki mwajiri wake.

Mwamakula naye amepinda tu kama mateja yanayovuta unga. Yeye Hana kanisa wala waumini popote japo anaitwa Askofu wa Moravian Uamsho
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]Yani nimecheka. Kumbe huyu askofu Hana kanisa Wala waumin,,[emoji16][emoji16][emoji16]ana kofia na fimbo tuu?? It's high time serikali iangazie leseni za makanisa, na viongoz wa hayo makanisa
 
Emmanuel Bandekile Mwamakula ni Tapeli tu kama tapeli yeyote unayomfahamu. Wenzie wa Moravian Mbeya walimtimua walipoona ni mdokozi wa sadaka
 
Jibuni hoja yake badala ya kulialia
Kwani Mkuu hujaona hoja hapo kwenye majedwali niliyokuwekea?
Maoni hayakatazwi na wala hawezi kupata shida kwa hilo. Tatizo yeye ni mtangazaji ni kutumia chombo cha mwajiri vibaya kuelezea maoni binafsi.

Kama unajuwa newsrooms zina watu wanaitwa News Editors, ndiyo wenye kazi za kuchuja habari ili wananchi wapate habari ambazo ziko na maadili na haziko biased.

Bunge lilipitisha Bajeti ya Tsh 42 Trllioni yenye nakisi dhidi ya mapato ya Tsh 19 Trillion, je Gerald Hando anadhani nakisi itazibwa na nini?

Miradi mikubwa ya SGR, JNHEPP, Busisi na Makao Makuu Dodoma ndiyo vinakula sehemu kubwa ya mikopo. Je tuache hiyo miradi isikamilike mpaka tupate makusanyo yetu ndiyo tujenge?
 
Emmanuel Bandekile Mwamakula ni Tapeli tu kama tapeli yeyote unayomfahamu. Wenzie wa Moravian Mbeya walimtimua walipoona ni mdokozi wa sadaka
Mtu akiwa na mawazo tofauti na weye usimchukie.Hizo sadaka alidokoa lini na kiasi gani?
 
The best way kwa Gerald Hando kama mtangazaji wa kipindi angemualika mtaalamu wa uchumi na fedha kutoka kwenye vyuo bobezi kama UDSM, IFM au Mzumbe halafu yeye awe anauliza maswali then mtaalamu ndiyo a make opinion. Ila yeye kuongea mambo ya kijiweni kwenye ulevi ni kutomtendea haki mwajiri wake.

Mwamakula naye amepinda tu kama mateja yanayovuta unga. Yeye Hana kanisa wala waumini popote japo anaitwa Askofu wa Moravian Uamsho
Unampangia namna ya kufanya kazi?Umesikia ni sinema hiyo hadi upange scenes?
 
Gerald Hando ni form IV leaver hana elimu yeyoye kwenye sekta ya habari au kwenye uchumi. Hajui vigezo vya kukopa ni vipi katika level ya nchi. Tanzania mpaka sasa haipo kwenye nchi 20 zenye mikopo mibaya. Wataalamu huangalia mikopo kwa kutumia index inaitwa debt/equity ratio au debt/ gdp ratio. Jedwali lifuatalo linaonyesha nchi za Afrika zenye ratio mbaya:
View attachment 2465980View attachment 2465981
Kama ni form 4 leaver, mbona mnaangaika nae?
 
Gerald Hando ni form IV leaver hana elimu yeyoye kwenye sekta ya habari au kwenye uchumi. Hajui vigezo vya kukopa ni vipi katika level ya nchi. Tanzania mpaka sasa haipo kwenye nchi 20 zenye mikopo mibaya. Wataalamu huangalia mikopo kwa kutumia index inaitwa debt/equity ratio au debt/ gdp ratio. Jedwali lifuatalo linaonyesha nchi za Afrika zenye ratio mbaya:
View attachment 2465980View attachment 2465981
Kwa hiyo form 4 leaver ndo hawatakiwi kutoa maoni kuhusu uchumi? Mmeishiwa akili Hadi za kuendea chooni!?
 
Gerald Hando ni form IV leaver hana elimu yeyoye kwenye sekta ya habari au kwenye uchumi. Hajui vigezo vya kukopa ni vipi katika level ya nchi. Tanzania mpaka sasa haipo kwenye nchi 20 zenye mikopo mibaya. Wataalamu huangalia mikopo kwa kutumia index inaitwa debt/equity ratio au debt/ gdp ratio. Jedwali lifuatalo linaonyesha nchi za Afrika zenye ratio mbaya:
View attachment 2465980View attachment 2465981
We utakuwa chizi, Hando ana degree ya software engineering, we una usomi wako umesaidia nini taifa?
 
Back
Top Bottom