#COVID19 Askofu Niwemugizi, asitisha Misa na Ibada zote Jimbo la Rulenge, awataka waumini Wasali Majumbani pia Wajikinge na Corona

#COVID19 Askofu Niwemugizi, asitisha Misa na Ibada zote Jimbo la Rulenge, awataka waumini Wasali Majumbani pia Wajikinge na Corona

Sikujua km kanisa halina demokrasia

Sent using Jamii Forums mobile app
Lini ulisikia kuna uchaguzi wa kumchagua paroko au Askofu wa katoliki?Papa alishatoa waraka kwa Askofu Mahalia kuangalia hali ya eneo lake na kuamua kama asitishe ibada au ziendelee.
Kama Niwemugizi ameona inafaa(na kwa kweli yuko sahihi) hajavunja sheria yoyote ya kanisa bali ametekeleza waraka wa Pope
 
Mkuu wa nchi ametangaza siku tatu za maombolezo kwa ajiri ya nchi kama mfalme wa Ninawi alivyofanya.Unafahamu fika kuwa kila utawala hapa duniani unatoka kwa Mungu, uwe mzuri au Mbaya.

Neno la mfalme huwa linaheshimika na Mungu analiheshimu. Rais wetu Magufuli amenena maneno mema juu ya Mungu na hii lazima Mungu atakuwa upande wake regadless ana dhambi au hana kwa sababu ameonyesha unyenyekevu kuliko wewe Askofu .

Mwenye unyenyekevu atainuliwa tu lakini mwenye kiburi atashushwa wakati Mkuu wa nchi anahimiza watu kuomba wewe Askofu unatangaza waumini wasiende kanisani. Unafikiri ndiyo umewapenda waumini wako?

Umwonyesha udhaifu mkubwa wa imani, hufai kuwa askofu. Umechanganya imani na siasa hufai kuongoza kondoo. Umemdhalilisha aliyekufia msalabani kwa sababu umeenda kinyume na matakwa ya mfalme wa nchi(rais) umeenda kinyume na Mungu, umeenda kinyume na Biblia.

Mbona sasa hao waumini wako ni wa mfalme wa nchi ambaye yeye Amemheshimu aliyezifanya mbingu na nchi. Kanisa tujifunze kuheshimu katiba, tujifunze kuendana na Biblia. Moyoni umejaa chuki halafu unajifanya mtumishi wa Mungu.Mungu yupi huyo labda miungu.

Nashauri ukatubu wewe uendaye kinyume na matakwa ya mfalme vinginevyo waweza kuwa mfano wa manabii ya baali kipindi cha Elia Mtishbi.
Are you sober?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatuwezi kushimu maamuzi hiovyo kama yaha. Kiongozi wa kiroho alitakiwa kuwa mfano wa kushimu mawazo na maamuzi ya mkuu wa nchi。jino kwa jino hatuwezi kumheshimu mtu wa aina hii ambaye anawapelekea waumini wake kwenye uasi.
Unajua uasi?
Huyo ni askofu mbona unaleta siasa huku unamvuta Mungu upande wako.Maaskofu ni viongozi wa kiroho sio siasa.

Hafu hajasema watu wasiombe ila wafanye hivo wakiwa kwao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muwe mnauliza taratibu jinsi zilivyo ndani ya kanisa katoliki sio mtu unajiandikia tu kitu usichokielewa.
Askofu wa kikatoliki huwa anapewa nguvu ya kufanya maamuzi katika eneo analoliongoza bila kuingiliwa kimaamuzi na askofu mwingine.
Kardinali ni cheo cha heshima au kwa lugha nyepesi ni mshauri wa papa hivyo hana uwezo wa kutengua maamuzi ya askofu yeyote nchini Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilijiandikia coz sikumpata wakunielewesha, ungekuwa na akili nzuri ungetambua hilo mapema, ndio maana comments zangu juu zilitawaliwa na maswali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie wasomi anzeni mchakato, acha dunia imtambue, ikiwezekana hata jf tumtambue. Na kama wapo pia waliofunga milango ya misikiti kipindi hiki cha Corona tuwatambue, wameokoa roho za watu.

