Uchaguzi 2020 Askofu Mwamakula: Ninakwenda katika msafara wa Lissu pamoja na uwezekano wa kupigwa mawe au kurushiwa mabomu na risasi

Iwe kwa damu ama maji mwaka huu ikulu ni yetu wazarendo wa kweli wa taifa hili.
 
Askofu amejijengea heshima kwa kuendelea kuihubiri haki kwa vitendo, abarikiwe sana.

Wengine wanashindwa hata kutoa kauli tu za kukemea hayo matendo ya kihuni anayofanyiwa Lissu, wanatakiwa kuona aibu sasa, wajue dunia inawatazama.
Nitaanza kwenda kanisani tena siku nitakapoona maaskofu wa Kanisa Katoliki wakikemea vitendo viovu vya magufuli hadharani bila kupepesa macho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sauti ya mtumishi huyu wa Mungu ni sauti ya Mungu mwenyewe. Sauti ya wengi ni sauti pia ya Mungu, kwa kila aina visa na vitimbwi wanayomfanyia Tundu Lissu ndiyo ambavyo inazidi kumfanya kuwa imara na kumjengea umaarufu zaidi.

Uchaguzi huu ni "replica" ya mpambano kati ya mfalme Sauli na Daudi. Mmoja ijapokuwa yupo madarakani, lakini Mungu amemkataa, lakini mwingine ndiye mpakwa mafuta wa BWANA. Hongera sana askofu Mwamakula kwa kusimamia upande sahihi wa maono ya Mungu wetu Muumba.
Kwenye uchaguzi wa mwaka 2000 Askofu Kakobe alikuwa anatembea na Mgombea Urais Augustine Lyatonga Mrema akidai kuwa NDIYE Rais aliyetabiriwa! Leo yupo huyu!! Ahahahahahaah!!!
 
Nilikuwa nasikia watu wanachukuliwa kwenda kwenye kampeni leo nimeshuhudia mwenyewe

Kikubwa tujuze uwanja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi kujaza uwanja Kuna faida gani? CCM wameishiwa kabisa.
Leo weeeeengi wameletwa Kawe kea mabasi, jamaa HATA hajamaliza kuongea watu wakaanza kuelekea Beach.
 
Attachments

  • Screenshot_20201014-215639.png
    Screenshot_20201014-215639.png
    116.1 KB · Views: 1
Itumie vizuri akili uliyopewa na Muumba, huyu Askofu na yule gwajiboy ni watu wawili tofauti.

Askofu anakemea maovu hajajiingiza kwenye siasa yupo neutral lakini gwajiboy amejiingiza kwenye siasa maana ni mgombea ubunge kupitia chama cha mapinduzi chama ambacho kinatenda maovu bila kujari bila aibu.
Narudia tena wote ni wapumbv.... dini na siasa havitakiwi kuchanganywa. Ni lazima wachague moja.
 
Ya kaisari ampe kaisari, na ya Mungu ampe Mungu wa kweli. Ila kama ni tumbo lake, kila la kheri maana ndio msingi wa ukamanda wa chama cha Mbowe.
Tumbo?? Chadema wanaaccess ya kuchota hazina
 
Ya kaisari ampe kaisari, na ya Mungu ampe Mungu wa kweli. Ila kama ni tumbo lake, kila la kheri maana ndio msingi wa ukamanda wa chama cha Mbowe.

Ma-CCM acheni kuwafanya Watz hawana akili. Yaani Askofu, padre au mchungaji akikemea UOVU unaofanywa na Polisi kwa Raia mnamwambia ni mchochezi au siyo MZALENDO.......!??
Hivi Askofu Gwajima anagombea Ubunge Kawe kama Askofu au Mwanasiasa???
Lakini pia kuna marehemu Askofu Dk. Rwakatare alikuwa Mbunge wa Kuteuliwa na CCM sijui alikuwa anavua Uaskofu akiingia Bungeni au???
 
NINAKWENDA KATIKA MSAFARA WA LISSU PAMOJA NA UWEZEKANO WA KUPIGWA MAWE AU KURUSHIWA MABOMU NA RISASI!

Wiki iliyopita Jeshi la Polisi lilizuia Msafara wa Mheshimiwa Lissu eneo la Kiluvya jijini Dar es Salaam pasipo sababu za msingi kwani kama kungelikuwa na ukiukwaji wa taratibu za Kampeni basi Tume ingelimchukulia hatua. Nilipokwenda kumuona, Polisi waliokuwa na silaha walinitisha wakitaka kunizua nisiende kumuona Lissu. Kilikuwa ni kituko cha aina yake! Utamzuiaje kwa kumtisha Askofu huru katika nchi huru ili kumkataza kumuona raia huru katika mazingira huru? Walilenga kuficha nini kwa Askofu na kwa jumuiya ya kimataifa? Watu wengi hawajui kuwa Askofu ni jicho pia la Jumuiya ya Kimataifa katika nchi ye yote ile. Vitisho na zuio lao hata hivyo havikufanikiwa!

