Askofu Mwamakula: Sikutarajia yaliyoandikwa na Kabendera yangewekwa hadharani wakati wa uhai wangu

Askofu Mwamakula: Sikutarajia yaliyoandikwa na Kabendera yangewekwa hadharani wakati wa uhai wangu

Kwa maneno mengine, Askofu anatuthibitishia kwamba yaliyoandikwa katika kitabu cha Kabendera ni kweli kwani naye alipewa taarifa hizohizo ila hakuwahi kuzisema kokote.
Yes ,

Na kitu kingine ambacho Askofu amekielezea hapa ni kuwa iliandaliwa pesa nyingi sana ya kuhakikisha wale wabunge 19 wa viti maalumu wanaingia bungeni.Yeye askofu alikataa hiyo aliyoiita dili.Lakini kwakuwa tunajua sasa kuwa walienda bungeni,basi tuna uhakika kuwa kuna watu walikula hiyo pesa ndefu....Nani walikula hiyo pesa?Mcha kato unaoendelea wa uchaguzi wa mwenyekiti na makamu mwenyekiti chadema umetupa majibu yote hadi sasa......

Tunategemea vitu vingi kujulikana zaidi ingawa vingine vinafichwa katikati ya mistari kwenye maandishi ya kifalsafa kama hili andiko la Askofu.
 
Mkienda kutubu kwenye mtandao wa "Sisi Askofu" mtandao unarekodi na kuweka backup data zote mshaambiwa.

Sisi Askofu Mwamakula.
 
Humu kuna watu na mahaba yao wanamchukulia Magufuli kama mtakatifu.
Niseme tu kuwa pamoja na mazuri yake lakini pia alikuwa na mabaya yake tena mengi mno.
 
Ukitaka kujua mtu muongo aliyekubuhu wana sifa moja za kufanana wawe maaskofu au yeyote utasikia marehemu aliniambia wakijua marehemu hawezi fufuka kujitetea au kusema muongo huyu Askofu

Askofu Mwamakula anaangukia kwenye hilo kundi la waongo wabobezi kwa nini hakusema hayo Magufuli akiwa hai?
Kwa nini mnajitoa ufahamu kwa sentensi hii
Ukitaka kujua mtu muongo aliyekubuhu wana sifa moja za kufanana wawe maaskofu au yeyote utasikia marehemu aliniambia wakijua marehemu hawezi fufuka kujitetea au kusema muongo huyu Askofu

Askofu Mwamakula anaangukia kwenye hilo kundi la waongo wabobezi kwa nini hakusema hayo Magufuli akiwa hai?
Mnajitoa ufahamu. Nani angesema haya akaendelea kuishi.
Ukitaka kujua mtu muongo aliyekubuhu wana sifa moja za kufanana wawe maaskofu au yeyote utasikia marehemu aliniambia wakijua marehemu hawezi fufuka kujitetea au kusema muongo huyu Askofu

Askofu Mwamakula anaangukia kwenye hilo kundi la waongo wabobezi kwa nini hakusema hayo Magufuli akiwa hai?
Nani angetaka kufa kabla kwa kuyasema hayo mbele ya jiwe akaendelea kuishi ? Msijitoe ufahamu.
 
Tangu hizi habari zianze kusambaa hatujaona uthibitisho hata mmoja. Ni hearsays, speculations na personal opionions tu zinatawala. What a crap kutoka kwa a self-declared bishop.

Na bahati nzuri zinatoka kwa walewale vibaraka wa mabeberu. Hatushangai kama ambavyo hatushangai panya kumchukia paka.

It changes nothing especially kazi kubwa aliyolifanyia taifa hili Rais bora kabisa kuwahi kutokea.
Rais Bora kumpita Nyerere aliyetuachia viwanda zaidi ya 400, migodi, shule bure mpaka university, afya bure.
 
Ndugu askofu hapo unayumba sana

Umesema mambo hayo ni siri kati yako na mtubio

Kitabu kimeandikwa unaafikiana nacho

Sasa which is which??

Kwa hiyo unauthibitishia umma kuwa huu ni ukweli mtupu???


Nah umechelewa sana, ungekuwa na mashiko kama ungeyasema hayo mwanzo
Mbona mnarudia kusema alipaswa kusema kabla. Angesemea wapi na kwa nani ? Humu wote ni I'd ya kificho mpaka wewe.
 
KABENDERA ANADAI BEN SANANE ALIUAWA NA 'BWANA MKUBWA'!

