BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
ASKOFU MWAMALANGA ATUMA UJUMBE MZITO KUHUSU FREEMAN MBOWE!
"Mpendwa Askofu Mwamakula, nakutumia ujumbe huo ninataka usomwe na watu wote!
Kukamatwa kwa Mheshimiwa Freeman Mbowe na kubambikiwa Kesi ya Ugaidi ni kitendo cha kulibandika kinyesi Taifa la Tanzania mbele ya mataifa. Kwetu sote Watanzania, tunamuona Mbowe kuwa ni mtu mwadilifu miongoni mwa wanasiasa wa vyama vyote nchini. Hivyo, Mheshimwa Mbowe kupewa kesi ya Ugaidi ni kitendo cha aibu kwa Watanzania. Aliyepanga bandiko hilo bado hajafaulu. Lengo lake ni kuitia moto jamii ya Watanzania!
Ninawasihi Watanzania kumtegemea Mungu Mwenyezi mia kwa mia; nanyi mtaona haki yake itakavyoshuka haraka na kutuliza mioyo yetu! Msiogope wala msinung'unike, fanyeni sala na dua, adhabu zao ni sasa. Duniani kote, Mbowe anaheshimika kama mwanasiasa salama na safi. Msiogope! Tazama, mipango ya shetani juu ya nchi yetu haitafaulu. Ombeni rehema za Mungu Mwenyezi kila mtu mahali alipo. Yesu Kristo ni yote katika yote. Amini na Amina! Ujumbe huu usomwe na kila mtu
Ujumbe huu umetolewa nami Askofu William Mwamalanga kwenye Kongamano la Amani kwa Afrika linalofanyika Lusaka, Zambia na kushirikisha viongozi wa dini wa nchi za Maziwa Makuu kwa kuiombea Afrika. Ndipo Dkt. Wood Edwards kutoka Uingereza akaomba kuiombea Tanzania ili inusurike na dhambi ya uonevu unaoendelea nchini Tanzania.
Mimi Askofu William Mwamalanga nimeubariki ujumbe huu kwani ni ujumbe hakika wa Mungu Mwenyezi kwa Watanzania kwani vitendo vya kubambikia watu kesi vimeota mizizi nchini pamoja na kumwaga damu zisizo na hatia. Ole wao wafanyao ubambikiaji huo na ole wao wawatumao watu kufanya hayo!
Askofu William Mwamalanga - Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashehe ya Kamati na Amani"