#COVID19 Askofu Niwemugizi, asitisha Misa na Ibada zote Jimbo la Rulenge, awataka waumini Wasali Majumbani pia Wajikinge na Corona

#COVID19 Askofu Niwemugizi, asitisha Misa na Ibada zote Jimbo la Rulenge, awataka waumini Wasali Majumbani pia Wajikinge na Corona

Umenikumbusha mbali. Wakati ule nilipokuwa nawakikisha vijana, wakati wa kikao cha Baraza la Kichungaji la jimbo ambalo Mwenyekiti alikuwa Baba Askofu, wajumbe ni ngazi ya jimbo na mapadre wakuu wa dekania, kulikuwa na ajenda ya kukea miito mitakatifu. Baada ya maoni ya sisi wajumbe wote kusikilizwa, mwishowe Baba Askofu, bila ya kujali wangapi mmeshauri nini, alisema, "Roma Lacuta" kisha akaeleza kitakachotakiwa kufanywa.
Kutokana na hiki ulichoandika hapa huoni Askofu nae kuna mamlaka anatakiwa kuisikiliza?

Labda sifahamu, hivi kati ya Askofu na Kadinali nani yupo juu ya mwingine?

Kama itatokea Kadinali yupo juu ya Askofu, sitashangaa siku za mbeleni hilo tamko la leo la Askofu likatenguliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani ulivyo tutusa unataka mimi niwaze kama wewe ?

Kwani papa anashindwa nini kuingilia?

Yanayoendelea Italy sio Tanzania

Usije ukafiri unauwezo mkubwa wa kuyatafakari mambo kumbe umejaa ujinga tu kichwani mwako

Shika adabu yako usinizoee



Sent using Jamii Forums mobile app
Acha ujinga kakueleza ukweli, ulipaswa umwambie asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Askofu angekaimisha ibada kwa shemasi haya ni maamuzi ya kidikteta

Waumini hawajashirikishwa

Papa aingilie kati

Sent using Jamii Forums mobile app

Vijana wa siku hizi na kutofahamu mambo ya dunia mnapeleka wapi upupu wenu huu??

Hivi hufahamu kuwa kwa mara ya kwanza toka vita kuu ya pili ya dunia, vatican sio sehemu ya kufanyia ibada tena? Hata pasaka papa kasalia kwenye chumba huku waumini wakijiunga kwa podcasts, vc na television.

Unashauri waiumini waulizwe bila kusema hata waulizwe vipi! Je kuna uamuzi wowote wa Papa au askofu waumini waliwahi kuulizwa? Nimegundua hujui majukumu ya uongozi. Uongozi ni kufanya uamuzi kwa niaba ya wengine ukiamini umechukua uamuzi ambao ungeungwa na wote.

Je, waliosema tuendelee na shughuli kama kawaida, wameuliza wananchi kwanza??
 
Kanisa Katoliki Jimboni Rulenge-Ngara, wamesitisha kabisa Ibada/misa. Watu wasali nyumbani! Pia amewataka waumini wajikinge na COVID-19 na kuchukua tahadhari


Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge-Ngara limesema limesitisha Ibada za Misa, maadhimisho mengine yanayokusanya Waumini wengi Kanisani na sala za Jumuiya kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia Aprili 19, 2020

Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo hilo amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kutafakari alama za nyakati na kujifunza kutoka kwa watu wa Ulaya, Marekani na nchi za jirani na hatua ambazo Baba Mtakatifu alizichukua kwa kutoa maelekezo kwa Maaskofu Wakatoliki Duniani na namna ya kuadhimisha Ibada

Amesema pamoja na kumshukuru Rais Magufuli kutotoa amri ya kufunga Makanisa na Misikiti, akihimiza kufanya ibada kumuomba Mungu atunusuru na janga hili, kama Mchungaji wa Jimbo la Rulenge-Ngara ameamua kuchukua uamuzi huo

Aidha, Askofu Niwemugizi amesema pale itakapowezekana wataomba redio Kwizera irushe adhimisho la Misa fupi na Waamini wafuatilie redioni. Baada ya mwezi kuisha Kanisa litaangalia hali ilivyo ili kama iliongeze muda

Pia, amewataka mapadre kuadhimisha misa peke yao kwa niaba ya waumini kuwaombea na kuiombea dunia ili Mungu atunusuru na #COVID19 hili na kuagiza sala za Jumuiya kufanyika ndani ya familia kwa familia moja moja
View attachment 1422602
Katika viongozi wanaojali waumini au wananchi huyo Askofu ni namba moja Tanzania. Ubarikiwe Askofu
 
Roma Locuta Est, Causa Finita Est = "Rome has spoken, the case is closed".
Ngara sio Rome. Ni Askofu wa ngara ameamua hivyo.
I am interested to know this guy. He has been a source of many controversies. Who is he?
 
Safi sana,huu ndio utumishi wa Mungu tunaouhitaji.

Better late than never.

Waumini katika maeneo mengine, mjiongeza,msisubiri taarifa kama hii kwani si kila kiongozi wa dini atafanya hivi katika maeneo yenu.

Viongozi wa madhehebu mbalimbali(RC,KKKT.n.k) wanaokutana kutoa matamko ya pamoja(waraka) kama ya kukemea maovu,kukemea wanasiasa,n.k,walipaswa kuwa wamekutana na kuja na tamko kama hili; hivyo, tunatumai tangazo hili litatumika kama mfano kwa viongozi wengine wa dini waliobaki.

Baba Askofu,katika hili,umevaa viatu vilivyowapwaya wengi wakiwemo viongozi wa dini na wasio viongozi wa dini.

Hongera sana Baba Askofu!
Angalizo
Kanisa Cathoric sio Dhehebu
 
Back
Top Bottom