Askofu Niwemugizi: Nyerere angekuwapo angewacharaza CCM viboko

Tokea Lini? Yule Kassim Hänga aliyempeleka kuuwawa huna habari yake? Na vipi Kambona alimfanya nini ??
 
Tokea Lini? Yule Kassim Hänga aliyempeleka kuuwawa huna habari yake? Na vipi Kambona alimfanya nini ??

Wapi uliposikia makosa mawili yakafanya moja kuwa sahihi?

Wako wapi Azory, Ben, Lijenje?

Nani walikuwa kwenye viroba?

You're very guilty!
 
Namheshimu sana Baba Askofu Niwemugizi, na wachangiaji wengine. Ila tuweke sawa mambo; Mwalimu alipenda kusikia hoja siyo porojo..
Baba Askofu angeweza kujenga hoja bila kujadili CCM au viongozi wa Serikali.

Kwa sababu maono ya Mwalimu yanagusa hadi viongozi wa upinzani , ambapo vipo vyama vinatumia ruzuku ya kodi za wananchi kununulia magari used tena kutoka kwa viongozi wao bila kufuata taratibu za manunuzi. Huku ni kukiuka maadili na miiko ya uongozi. Ni ufisadi.

Kwa hiyo Mwalimu asitumike kuchapa fimbo upande mmoja. Mwalimu alipenda hoja za kitaifa. Alitaka vyama vingi ili viiamshe CCM kwa hoja.

Tukumbuke huyu ni mwasisi na Baba wa Taifa. Hakutaka pia vyama vingi vya upinzani viwe vya wezi, viongozi vibaraka na wasaliti wa Taifa (Tafuta hotuba ya Mwalimu anang'atuka Uenyekiti wa CCM Agosti 16, 1990).

Hivyo, na-challenge hoja ya Baba Askofu Niwemugizi haiko balanced hasa anapomjadili Mwalimu. Bahati nzuri mimi ni mjukuu mfuasi wa falsafa za Mwalimu na siasa za umajumui wa Afrika wa kizazi kipya.
 
Mi natofautiana na wengi nyerere ndo chanzo cha matatizo mengi tuliyo nayo kumsifia bila kumchallenge ni upumbavu

Hapana utakuwa umewahi mno kurukia kwenye conclusion.

Nyerere alikuwa Jembe mno kuliko hawa!

Uzi huu title yake ilikuwa "Mjue Nyerere in a Nutshell" bahati mbaya @mods wamekarabati kichwa kikaingia maji:

Mwalimu Nyerere alipunguza mshahara wake kwa uzalendo

Kukupa picha.

Nyerere alikuwa binadamu na kiongozi bora mno kuliko hawa.

Kuwa bora kuliko hawa hakuna maana ndiyo alikuwa optimal.
 
Comment ya DHAHABU....

Mkuu wangu kukosoa ni kazi rahisi mno haswa mtu akiwa "biased"......
 
🤣🤣🤣
 
Ni hayati Nyerere aliyevifuta vyama vya upinzani ule mwanzo wa KULIJENGA TAIFA.....kwa kuogopea "miluzi mingi humpoteza mbwa".....

Ni Nyerere aliyevirudisha kwa kutambua kuwa yalifanyika makosa
 
Yupo sahihi sana kiongozi
 
Alichofaulu Nyerere ni kudhibiti mabaya yake yasijulikane.Magu alishindwa sababu ya teknologia.
 

Unilaterally - "kujidhania wewe ni mjukuu mfuasi wa falsafa za mwalimu" ni kujilisha upepo.

Kwa maneno mafupi Baba Askofu Severine alichosema ni kuwa muumini wa CCM ya Nyerere hawezi kuwa muumini a CCM hizi tunazoziona.

Mengine ya kwako labda kama ni jitihada za kutengeneza pambio ambalo kuliimba utakwama tu.

Tafadhali jitahidi kutengeneza hoja yako badalq ya kujaribu kutumia ya baba askofu kusukuma agenda zako zilizo nje kabisa ya uwanja.

Uko nje ya uwanja mkuu.
 
CCM ya Nyerere na CCM hii ni moja. Misingi ya kuanzishwa kwake kwa kuunganisha TANU na Afro (ASP) mwaka 1977, ni ileile. Kama hoja yako ni hii (siamini kama ndiyo ya Baba Askofu ), basi iko very subjective in its realistic measures.😀😀😀
 
Huyu Askofu kasahau historia Ina maana ajui yaliyomkuta tutemeke sanga,kassanga tumbo,kambona,bibi titi, mohamed seif,james mapalala,nk.Nyerere alikuwa ni cold black dikteta na sio pure blood dikteta.
 

Ninakazia:

"muumini wa CCM ya Nyerere hawezi kuwa muumini wa CCM hizi tunazoziona."

Unaelewa maana yake?

Hicho ndicho alimaanisha baba askofu wala si fimbo katika uelewa wako mfinyu.
 
Ninakazia:

"muumini wa CCM ya Nyerere hawezi kuwa muumini wa CCM hizi tunazoziona."

Unaelewa maana yake?
Nami nakazia; hakuna tofauti ya misingi ya CCM ya mwaka 1977 na CCM ya October 14, 2021. Ni hivyo tu yaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…