Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna katuni ya Kipanya inasema kuwa mwanasiasa ni kuleta tatizo halafu unalitatua.Aliyeagiza anyanganywe ni nani ?
Its bygone, amsalie tu sala njema. Yeye ni mtumishi wa Mungu, Je Mungu tumuabuduye asemaje juu ya visasi?Hakika duniani hakuna aijuaye kesho, natamani askofu awapige vijembe kwenye mahubiri yake kesho.
Biblia haitufundishi kurudisha kisasi.Mimi ningekuwa askofu ,ubaya ubaya tu
Kudddddadeeeeeeki
Hata mimi najiuliza hili swali.Hapa kuna chai kidogo kwa hiyo alijuaje kwamba yeye atatangulia kufa amuache Askofu kiasi kwamba amwambie yeye ndo atamzika?
Uzi kuhusu Bishop Severine umeisha ongelewa sana hapa Jukwaani.Mhashamu Baba Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara,amesema kuwa Hayati Rais Magufuli alimtamkia mara mbili wakati alipowataka Maafisa Uhamiaji kumrudishia Hati yake ya kusafiria,Kadi ya kupigia kura na Cheti cha kuzaliwa kuwa yeye Askofu ndiye atakayemzika.
View attachment 1734259
Sasa si uhamiaji walikuwa wakichunguza uraia wake? Iweje Magufuli aingilie kati uhamiaji kabla hawajakamilisha uchunguzi wao na kuwaamrisha warudishe? Au yeye ndiye aliyewatuma huku akijua kabisa uraia wake hauna shida[emoji1787][emoji1787]Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi amesema aliyekuwa Rais wa Tanzania marehemu, John Magufuli aliagiza arejeshewe hati yake ya kusafiria na alimtamkia mara mbili kuwa kiongozi huyo wa kiroho ndiye atakayemzika.
Akizungumza leo Alhamisi Machi 25, 2021 katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato, Askofu Niwemugizi ambaye hakutaja muda maalum wa agizo la kurejeshewa hati hiyo, amesema Magufuli aliagiza idara ya uhamiaji kumrejeshea.
"Kwa kweli niwaambie mara mbili, Magufuli aliniambia, ‘wewe ni Askofu wangu utanizika. Mwaka ule 2015 akaniambia hivyo, mara ya pili akamwagiza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anirudishie passport akaniambia wewe ni Askofu wangu utanizika.”
Wasalaamaidi, soma: Askofu Niwemugizi wa Kanisa Katoliki aitwa Uhamiaji kuhojiwa juu ya uraia wake
Iweje Rais aingilie taasisi ya uhamiaji kama kweli ilikuwa na sababu za msingi za kuchunguza uraia wake? Hii si rushwa au matumizi mabaya ya madaraka?Rais hata akikohoa ni amri ....
Hiyo Passport itakuwa imerejeshwa mambo yashaharibika, na inawezekana kabisa sio Magu aliyeagiza bali ni kama ilivyokuwa ishu ya akina Halima Mdee na covid 19 yao. Mzee kavuta. Mzikaji wa Rais ni Askofu. Askofu umemnyang'anya Passport. Unafanyaje? Yale yale ya akina Halima Mdee.Sasa naelewa kwanini Magufuli alitubu kabla hajakata roho .