Askofu Mwamakula: Ole kwa Taifa lisilotenda HAKI kwa watu wake! Unamkamata mtu eti upelelezi haujakamilika karne hii?

Angesifia msingesema yote haya.
 
Hatuwez kupata maendeleo kitaifa kwa junsi tunavyowatenda wengine! Hakika laana ya kitaifa haiwez kutuacha! Asiye amin haya ni yule asisoma historia
 
Kazi Yake kuu anayotakiwa kufanya Ni ya kumsifu Mungu na kutunga nyimbo na pambio za kumsifu Mungu Sio binafamu
Yehodaya labda makusudi unafanya ?!. Askofu anaongoza jamii hiyo hiyo inayoongozwa na serikali . Anapoona sheria kandamizi zenye elements za kikoloni ni wajibu wake kuzikemea. UtamkamataJe mtu huku upelelezi bado ?! Unamuweka ndani miaka na baadaye inathibitika alionewa. Nani anamlipa muda wake na afya yake alizopoteza ?!.
 
Yesu alitamka wazi kabisa utawala wangu SI wa dunia hii.Ukiona Askofu anajihusisha na mambo ya utawala wa dunia hii huyo SI Askofu wa Yesu
Lakini Yesu huyo huyo alipoambiwa aondoke Galilaya maana Mfalme katili Herode alitaka kumuua alijibu: "Nendeni mumwambie yule mbweha, leo na kesho natoa pepo, nafufua wafu, na siku ya tatu nakamilika." Ililuwa sawa kumwita mfalme 'mbweha!!!?'
 
Ninafurahia sana sheria za nchi ya Kenya! Unamkamata mtu, na mahakama ndiyo yenye mamlaka ya kutoa ruhusa mtuhumiwa akae muda gani mahabusu kama upelelezi haujakamilika na mara nyingi haizidi wiki mbili!
 
Kumbuka, huyu ni kiongozi wa kiroho, na maendeleo kwake ni ya kiroho zaidi kwanza. Kama ujumbe ukiwagusa majaji, mahakimu, mawakili wa upande wa mashtaka na wapelelezi na wakaufanyia kazi, kwake yeye ni hatua kubwa ya maendeleo kuliko akajenga makanisa mengi bila kufanikiwa kubadilisha roho za watu
 
Sometime uwe unatumia akili mkuu. Kuna kitabu kilichoongelea haki ya mtu hapa duniani kuliko biblia?. Wachungaji wanasomea vitu vingi sana hata management and leadership.
Kanisa limefanya kazi kubwa sana kuelimisha jamii ya kitanzania. Viongozi wengi wamesoma shule za kanisa na leo wana uewelewa.
Kanisa likihoji mnasema siasa lakini elimu mnasoma shule zao.
Sometime weka mihemko mbali ona kwa jicho la tofauti utawala wa sasa hivi.
Watu wengi wako gerezani na kuacha shughuli zao hivyo familia zao zinateseka sana
 
Watumishi wa Mungu wanamukomboa mwanadamu ki roho na mwili huwezi kuvitenganisha.Haki za wananchi zinapokanyagwa kwa hajili ya kuwakomoa au kuwabaguwa wale wasiopendwa ni haki ya kila raia regardless ni mtumishi wa Mungu au la kukemea ugandamizaji usiopendwa hata chembe na Mwenyezi Mungu.
 
Wewe ndio umechanganyikiwa na hulijui uandikalo. Askofu anayo haki ya kukemea maovu
 
Wewe umedhulumika nini ? Umebambikiwa kesi !?
 
.....wewe ni mfuasi wa nini ?
 
...wakati wake ukifika kama vile wako utakapo fika. Ufunguo wa 'ghaibu' anao Mungu tu.
ukiwa na damu ya mtu mkononi haisubiri wakayi, nyie endeleeni kuteka, tesa na kuua alafu useme nye nye hapa
 
Lakini Yesu huyo huyo alipoambiwa aondoke Galilaya maana Mfalme katili Herode alitaka kumuua alijibu: "Nendeni mumwambie yule mbweha, leo na kesho natoa pepo, nafufua wafu, na siku ya tatu nakamilika." Ililuwa sawa kumwita mfalme 'mbweha!!!?'
Mbona wayahudi walimwita Yesu 'mwana haramu' !
 
Kazi ya kiongozi wa dini sio kuongelea maovu Ni kuongelea mambo ya Mungu
Ni mambo gani ya Mungu ambayo atayaongelea huku haki ikiminywa? Soma vitabu vitakatifu uone jinsi vinavyokemea maovu katika jamii. Unataka viongozi wa dini hayo wasiyaseme kwa vile wanayoyatenda ni wanasiasa?
 
ukiwa na damu ya mtu mkononi haisubiri wakayi, nyie endeleeni kuteka, tesa na kuua alafu useme nye nye hapa
Labda kama umepewa.mamlaka ya 'kukaimu' ndio mambo yatenda utakavyo wewe !.....endelea tu na nyefu nyefu nyefu !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…