Askofu Niwemugizi: Rais Magufuli aliagiza nirejeshewe Passport yangu na alisema 'Wewe ni Askofu wangu utanizika'

Askofu Niwemugizi: Rais Magufuli aliagiza nirejeshewe Passport yangu na alisema 'Wewe ni Askofu wangu utanizika'

Aisee!
Sema mzee baba si ndo vile tena, hata ukimpa makavu hakusikii.

[emoji444][emoji445][emoji444]Nyumba yangu leo, ni chini udongoni
Hakuna mlango,
Hakuna madirisha
Kitanda changu, nalo blangeti langu,
Wameninyang'anya hata senti moja.
[emoji444][emoji445][emoji445][emoji445]
Tuishi kwa upendo.
 
Ndiyo Ukweli Wenyewe
Nasema Uongo Ndugu Zangu
 
Aisee, asikose kuwachana kuhusu haki za raia na usawa katika Taifa.
 
Hapa kuna chai kidogo kwa hiyo alijuaje kwamba yeye atatangulia kufa amuache Askofu kiasi kwamba amwambie yeye ndo atamzika?
Hata mimi najiuliza hili swali.
 
Mara nyingine watu wanaoohoji mamlaka huwa wanashighulikiwa na.machinery na sio mhusika mwenyewe....


Ndio maana jk aliwahi kuonya kuhusu kiongozi kuchunga ulimi wake na hisia zake maana hiwaumiza wengi...bilamwao wenyewe kujuwa....

Mfano siamini Kama jk alituma watu wakamuumize ulimboka....na yeye alisikitika pia na kumtakia pole
 
Mhashamu Baba Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara,amesema kuwa Hayati Rais Magufuli alimtamkia mara mbili wakati alipowataka Maafisa Uhamiaji kumrudishia Hati yake ya kusafiria,Kadi ya kupigia kura na Cheti cha kuzaliwa kuwa yeye Askofu ndiye atakayemzika.
IMG-20210325-WA0005.jpg
 
Mhashamu Baba Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara,amesema kuwa Hayati Rais Magufuli alimtamkia mara mbili wakati alipowataka Maafisa Uhamiaji kumrudishia Hati yake ya kusafiria,Kadi ya kupigia kura na Cheti cha kuzaliwa kuwa yeye Askofu ndiye atakayemzika.
View attachment 1734259
Uzi kuhusu Bishop Severine umeisha ongelewa sana hapa Jukwaani.
 
Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi amesema aliyekuwa Rais wa Tanzania marehemu, John Magufuli aliagiza arejeshewe hati yake ya kusafiria na alimtamkia mara mbili kuwa kiongozi huyo wa kiroho ndiye atakayemzika.

Akizungumza leo Alhamisi Machi 25, 2021 katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato, Askofu Niwemugizi ambaye hakutaja muda maalum wa agizo la kurejeshewa hati hiyo, amesema Magufuli aliagiza idara ya uhamiaji kumrejeshea.

"Kwa kweli niwaambie mara mbili, Magufuli aliniambia, ‘wewe ni Askofu wangu utanizika. Mwaka ule 2015 akaniambia hivyo, mara ya pili akamwagiza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anirudishie passport akaniambia wewe ni Askofu wangu utanizika.”

Wasalaamaidi, soma: Askofu Niwemugizi wa Kanisa Katoliki aitwa Uhamiaji kuhojiwa juu ya uraia wake
Sasa si uhamiaji walikuwa wakichunguza uraia wake? Iweje Magufuli aingilie kati uhamiaji kabla hawajakamilisha uchunguzi wao na kuwaamrisha warudishe? Au yeye ndiye aliyewatuma huku akijua kabisa uraia wake hauna shida[emoji1787][emoji1787]
 
Rais hata akikohoa ni amri ....
Iweje Rais aingilie taasisi ya uhamiaji kama kweli ilikuwa na sababu za msingi za kuchunguza uraia wake? Hii si rushwa au matumizi mabaya ya madaraka?
Au Rais anaweza kuingilia uchunguzi wowote kwa sababu ni wa watu wake wa karibu na yeye ni Rais???!
 
Sasa naelewa kwanini Magufuli alitubu kabla hajakata roho .
Hiyo Passport itakuwa imerejeshwa mambo yashaharibika, na inawezekana kabisa sio Magu aliyeagiza bali ni kama ilivyokuwa ishu ya akina Halima Mdee na covid 19 yao. Mzee kavuta. Mzikaji wa Rais ni Askofu. Askofu umemnyang'anya Passport. Unafanyaje? Yale yale ya akina Halima Mdee.

Lakini jamani, hivi si ni huyu Askofu alimzika dada wa Magu? Sasa ilikuwaje hii Passport ilicheleweshwa hivi? Maana Askofu alilalamika sio siku nyingi kwamba mambo yake mengi yanakwama kisa hana Passport. Kwani Magu hakujua huyu Askofu ndio atamzika? Maana alishachagua kuzikwa Chato!!
 
Back
Top Bottom