Sent using Jamii Forums mobile app


Hata kabla ya kufikia kwenye Nobel huyu na wote waliofunga makanisa na misikiti ilikuwa vyema kuwamo kwenye Taskforce ya kutokomeza Corona. Hii ikiwa ni katika kutambua jitihada zao za dhati kabisa za kuokoa maisha zisizokuwa na ubinafsi wala siasa hata kidogo.

Ukweli mchungu waliomo sasa hawatusaidii na hawatufai.
 
Mungu aliagiza watu wasiache kukusanyika kumeabudu huyo askofu ni Nani Wa kutengua alichoagiza Mungu? Hana mamlaka hayo

Kukusanyika kuabudu Mungu ndie kaagiza yeye Nani Wa kukataa.

Raisi yuko sahihi sababu hayuko juu ya Mungu na kaona asitdngue alichoagiza Mungu

Raisi anaijua dini kuliko huyo Askofu
Mkuu YEHODAYA, Italia imezika mapadre 30 kwa sababu ya hii corona, huo ukatoliki umeanzia Italia lakini msiba walioupata ni mkubwa sana.

Mecca ambako kila muislamu anakwenda kuhiji mwaka huu pamefungwa, kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi hakutakuwa na Alhaji au Hajjat ambaye ni matokeo ya Hija ya mwaka 2020.

Mungu yupo lakini majanga ya maradhi yanapoibuka Mungu huyo huyo anatambua dharura na maamuzi yanayotokana na dharura hiyo.

Sio jambo la kiungwana kumtukana Baba Askofu ukiwa unaongozwa na hizi hulka za kisiasa.
 
Askofu yupo sahihi kabisa.

Ukweli viongozi wa Serikali wanapwaya sana kwenye hili suala la janga la Corona. Mpaka sasa watu wanauza bidhaa bila kuvaa Maski.

Watu bado wanauza vyakula na vinywaji bila kuvaa maski. Watu wanaenda kanisani na misikitini bila kuvaa maski.
Halafu wakitoka hapo wanaenda kwenye mabaa ,magesti, ufukweni,kwenye mapull table ,kwenye mabasi ,mabodaboda bila kuvaa maski.

Watu wanaenda mahosipitalini bila kuvaa maski halafu wanarudi majumbani na kwenda kanisani bila kuvaa maski.
Ni kiongozi gani mwenye maono makubwa atakubali hali hiyo iruhusu mikusanyiko.

Watu wanauza bidhaa na kupiga chafya au kukohoa na unyevu unasambaa kwenye bidhaa zake halafu wateja wanakuja wanashika bila kuvaa maski kwa sababu tu wamenawa mikono bila kujiuliza inakuaje kwa wale wanaopiga chafya kwenye mabasi bila kuvaa maski.

Kuna siku abiria mmoja alitapika kwenye basi .Akahama siti na abiria waliopanda njiani wakawa wanaingia na kukaa kwenye ile siti na kukanyaga mapatishi na waliposhtuka ndio Wakahama.

Basi lilikua ni Luxury vioo vimefunwa mwanzo Mwisho. Mpaka walipofika hotelini ndio Basi likasafishwa na wahudumu wa vyoo vya hoteli. Sasa cha ajabu Basi zima hawakuvaa maski wanapumua tu na kuvuta hewa iliyojaa harufu ya matapishi.

Hawakuvaa maski kwa sababu mwanzoni waliambiwa kuwa hakuna haja ya kuvaa maski mpaka MTU apate maambukizi.
Kila mmoja anahisi akivaa maski ataonekana kuwa ameshapata maambukizi.

Kabisa Katoliki Mara nyingi limekua likitangulia kabla ya taasisi nyingine zote. Kabisa katoliki lilizitangulia mpaka serikali enzi za mkoloni.Walijenga mahospitali na mashule kabla ya serikali. Watu wao wakasoma wakati wengine wakiona kusoma ni kupoteza muda. Walisimama kidete kupinga biashara ya utumwa kwa kuwanunua watumwa na kuwaachia huru.