Jana tarehe 13 Oktoba 2020, nilipata muda wa kuongea kwa simu na baadhi ya walinzi wa Lissu baada ya kupata taarifa kuhusu shambulio dhidi ya Mheshimiwa Lissu kule Chato! Mmoja alikuwa ana maumivu makali katika bega baada ya kurushiwa mawe. Niliarifiwa kuwa watu kadhaa waliumizwa katika tukio lile.

Bado tunajiuliza maswali mengi kuhusu vurugu za Chato na Geita kwa ujumla dhidi ya Mheshimiwa Lissu. Hivi inakuwaje Mgombea Urais kufanyiwa chuki na vurugu kubwa kama zile nyumbani kwa Rais? Hivi ni nani na nini kilichokuwa nyuma ya hayo yote? Je, ni wivu, uhuni, chuki, wivu, au ukabila? Hiki ni kiashirio gani katika eneo ambalo asilimia kubwa ya wakazi wake ni Wakristo? Viongozi wakuu wa Kanisa katika Mkoa wa Geita wamelichukuliaje jambo hilo?

Tangu kampeni zianze, Lissu na Mgombea Mwenza wake wamekuwa wakilengwa kwa vurugu dhidi yao kutoka kwa makundi yanayoandaliwa kimkakati. Kama hilo halitoshi, manyanyaso kutoka Jeshi la Polisi katika baadhi ya maeneo na mikakati ya Tume kuengua Wagombea wa CHADEMA na ACT Wazalendo vimetumika kama mbinu ya kudhoofisha na kuhujumu upinzani katika Uchaguzi huu. Hii si HAKI hata kidogo.

Kama Askofu ninakemea vitendo hivyo na ninaomba viongozi wote wa dini tukiwa kama sauti ya maadili nchini tuungane katika kuonya na kukemea uovu huu na uporaji wa haki nchini.

Pamoja na vitisho hivyo, nipo njiani kwenda katika Msafara wa Mheshimiwa Lissu. Haki huinua taifa!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

+Emmmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.

Pamoja[emoji109]
 
Huyu ni

Huyu ni Askofu Tutu wa Tanzania
 
Narudia tena wote ni wapumbv.... dini na siasa havitakiwi kuchanganywa. Ni lazima wachague moja.

You can't serve two Masters at one time! But both politics and religions move together, you can't separate them.
Ndo maana tuna Balozi wa Pope toka Vatican hapa Tanzania na Serikali ya Tanzania ina Ubalozi wake huko Vatican.
Kanisa linapojenga Hospitals, Shule na Vyuo halifanyi siasa baali linatoa huduma kwa Jamii na KULIPA Kodi.
Kinachoshangaza Tanzania ni pale Kanisa linapoanza kukemea maovu na kukosoa Wanasiasa linaambiwa liache Siasa.....ebho? Huu ni uwendawazimu!!
Gwajima ana platform yake ya kuisemea na kuikosoa Serikali AKIWA KANISANI KWAKE na siyo kuomba KURA KWENDA BUNGENI....That's a BIG NO!!
 
Ma-CCM acheni kuwafanya Watz hawana akili. Yaani Askofu, padre au mchungaji akikemea UOVU unaofanywa na Polisi kwa Raia mnamwambia ni mchochezi au siyo MZALENDO.......!??
Hivi Askofu Gwajima anagombea Ubunge Kawe kama Askofu au Mwanasiasa???
Lakini pia kuna marehemu Askofu Dk. Rwakatare alikuwa Mbunge wa Kuteuliwa na CCM sijui alikuwa anavua Uaskofu akiingia Bungeni au???
Uzalendo ni kupiga watu risasi
 
You can't serve two Masters at one time! But both politics and religions move together, you can't separate them.
Ndo maana tuna Balozi wa Pope toka Vatican hapa Tanzania na Serikali ya Tanzania ina Ubalozi wake huko Vatican.
Kanisa linapojenga Hospitals, Shule na Vyuo halifanyi siasa baali linatoa huduma kwa Jamii na KULIPA Kodi.
Kinachoshangaza Tanzania ni pale Kanisa linapoanza kukemea maovu na kukosoa Wanasiasa linaambiwa liache Siasa.....ebho? Huu ni uwendawazimu!!
Gwajima ana platform yake ya kuisemea na kuikosoa Serikali AKIWA KANISANI KWAKE na siyo kuomba KURA KWENDA BUNGENI....That's a BIG NO!!
Wakisifia wanaitwa viongozi wa dini wakikemea maovu wanaitwa siyo wazalendo
 
Huyu ni

Huyu ni Askofu Tutu wa Tanzania
Amina kubwa hapo.
Askofu Desmond Tutu alipigana bega kwa bega na Mzee Nelson Mandela(rip)kutokomeza Ukaburu nchini Afrika Kusini!
Hivo Askofu Mwamakula Yuko sahihi kabisa kwa 100%!!!
 
Back
Top Bottom