Nami nakazia; hakuna tofauti ya misingi ya CCM ya mwaka 1977 na CCM ya October 14, 2021. Ni hivyo tu yaani.
Haaaah...sasa angalau umekuja ktk hoja nyingine tofauti na CCM ya Nyerere na CCM ya sasa. Naweka sawa; misingi ya CCM ni ileile ya mwaka 1977 na sasa.
Hii hoja yako ya pili sasa, nayo inahitaji uthibitisho.
Tatu, kama ni kuzungumzia misingi ya Mwalimu ktk maadili na miiko ya uongozi, basi inagusa hadi wapinzani. Kwani Mwalimu alitaka CCM na vyama vya upinzani vizingatie miiko na maadili ya uongozi, utu, demokrasia , utaifa, uzalendo na kulinda Uhuru wetu.