Tuabudu na kusali maana hawajakataza. Lakini pia tujiulize tunakusanyika kama watakatifu au ni makundi ya watu waovu waliojaa mioyo ya chuki na ubinafsi halafu tunafikiri kuwa Corona itaisha kwa kukusanyika bila kutakasa mioyo yetu.

Mungu anapotoa adhabu analengo la kuona toba ikifanyika sio kukusanyika bila kuacha dhambi na kutenda mema kwa imani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ugonjwa huu ni wa hasira ya Mwenyezi Mungu au vipi.kama ni wa Mungu kwa Nini na Nini kifanyike au jibu ni kutokwenda makanisani kweli,nchi hi imekosa hata mtu mmoja wa kuongea na Mungu mbona Mambo yalipo waendea vibaya Waisrael walimtuma Mussa leo hakuna hata mmoja kweli badala yake tunakimbia uso wa Mungu kwa kuwaambia watu wasiende makanisani na misikitini.

Rais ana maono Tena Sana lakini kwa Nini watu wasitubu kwa makosa mbalimbali tuyomkosea Mungu au my akisema hivyo amefanya kosa kwa vile wote tumepungukiwa ukweli nchi hi umekuwa adimu mno, Mungu c kiziwi Wala kipofu kiasi hiki.tumekosa sauti ya mtu mwadirifu kweli? Hatuwezi kuomba msamaha Kama hatuna kosa na Kama hatuna kosa kwa Nini tupigwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha ujinga, kati ya rais na mtumishi wa Mungu nani anapaswa kusikilizwa zaidi? Rais akitoa amri wanawake wote wanavyoingia kanisani wavae suruali za jinsi utatii wakati unajua ni makosa kibiblia mwanamke kuvaa suruali?
Askofu kashaongea na Mungu wake kampa hekima hiyo sasa wewe na Mungu nani mkubwa?au Magufuli ni Mungu wako?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kanisa sio ofisi ya mkuu wa mkoa kwamba itekeleze maagizo ya Rais.

Hivi vifungu vya biblia hao walioviandika huko ulaya wakatuletea sisi Afrika havijawasaidia wamesalimu amri.
Ttz la kisayansi litamalizwa kusayansi
 
Ugonjwa huu ni wa hasira ya Mwenyezi Mungu au vipi.kama ni wa Mungu kwa Nini na Nini kifanyike au jibu ni kutokwenda makanisani kweli,nchi hi imekosa hata mtu mmoja wa kuongea na Mungu mbona Mambo yalipo waendea vibaya Waisrael walimtuma Mussa leo hakuna hata mmoja kweli badala yake tunakimbia uso wa Mungu kwa kuwaambia watu wasiende makanisani na misikitini.

Rais ana maono Tena Sana lakini kwa Nini watu wasitubu kwa makosa mbalimbali tuyomkosea Mungu au my akisema hivyo amefanya kosa kwa vile wote tumepungukiwa ukweli nchi hi umekuwa adimu mno,Mungu c kiziwi Wala kipofu kiasi hiki.tumekosa sauti ya mtu mwadirifu kweli? Hatuwezi kuomba msamaha Kama hatuna kosa na Kama hatuna kosa kwa Nini tupigwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Walokole bwana.Si uende wewe mbele za mungu kwani unahitaji cheti mkuu.
 
Mwoga asiye na imani anaogopa kuwa Mungu atampa corona kwenye ibada!!!!! Kazi ya Mungu sio kugawa corona ibadani lioga hilo halina imani ndio maana limejifungia ndani.
Wachungaji na manabii wa mwendo kasi mnaona njaa imebisha hodi mnapambania sadaka. So far Mungu yupo kila mahali na kuwasiliana na mungu ni suala la kiimani sio suala la jengo.
 
gosp.jpg
 
Kinachosikitisha ni huu uamuzi muhimu kabisa kuachiwa viongozi wa dini wenyewe watumie utashi wao!

Je makanisa ya watu binafsi yatafungwa kwa hiari ilhali wanahubiri Yesu hashindwi?
Gwajima akale wapi huoni anavyohaha huko anavyoumbuka?
 
Back
Top Bottom