Askofu Niwemugizi: Rais Magufuli aliagiza nirejeshewe Passport yangu na alisema 'Wewe ni Askofu wangu utanizika'

Askofu Niwemugizi: Rais Magufuli aliagiza nirejeshewe Passport yangu na alisema 'Wewe ni Askofu wangu utanizika'

Hapa kuna chai kidogo kwa hiyo alijuaje kwamba yeye atatungulia kufa amuache Askofu kiasi kwamba amwambie yeye ndo atamzika?
Kwani mtu anapoandika wosia huwa ana uhakika gani kuwa yeye atatangulia na kuwaacha warithi? Hata angekufa Askofu kabla Rais angesema huyu Askofu nlimwambia atanizika lakini leo ni mimi namzika
 
Huko FB kumechafuka! Sasa hizi fake account zitachafuana sana. Nimesoma tuhuma kwenye wall ya Veronica France huko FB sijui tutafikia wapi.
Huyu anapaswa kuitwa mbele ya vyombo husika vimuhoji kulingana na tuhuma anazo toa ili zifanyiwe kazi kwa sababu baadhi ya tuhuma hizo Ni chonganishi saba
 
Askofu nae aache unafiki siku zote kwa nini hakutangaza ?ina mana hata Magufuli asingekufa ni lini tungejua kuwa alirejeshewa.hu msiba tutaona na kusikia mengi.

Kuna tetesi tena kilya kwa hery.

Naomba niishie hapo tafadhali.
 
Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi amesema aliyekuwa Rais wa Tanzania marehemu, John Magufuli aliagiza arejeshewe hati yake ya kusafiria na alimtamkia mara mbili kuwa kiongozi huyo wa kiroho ndiye atakayemzika...
Siku hizi viongozi wengi wa kiroho wameacha kusema ukweli, hawana tofauti na wanasiasa
 
Siku hizi viongozi wengi wa kiroho wameacha kusema ukweli, hawana tofauti na wanasiasa
Neno la Mungu ndio kweli.pekee

Maneno mengine yote sijui Tume huru sijui katiba mpya sio neno la Mungu na hivyo sio kweli.Yesu alisema Neno la Mungu ndio Kweli .Tume huru na katiba havikutungwa na Mungu.Askofu anatakiwa kusimama kwenye neno la Mungu sio matungwa na wanadamu yawe katiba au tume
 
Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi amesema aliyekuwa Rais wa Tanzania marehemu, John Magufuli aliagiza arejeshewe hati yake ya kusafiria na alimtamkia mara mbili kuwa kiongozi huyo wa kiroho ndiye atakayemzika.

Akizungumza leo Alhamisi Machi 25, 2021 katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato, Askofu Niwemugizi ambaye hakutaja muda maalum wa agizo la kurejeshewa hati hiyo, amesema Magufuli aliagiza idara ya uhamiaji kumrejeshea.

"Kwa kweli niwaambie mara mbili, Magufuli aliniambia, ‘wewe ni Askofu wangu utanizika. Mwaka ule 2015 akaniambia hivyo, mara ya pili akamwagiza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anirudishie passport akaniambia wewe ni Askofu wangu utanizika.”

Wasalaamaidi, soma: Askofu Niwemugizi wa Kanisa Katoliki aitwa Uhamiaji kuhojiwa juu ya uraia wake
Alijuaje kama atakufa yeye mwanzo? Au ndio ile ya Kipanya tengeneza tatizo halafu litatue ili uonekane wewe ni mwema?
 
Sasa naelewa kwanini Magufuli alitubu kabla hajakata roho .

Uongo jamani si mzuri, ni lini , wapi na mbele ya nani aliweza kutubu na ni dhambi gani, lete picha akitubu
 
Mwaka 2017 Askofu Severine Niwemugizi wa jimbo katoliki Rulenge alitoa ushauri kwa Rais Magufuli kuhusu mchakato wa katiba mpya.

Askofu alisema ni vizuri mchakato wa katiba mpya ukaendelea.

Siku chache baada ya kutamka hayo, Askofu alifuatwa na maofisa wa uhamiaji na kumtaka afike ofisini kujieleza. Maofisa walitilia shaka uraia wake na kwahiyo walitaka vithibitisho vya kuwa Severine Niwemuhizi ni raia wa Tanzania. Ifahamike kuwa Askofu Niwemugizi aliwahi kuwa Rais wa baraza la maaskofu katoliki (TEC) kuanzia mwaka 2000 hadi 2006 na baadae kuwa makamu wa Rais wa baraza hilo mwaka 2010 hadi 2015.

Baada ya wito wa maofisa wa uhamiaji, Askofu alitii amri bila shuruti. Alitakiwa kukabidhi hati ya kusafiria, kitambulisho cha kupiga kura na cheti cha kuzaliwa. Nyaraka zote hizo zilizuiwa na idara ya uhamiaji na kwahiyo Askofu hakuweza kusafiri wala kupiga kura (kama kungekuwa na uchaguzi).

Kwa mujibu wa Baba Askofu Severine Miwemugizi, alizaliwa tarehe 3 Juni 1956 katika kitongoji cha Kayanza, kijiji cha Kabukome, kata ya Nyarubungo, wilaya ya Biharamulo. Alibatizwa katika parokia ya Katoke, Biharamulo, akasoma shule ya msingi Katoke na baadae sekondari ya Nyakato, Bukoba. Safari yake ya utumishi ilianzia Seminari kuu ya Ntungamo, Bukoba kisha akaendelea Seminari ya Kipalapala huko Tabora.

Askofu Severine Niwemugizi alirudishiwa nyaraka zake mwaka 2020, siku chache kabla ya uchaguzi mkuu.

Kesho Ijumaa, Askofu Severine Niwemugizi ataongoza misa ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania, John Pombe Joseph Magufuli.
FB_IMG_1616679771078.jpg
FB_IMG_1616679773330.jpg
 
"Mimi nimemsikia akisema kule Dodoma kwamba yale aliyoyatamani Magufuli yakiwa katika nchi ya Tanzania yeye atayakamilisha. Kati ya aliyotamani Magufuli nakumbuka mwaka 2009 nafikiri nilikuwa hapa alimwambia Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda kuwa alitamani kuona Chato inakuwa makao ya mkoa, sasa sijui mheshimiwa Samia atalikamilisha," amesema.

Mwananchi

Hawa wateule wa Magufuli watampa shida sana Rais Samia asipokuwa makini.

Kwa kuwa JF ni kama maktaba inayojitosheleza, embu tufukunyue tuone kama hii kauli iliwahi kweli kutolewa mwaka 2009. Na kwa nini wakati watu wanapiga kelele za CHATO, serikali haikukiri kuwa Rais alikuwa na ndoto za kupafanya makao makuu ya mkoa. Hiyo ingezima malalamiko yote yale au kuyaweka katika muktadha mwingine.

Hii ni kauli hatari sana kisiasa kwa Rais Samia. Naona kama kauli hii imetolewa sasa kama shinikizo. Wanataka Rais Samia aendeleze miradi ya CHATO kwa jinsi ilivyokuwa imepangwa na Magufuli, otherwise wafuasi wa Magufuli watamuona ni msaliti na hilo litamgharimu mbele ya safari.
 
Hakika duniani hakuna aijuaye kesho, natamani askofu awapige vijembe kwenye mahubiri yake kesho.
 
Back
Top Bottom