#COVID19 Askofu Niwemugizi, asitisha Misa na Ibada zote Jimbo la Rulenge, awataka waumini Wasali Majumbani pia Wajikinge na Corona

#COVID19 Askofu Niwemugizi, asitisha Misa na Ibada zote Jimbo la Rulenge, awataka waumini Wasali Majumbani pia Wajikinge na Corona

Jifunze kuheshimu maamuzi na mawazo ya mtu. Ukae ukijua binadamu hamuwezi kufanana kwa mawazo kimya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hatuwezi kushimu maamuzi hiovyo kama yaha. Kiongozi wa kiroho alitakiwa kuwa mfano wa kushimu mawazo na maamuzi ya mkuu wa nchi。jino kwa jino hatuwezi kumheshimu mtu wa aina hii ambaye anawapelekea waumini wake kwenye uasi.
 
hatuwezi kushimu maamuzi hiovyo kama yaha.Kiongozi wa kiroho alitakiwa kuwa mfano wa kushimu mawazo na maamuzi ya mkuu wa nchi。jino kwa jino hatuwezi kumheshimu mtu wa aina hii ambaye anawapelekea waumini wake kwenye uasi

Mkuu wa nchi atoe hela kwenye zile $5.3b zikanunulie vifaa tiba, mambo ya imani awaachie viongozi wa imani. Corona haiondolewi na Sala ya siku 3, bali matibabu ya kisayansi yanayohitaji fedha fullstop.
 
Mfalme hapigiwi kura acheni kupotosha maandiko
8F720897-FC36-4528-8EC9-C7E4D3D39DF5.jpeg
 
Kwani watu wakiomba kwenye majumba yao Mungu hasikii? Mnatetea kila aina ya ujinga anaosema huyo mnaemwita kiongozi wenu. Papa kaendeshs ibada bila waumini. Nyie ndio mnajifanya mnamjua Mungu sana kwa kuendelea kukusanya Waumini sehemu moja
 
Watu kama hawa usikute ndio wanatuongoza nchini wana madaraka. Anashindwa tu kungalia Italy na Saudi arabia pamoja na itikadi kali zote ila wamaufyata.

Huyu inabidi afiwe na mtu wake wa karibu kimuume ndio atajua kuwa akiwa kiongozi hatakiwi kuwa mpumbavu na kuchezea afya za wananchi.
 
Tatizo umeendika kwa mihemko sana! Askofu hajesema watu wasifanye maombi kumbuka pia maombi sio lazima uwe kanisani hata ukiwa nyumbani unaweza kufanya pia... Ningeshangaa kama askofu angesema watu wasifanye maombi

Sent by nokia tochi
 
Roma Italy wenye dini Yao wanasali majumbani ,,,,#wakusanyikapo wawili au watatu Kwa Jina langu Mimi nipo Kati Yao,,,, Mwisho askofu anaijua misingi ya Dini KULIKO huyo mfalme wako!..
Mpaka sasa itali wameshazika zaidi ya 20 elfu.hapo aliyeshinda ni Mungu au shetani?
 
Hv una akili za hivi? Unajua Corona inambukizwa sana ktk mikusanyiko? Kusali ulijua lazima uende kanisani au msikitini? Ww ndio hukumuelewa Mh. Rais hata kidogo unaropoka hapa, Mh. Rais kasema tuombee nchi kwa siku 3, sio tuende kanisani kwa siku 3, na kuomba sio kwenda kanisani tu, acha ujinga mkubwa huu. Coronavirus inaua sana sasa hv nchi kama Italy, US, UK, France, sbb hawakuzuia mikusanyiko mapema, jua hilo, mikusanyiko yoyote ni hatari sana sana, au ulijua huko nje hawakuwa wanasali ww ndio unajua kusali kuliko wao? Tahadhari hapa muhimu sana kabla ya yote, kusali ni sehemu yoyote kaa nyumbani sali, acha ujinga. Akili kama hizi ndio utaambukiza wengi kisha watapata infection, acha ujinga, epuka mikusnayiko yote, fuata ushauri wa wataalam wa afya, sali home, ombea nchi ukiwa nyumbani, sio lazima uende kanisani au msikitini ktk mikusanyiko.
 
ZALEMDA,
kajifunze utaratibu wa kanisa katoliki acha kuchoropoka toka polini,Rais ni mtoto mbele ya Askofu kwa Imani ya kanisa.Maamuzi ya askofu ni maamuzi ya jimbo labda yawe yanakiuka misingi ya kanisa kwako wewe maombi ni kanisani tu?Unajidanganya kanisa katoliki liko tofauti na fikra zako.Tena askofu huyu Sara zake zinaweza sikilizwa zaidi maana amejali maisha ya kondoo wake na ndio maana amesisitiza Sara ndani ya familia.
 
yeye si ana majeshi nchi nzima. ayaite yafanye maombi kwa pamoja Mungu atasikia kilio chake.

wakati watu wanakusanyika kumubea Lissu aliona wako na mzaha sasa ni hivi si ndio hatumuelewi kabisa.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria ichukue mkondo wake na achukuliwe hatua kali..
 
Uongozi wa wakoloni nao uliletwa na mungu? Iddi Amini? Kim Jeong Eun? wote tuwaheshimu na ushenzi wao kwa kua mungu kachagua? Watu wa dini ukilaza lini utawatoka? Kama mungu anapanga watu kama hawa huyo mungu kimeo kabisa
 
Back
Top Bottom