Mwishoni mwa mwaka 2020, nilipata ujumbe mzito kutoka kwa Rais Magufuli kupitia kwa mtu wake mmoja ambaye jina lake linatunzwa. Rais alimtuma kwangu akiniomba nishawishi Mhe. Freeman Mbowe na Mhe. Tundu Lissu waridhie wabunge wanawake 19 waapishwe kuwa Wabunge wa Viti Maalum.

Nilijitahidi kufurukuta kueleza Rais ajue kuwa sikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA wala mimi sikuwa na ushawishi wowote katika jambo lile. Lakini Rais aliamini kuwa Lissu na Mbowe watanisikiliza mimi. Lilikuwa jambo gumu sana kwangu kumshawishi mtu yule aniamini mimi. Ahadi niliyoahidiwa na ambayo pia CHADEMA wangepewa kama 'dili' lile lingefanyika ingali katika kilindi cha moyo.

Nakiri kuwa baada ya ombi la Rais la kunitaka niwashawishi Lissu na Mbowe kushindikana, zoezi la uapishwaji liliendelea na mimi nikajua kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari. Lakini hoja la andiko hili sio jambo hili.

Mwezi Januari 2021, alitumwa tena kwangu mtu yule yule. Safari hii haikuwa kunishawishi ili niwashawishi Mbowe na Lissu, bali ilikuwa ni kunitisha niachane na harakati, la sivyo basi nilikuwa nachungulia mauti. Nilikuwa nimetoka kuitangazia dunia kuwa maisha ya Mhe. Lissu yalikuwa hatarini na ndipo Ubalozi mmojawapo ukamchukua na kumpeleka nje ya nchi.

Kwa hiyo jibu langu kwake lilikuwa moja tu: "Mwambie Mheshimiwa kuwa akitaka aniue, lakini Askofu hatarudi nyuma"! Vitisho vya aina hiyo niliwahi kupewa na Polisi mmoja nikiwa Central Polisi, Dar es Salaam mwezi mmoja kabla Rais Magufuli hajafariki dunia.

Baada ya majibu yale, yule mtu alitetemeka na ikabidi aropoke mambo mengi sana ambayo sio sehemu ya andiko hili kwani kwa sasa Bado mambo yale ni 'classified information'! Baada ya hapo nikaanza kupata taarifa nyingi ambazo zilinitisha na kunipatia matumaini.

Siku moja nilitafutwa na mtu mmoja ambaye ni mzima na kada wa CCM. Kwa kuwa mtu huyo tunaheshimiana na kwa kuwa aliaminishwa ya kuwa mimi nilikuwa natumiwa na 'mabeberu'; ilibidi nimueleze pia baadhi ya mambo ambayo yalikuwa yanamzunguka Rais. Nilifanya hivyo ikiwa kinga yangu kwani nilijua kuwa ataelewa mazingira yangu na hivyo ataweza kupangua hoja dhaifu dhidi yangu akiwa katika 'Pango la Wakilindi'. Aliishia kunikodolea macho na ndipo tukaagana akiwa kama mtu asiyeamini.

Lakini kabla mtu huyo hajaondoka, aliniuliza: "Wewe umejuaje habari hizi'? Nikamjibu kuwa: "Mimi ni mskofu wa mnyororo na pia mimi ni askofu wa kiapo"! Mambo haya yaliaminiwa pia kwangu chini ya kiapo kwa hiyo nisingeyasema hadharani wakati ule na hata sasa. Hapa sio mahali pake kuelezea kisa cha askari aliyeacha kufanya ibada baada ya kushiriki kuwaua watu na baadaye kumbukumbu za watu wale zikawa zinamjia na kuharibu akili yake.

Mambo haya ni ya kitubio na kwa hiyo mtu ye yote atakayemuendea Mchungaji (Padri) au Askofu kwa kitubio, jambo lile linabakia katika kifua cha mtubishaji, anayetubu na Mungu.

Taarifa za kuchapishwa kwa kitabu cha Erick Kabendera zimeanza kusambaa kwa kasi sana mitandaoni siku ya leo tarehe 3 Januari 2025. Kitabu kinaitwa: 'In the Name of the President: Memoirs of a Jailed Journalist'. Nimesikiliza mahojiano ya Erick Kabendera kuhusu kitabu hicho. Nimeanza kufuatilia maudhui ya kitabu. Mengi ya mambo anayojadili ni sehemu ya yale niliyojulishwa kama 'sisi Askofu'! Ila sikutarajia mambo yale yangewekwa hadharani wakati wa uhai wangu. Ujasiri wa Kabendera unaivuka mipaka ya Nshamba na Kamachumu.

