Askofu Mwamakula: Rais Samia, tunakuandikia kuhusu Dkt. Nchimbi, ujumbe uliobeba majonzi, hofu, vilio, minong'ono, masengenyo

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
WARAKA WA KIASKOFU JUU YA DKT NCHIMBI

Mpendwa Mhe. Samia Suluhu Hassan!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
Tunasalimu kwa jina la Mungu aliye hai, Bwana wa mabwana, mfalme wa wafalme na mkuu wa majeshi yote ya mbinguni (The Lord of Hosts) na ambaye kwa rehema zake mimi nimepata neema ya kuisema kweli na haki yake miongoni mwa mtumishi watumishi wake!

Tunatambua ya kuwa uko katika maombolezo kufuatia kifo cha mume wako. Lakini kwa kuwa wewe ndiye Rais na kwa kuwa jambo hili ni zito na linakuhusu wewe, imetubidi tukuandikie!

Mpendwa Rais! Tunakuandikia ujumbe lakini moyo ukiwa mzito sana kuhusu mambo mengi yanavyoendelea katika taifa hili ambalo wewe umepata kuwa mtawala wake katika zama hizi.

Ujumbe huu umebeba muhutsari wa majonzi, hofu, vilio, minong'ono, masengenyo, maneno na hasira za Watanzania walio wengi sana. Hii ni kwa sababu inaonekana hakuna mtu aliye na ujasiri wa kukueleza ukweli wa mambo kwani imedhihirika kuwa watu wanaojaribu kufumbua vinywa vyao kushauri na kuonya hutenguliwa, hutekwa, hupotezwa au hata huuawa!

Leo tunakuandikia kuhusu suala la Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihudumu chini yako. Ninakuandikia wewe juu ya hili kwa sababu ya mazingira yanayohusisha Kiti cha Rais wa Jamhuri au Mwenyekiti wa CCM ambaye ndiye wewe.

Mheshimiwa Rais! Mwaka 2025, wewe na Dkt. Nchimbi mlizunguka nchi nzima kwa ajili ya kupiga kampeni ya Urais. Pamoja na mambo mengine, mliahidi Watanzania mambo mawili: kuwa mkishinda mtaanzisha mchakato wa katiba mpya na pia mtaanzisha mchakato wa maridhiano. Sisi wengine hatukuamini kama kweli kulikuwa na uchaguzi mwaka jana, lakini hiyo haiondoi ukweli wa ahadi zenu.

Siku ya uchaguzi, tarehe 29 Oktoba 2025 na siku mbili zilizofuata 30 - 31 Oktoba kulikuwa na mauaji ya maelfu ya watu. Kanisa lilaani sana mauaji yale. Dkt. Nchimbi hakutoa kauli yoyote kuhusu matukio yale.
Katika hali ya kushangaza, baadhi ya viongozi wa dini ya Kiislamu wakiwemo pia BAKWATA walitoka hadharani kuitetea Serikali. Lakini kwa lugha rahisi walikuwa wanakutetea wewe dhidi ya kile walichokiita 'Kanisa' kukushambulia!

Aliibuka sheikh mmoja akatamba hadharani ya kuwa watawakata vichwa watu watakaoipinga Serikali yako. Katika yote hayo, hakukutokea na hapakuwa na kauli yoyote ya kutoka serikalini au CCM ya kujitenga na kauli hizo. Lakini pia hakukuwa na mtu yeyote aliyehojiwa na Jeshi la Polisi kwa kutoa kauli zile zilizobeba jinai!
Baadaye, Sheikh Rajab Katimba akiambatana na masheikh wenzake aliitisha vyombo vya habari kumshambulia Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi. Sheikh Katimba alidai ya kuwa Dkt. Nchimbi alikuwa anatumwa na Fr. Charles Kitima ambaye ni Katibu Mkuu wa TEC ili kumhujumu Rais Samia.

Hata katika jambo zito kama hilo hakukutokea mtu yeyote wa serikali au CCM kujitenga na kauli ya Sheikh Katimba. Kwa wachambuzi wa mambo wakajua kuwa Sheikh Katimba alikuwa ametumwa kusema yale aliyoyasema. Baadaye aliibuka Mbunge kutoka Zanzibar na akatumia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumshambulia Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi akimuita kama 'Yuda'! Wakristo wanaelewa ni nini maana ya msemo wa 'Yuda'!

Hata katika hilo, hakutokea mtu yoyote ndani ya Serikali au CCM kujitenga na kauli ya Mbunge wa kutoka Zanzibar. Ilishangaza sana kuona hata Spika aliziruhusu kauli zile ziingie katika kumbukumbu za Bunge (Hansards)! Katika hili, wachambuzi wa mambo walijua kuwa Mbunge kutoka Zanzibar na Spika wa Bunge walikuwa wamepangwa!

