PostGE2025 Askofu Nkwande: Yaliyotokea Oktoba 29 ni fedhea kwa Taifa

PostGE2025 Askofu Nkwande: Yaliyotokea Oktoba 29 ni fedhea kwa Taifa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,933
Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mwanza, Mhashamu Renatus Nkwande amesema kilichotokea Oktoba 29 mwaka huu ni fedhea kwa taifa na kinalishushia taifa heshima iliyojengeka kwa miaka mingi kimataifa.

Akizungumza leo kwenye misa ya kuwaombea waliopoteza maisha kwenye vurugu zilizotokea wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29 iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Epifania Bugando, Nkwande ameonyesha kukerwa na matukio hayo huku akihoji kama ni kweli waliopoteza maisha haijulikani walikuwa wakipigania nini?.

"Hata hivyo wafu wetu hawa machoni pa wajinga wanaonekana wamekufa na kufariki kwa kunadhaniwa ni hasara yao, na kusafiri kwao kutoka dunia hii kuwa ni uharibifu kwamba kuondoka kwao walijitakia, walitafuta kifo, hivi ni kweli hatujui walichokuwa wakiomba, ni kweli hatujui walichokuwa wakikitafuta?,

 
IMG_8063.jpeg


Viherehere wengine wasiotaka kuelewa na wao zamu yao itawafikia kama huyo jamaa.

Nasikia alikuwa kibarazani tu jamaa wakampa na yeye risasi zake za kutosha.
 

Attachments

  • IMG_8063.jpeg
    IMG_8063.jpeg
    218.3 KB · Views: 32
Askofu huyu ameongea vizuri mno, nimependa sana wasilisho lake.
Asante sana Askofu mkuu Renatus nkwande, wajibu wetu ni kusiki na kutekeleza.
 
Back
Top Bottom