Ninaamini watu ambao walinishangaa kwa nini mimi nilijitoa muhanga kwa ajili ya kutetea haki nchini sasa wataanza kuelewa baada ya kuona na kusoma kitabu cha Erick Kabendera. Taarifa nyingi zilizofikishwa katika kilindi cha moyo wangu ziliishurutisha nafasi yangu kuchukua ili kupaza sauti na kutetea pale nilipoweza. Lakini pamoja na uropokaji wangu, mambo ambayo yalitiwa muhuri (sealed) katika moyo wangu yameamriwa na dhamiri iliyo kuu ili yasiyoke.

Kitabu cha Kabendera kitasaidia katika mambo muhimu. Kwamba tukisome na kumjua Rais Magufuli nje ya uelewa uliojulikana. Baada ya hapo, tuone kuwa alikuwa binadamu kama sisi na mwenye mapungufu na kisha tumsamehe. Kikubwa, kama jamii tutafute njia ya kuponya ikiwemo kuondoa vimelea au masalia ya yale aliyoayaasisi ambayo hayakuwa mazuri na hili itawezekana kama tutasoma na kuielewa sura ya mwisho ya Kitabu cha Kabendera.

Kitabu hiki kinaposambazwa na kusomwa ni vizuri tujue kuwa kinayahusu maisha fichika ya Rais Magufuli na sio maisha ya familia na ukoo wake. Hatuhitaji kwa namna yeyote kuwaona ndugu hata familia kama sehemu ya mambo aliyoyafanya kama Rais kwani nao walikuwa ni washangaaji kama sisi.

Mwisho, natoa wito kwa viongozi wa dini walio karibu na familia ya Ben Sanane na familia ya Azorly Gwanda kuzifikia kwa ajili ya huduma ya kiroho. Kupitia kitabu cha Erick Kabendera na mahojiano yake ni rasmi sasa ya kuwa umma umejulishwa kuwa watu hao hawapo pamoja nasi katika maisha haya.

Hekima iliyo ndani ya kilindi cha moyo wa Rais Samia inaweza kumsaidia afanye nini kwa ajili ya familia hizo. Bila shaka, CHADEMA itatafuta namna njema ya kuhitimisha kwa heshima kwa kumkumbuka Ben, mwanachama na Msaidizi maalum wa Mhe. Mbowe. Kadhalika, Gazeti la Mwananchi litaona pia namna ya kulihitimisha l kwa heshima ya Azorly, aliyekuwa mtumishi.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 3 Januari 2025; saa 2:00 usiku
da!!!...noma kuliko noma yenyewe!!!!
 
Sio vema kumsema au kusema maovu ya mtu aliye fariki kwani huwa unamjengea mazingira magumu huko aliko wewe ukiwa kama askofu unalijua hilo tunajifunza nini kwako, lakini kwanini haya mambo usiyaseme kipindi yupo hai na sifa moja wapo ya askofu ni kutofumbia maovu yanapofanyika🙄
Tulikotoka kwa udongo na tutarudi kwa udongo,Ukifa,umekufa haturudi kuishi hadi kiama!, Matendo uliyotenda ukiwa hai,ndio utaambatana nayo.Mungu mwema,tutende mema.
 
Huyu Mtumishi wa Mungu aliyehai anasema taarifa zilimtisha na tena zikampa matumaini? How?
zilimpa matumaini? mema au mabaya.kama ni mabaya yaletayo furaha ya moyo maana yake kulikuwa na mipango mibaya juu ya mtu yule
 
Kuna lijamaa ililikuwa kinaitwa Chacha jeusi hivi refu liliuwa sana naye Sasa hivi anaweweseka tu...
 
Ukitaka kujua mtu muongo aliyekubuhu wana sifa moja za kufanana wawe maaskofu au yeyote utasikia marehemu aliniambia wakijua marehemu hawezi fufuka kujitetea au kusema muongo huyu Askofu

Askofu Mwamakula anaangukia kwenye hilo kundi la waongo wabobezi kwa nini hakusema hayo Magufuli akiwa hai?
Na kwanini pia hamtaji yule aliye hai, aliyetumwa kwake amshawishi awashawishi mbowe na pia kumtishia kifo. Amtaje basi kama ni kweli ili tumsikie akikanusha au kukubali alitumwa na Magufuli. Vinginevyo huu ni uongo na uzushi kwani wanajua Magufuli hawezi kujibu. Wawahusishe kwa kuwataja wasaidizi wa Magufuli ili wajibu na sio kuzushia uongo kaburi.
 
Kama ndo hivo kwa nini mnamsimanga aliewafungulia milango ya kuyasema haya? Au wanafiki wakubwa tu,maana miongoni mwenu mmethubutu kusema bora ya mjomba kuliko bibi
 
Back
Top Bottom