Baadaye Dkt. Nchimbi alitoa kauli hadharani ya kuhamasisha Watanzania kupigania kwa nguvu zao katiba mpya. Jambo hili lilizidisha chuki dhidi ya Dkt. Nchimbi kutoka miongoni mwa watu wa CCM au Serikali kwani baadhi yao pia sauti zao zilisikika. Lakini Watanzania wengi na hata kwa watu wa nje, kauli ya Dkt. Nchimbi pia ilionyesha ufa wa wazi kati yake na Serikali ya CCM, kati yake na CCM au kati yake na Rais.

Baadaye, Dkt. Nchimbi alionekana akitembelea viongozi wastaafu akiwemo pia Rais mstaafu Jakaya Kikwete. Lakini zaidi ya picha kuwekwa hadharani hakuna ajuaye maudhui ya vikao au mazungumzo yao. Baadaye ikatangazwa ghafla kuwa Dkt. Nchimbi amejiuzulu. Taarifa hii pia ilitanguliwa na uvumi kuwa Dkt. Emmanuel Nchimbi alikuwa analazimishwa kujiuzulu.

Baada ya taarifa hiyo, CCM ikatangaza kumvua au kumfukuza uanachama bila kueleza sababu zozote za msingi. Baada ya hapo, Mwenyekiti wa UVCCM na wenyeviti wa CCM kutoka mikoa kadhaa wakaanza kumsema Dkt. Nchimbi.

Ni mwezi mmoja umepita tangu itangazwe ya kuwa Dkt. Nchimbi amejiuzulu lakini yeye bado hajaonekana hadharani. Kuna minong'ono na maneno mengi yanayozungumzwa kuhusu hali, afya na mazingira ya Nchimbi. Kwamba Dkt. Nchimbi yuko kizuizini hili sio jambo la kuficha.

Kwa mtiririko wa matukio hayo na muktadha huo, ni wazi kuwa Dkt. Nchimbi aligombana ama na Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Jamhuri, Serikali au CCM yenyewe! Na kama ni hivyo, ni wazi kuwa taasisi hizo zilimuona Dkt. Nchimbi kuwa alikuwa na makosa kiasi cha kupelekea yeye kulazimishwa kujiuzulu, kufukuzwa CCM na hata kuwekwa kizuizini na Serikali yake.

Kwa mantiki hiyo, tunayo katiba inayotuelekeza nini cha kufanya endapo mtu ama ameikosea Jamhuri au ameikosea taasisi yake. Tunataka kuona katiba ya nchi inafuatwa kwa mtu au kila Mtanzania ikiwa akihisiwa kuwa ana makosa!

Watanzania wanataka kumuona Dkt. Nchimbi akiwa mtu huru. Kama alikosea wanataka pia kumuona akipelekwa mahakamani badala ya kufichwa au kuwekwa kizuizini kinyume kabisa na matakwa ya katiba yetu!

Tunahitimisha kwa kukuomba Mheshimiwa Rais, serikali unayoingoza ifanye jambo moja kati ya haya: ama imuachie huru Dkt. Nchimbi awe huru kama wastaafu wengine wakiwemo Philip Mpango na Majaliwa Kasim

Majaliwa au impeleke mahakamani akajibu tuhuma zozote zinazomkabili.
Hakuna mamlaka yoyote nchini ambayo inao uwezo, amri na mamlaka ya kuondoa uhuru wa wa mtu ye yote kwa kipindi kirefu isipokuwa mahakama peke yake.

Kinyume cha hapo Mheshimiwa Rais, sisi na taasisi nyingine tutaanza kuitangazia dunia ya kuwa Dkt. Nchimbi anashikiliwa kinyume cha sheria na tutaanza kuunganisha Watanzania na dunia kwa ujumla kwa ajili ya kupiga kelele ili kuweka mashinikizo ya kutaka kuachiwa kwa Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.
Lililo kubwa zaidi, tunaombea na tunatarajia ya kuwa afya ya akili ya Dkt. Nchimbi iko salama na kuwa haitaingiliwa na michakato yoyote ya kibinadamu katika kipindi chote ambacho yuko mahali kusikojulikana na Watanzania!

Mheshimiwa Rais, wewe unayo nafasi kubwa kukufanya usilaumike katika jambo hili kama serikali yako itamuachia Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi awe huru kuishi maisha yake kama wastaafu wengine! Wakati ukifika Mheshimiwa Rais, watu wote wanaomzunguka Rais watajitetea kuwa walikuwa wanatumwa.

Soma Pia: Askofu Bangonza: CCM wanaomshambulia Dkt. Nchimbi ndio wanakwamisha Katiba mpya

Lakini kiti cha Rais kinapaswa kisilaumike!
Ni wajibu wetu kuionya, kuishauri, kuikemea na hata kuielekeza mamlaka yoyote ya kijamii au kibinadamu kwani jukumu hili pia ni sehemu ya wito wetu wa Ki-Biblia (Ezekieli 33:1-22).
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani (World Fellowship of Moravian Revival Churches, WFMRC).
Dar es Salaam; 20 Septemba 2026; Saa 7:32 adhuhuri
819175825_2095131614727532_939233339104620857_n.jpg
 
Nini kimekushangaza? Mwanakondoo ameshinda ,tumfuate.
 
Back
Top Bottom