#COVID19 Askofu Niwemugizi, asitisha Misa na Ibada zote Jimbo la Rulenge, awataka waumini Wasali Majumbani pia Wajikinge na Corona

Umejiunga jf juzijuzi tuu.lkn unadandia kila topic,huku ukijitanabaisha kama mpinga sugu wa mbeya.hebu kua muungwana,usituonyeshe jinsi ulivyo zero brain,utakwama tuu.ccm oyee
 
Naunga mkono hoja ya Askofu. Naitaka serikali yangu ya Tanzania ichukue hatua madhubuti ili kuwakinga watu dhidi Corona.
Serikali ijifunze kuwa mara baada sikukuu ya Pasaka wagonjwa wameongezeka maradufu kwa sababu ya mikusanyiko iliyopindukia. Hivyo naitaka serikali ifuate nyayo za Askofu Niwemugizi kwa kutekeleza yafuatayo:
Moja, Mikusanyiko yote mikubwa ipigwe marufuku.
Pili Askari kanzu wawekwe kwenye stendi na vituo vya mabasi ili kuhakikisha ile social distance inazingitiwa nchi nzima. Ifahamike kuwa hii ni Vita na wakati wa Vita Askari ni lazima wawe mstari wa mbele kuwatetea wananchi. Amiri Jeshi mkuu Sasa ndio wakati wa kuwatumia Askari kwa manufaa ya Watanzania, siyo kwenye korosho za hasara.
Nne, Kuwe na lockdown ya safari za wakazi kutoka mji mkubwa mmoja kwenda mahali pengine hasa maeneo ya vijijini.
Tano, masoko na minada ipangwe kwa Askari kuhakikisha watu wanazingatia umbali wa kukaa, kupanga bidhaa au wanyama wao wanaouzwa
Sita, maji yasikatike kwenye miji yenye wakazi wengi. Kwa kuwa kipindi hiki maji yanatumika sana, serikali itoe fedha na kuzipa mamlaka za miji na majiji ili kuwapunguzia watumiaji gharama.
Saba, Makonda na wakuu wengine wa mikoa viherehere wadhibitiwe ili waache matamko ya kibabylon.
Hongera Askofu.
 
Michango kama hii ikiwa mingi inaweza 'kuwaamsha'. Kuna wanaosifia hata 'uharo bin uharisho'.
 
Bado hawa wapiga makelele sijui watafunga lini tupumzike na maspika mitaani
 


Amenifurahisha sana.
Nikienda huko Ziwa Magharibi nitamtembelea kumsalimia. Ametoa mfano wa kuigwa.
 
Ingependeza Askofu wa DSM angekuwa wa kwanza.
Lkn huu ni mfano naamini wengine watarespond

Haitii akilini kuzuia ibada ya jumuiya na kuacha misa zenye watu wengi.

Atafanya hivyo sababu sasa jimbo la Dar lina askofu wa kanisa.Hapo nyuma tulikuwa na askofu wa CCM
 

Kadinari sio daraja ni hadhi askofu ana mamlaka kuliko kadinari maana ata mlei wa kawaida anaweza kuwa kadinari


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ungekuwa mpole ukawaza vizuri huenda usingetukana! Haitakiwa tusubiri iwe Kama ilivyo kwa Papa ndo makanisa yafungwe! Inatakiwa tuchukue hatua mapema ili tusifike huko

Waswahili wanamsemo wao usemao 'ukiona mwenzio ananyolewa, chako tia maji" walikuwa na maana kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
 
Atafanya hivyo sababu sasa jimbo la Dar lina askofu wa kanisa.Hapo nyuma tulikuwa na askofu wa CCM
Hapana
Umekosea.
Kila mwenye daraja anafungwa kwa cannon law kufanya siasa au kushiriki siasa kwenda kupata Madaraka au kukalia kiti cha maamuz. Askofu hafungwi kuwa na maoni binafsi ambayo hayapingi imani ya kanisa.

Kuwa na mapenzi na ccm basi yupo mwenye mapenz na cdm hivyo hawapaswi kufanya maamuz ya kufundisha, kutakatifuza na kuchunga kwa kutumia hayo mapenzi bali imani ya kanisa na fadhila za kimungu na kibinadamu.

Daima maoni ya Askofu yule hayakuwahi kuathiri kanisa LA DSM kwa utendaji. Na alifanya vizuri mpaka ( yesu aliposhushwa msalabani) staafu kwa sheria.

Mheshimu tafadhali kwani si kosa kutofautiana mtazamo. Licha ya kupinga mawazo ya maaskofu wenzake lkn waamini wake walipata kufundishwa maoni hayo. Je si fadhila hiyo.
 
Kwa utaratibu wa Roman Catholic Church, Askofu haripoti kwa Kadinali. Kadili kazi yake kubwa ni kumchagua Papa.

Mara nyingi kadili huwa pia ni Askofu japo siyo lazima. Unaweza kuwa kadinali na usiwe Askofu wa Jimbo lolote.

Ulikwishawahi kusikia jambo mara moja Kadinali Pengo akiwapa maelekezo maaskofu?
 
Washauri wa papa na warithi kiti cha petro.

Kwa sasa wanateua wenye daraja tu.

2017 papa aliteua padri kuwa kadinali toka Asia
 
Askofu pekee mwenye akili timamu Tanzania.
Wengine wote ni majanga tu bila kujali dhehebu.

Huyu akili zake sawa na imamu wa ule msikiti wa dar uliositisha matumizi hadi waandae utaratibu mzuri utakao punguza hatari ya maambukizi ya hili gonjwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…