#COVID19 Askofu Niwemugizi, asitisha Misa na Ibada zote Jimbo la Rulenge, awataka waumini Wasali Majumbani pia Wajikinge na Corona

#COVID19 Askofu Niwemugizi, asitisha Misa na Ibada zote Jimbo la Rulenge, awataka waumini Wasali Majumbani pia Wajikinge na Corona

Kinachosikitisha ni huu uamuzi muhimu kabisa kuachiwa viongozi wa dini wenyewe watumie utashi wao!

Je makanisa ya watu binafsi yatafungwa kwa hiari ilhali wanahubiri Yesu hashindwi?

Huyo mmoja kashachukua hatua, hao wengine itabidi wafuate tu, maana wakiendelea wataonekana ni wasaka sadaka tu.
 
Nishakwambia huna akili na nimekuthibitishia kutokana na ujinga ulioshauri. Bad enough kubishana na mwehu kama wewe naona unanipotezea tu muda wangu.
Usibishane na mjinga na wewe utaonekana mjinga,dishi limeyumba huyo Bia Yetu.
 
Safi sana hawa ndiyo watu wanajua kufikirj wenyewe sio kusubiri MTU mmoja afikiri kwaniaba yenu!! Wengi wanaojikausha kisa ni sadaka siokwamba wanatamani sana kuhubiria watu
Asikofu amedhihilisha kuwa hana Njaa ya sadaka.
 
Asante Baba Askofu. Mungu wetu wa mbinguni azidi kukubariki na kukuongezea hekima ili siku moja nawe, ukiwa mbele zake upate kunena, "Baba katika wale ulionipa, sikumpoteza hata mmojawapo kwa kukosa maarifa".
 
The truth will set you free. Askofu kaona mbali.Mungu akubariki.
 
Kanisa Katoliki Jimboni Rulenge-Ngara, wamesitisha kabisa Ibada/misa. Watu wasali nyumbani! Pia amewataka waumini wajikinge na COVID-19 na kuchukua tahadhari


Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge-Ngara limesema limesitisha Ibada za Misa, maadhimisho mengine yanayokusanya Waumini wengi Kanisani na sala za Jumuiya kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia Aprili 19, 2020

Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo hilo amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kutafakari alama za nyakati na kujifunza kutoka kwa watu wa Ulaya, Marekani na nchi za jirani na hatua ambazo Baba Mtakatifu alizichukua kwa kutoa maelekezo kwa Maaskofu Wakatoliki Duniani na namna ya kuadhimisha Ibada

Amesema pamoja na kumshukuru Rais Magufuli kutotoa amri ya kufunga Makanisa na Misikiti, akihimiza kufanya ibada kumuomba Mungu atunusuru na janga hili, kama Mchungaji wa Jimbo la Rulenge-Ngara ameamua kuchukua uamuzi huo

Aidha, Askofu Niwemugizi amesema pale itakapowezekana wataomba redio Kwizera irushe adhimisho la Misa fupi na Waamini wafuatilie redioni. Baada ya mwezi kuisha Kanisa litaangalia hali ilivyo ili kama iliongeze muda

Pia, amewataka mapadre kuadhimisha misa peke yao kwa niaba ya waumini kuwaombea na kuiombea dunia ili Mungu atunusuru na #COVID19 hili na kuagiza sala za Jumuiya kufanyika ndani ya familia kwa familia moja moja
View attachment 1422602
Mtu yeyote mweye akili timamu na Upako wa Mungu atafanya hivyo! Huyu ndiye kiongozi wa Kiroho, siyo wa dini. Wa dini ni akina Mwamposa, Gwajima &Co.Ltd
 
Roma Locuta Est, Causa Finita Est = "Rome has spoken, the case is closed".
Umenikumbusha mbali. Wakati ule nilipokuwa nawakikisha vijana, wakati wa kikao cha Baraza la Kichungaji la jimbo ambalo Mwenyekiti alikuwa Baba Askofu, wajumbe ni ngazi ya jimbo na mapadre wakuu wa dekania, kulikuwa na ajenda ya kukea miito mitakatifu. Baada ya maoni ya sisi wajumbe wote kusikilizwa, mwishowe Baba Askofu, bila ya kujali wangapi mmeshauri nini, alisema, "Roma Lacuta" kisha akaeleza kitakachotakiwa kufanywa.
 
Back
Top Bottom