Askofu Nyaisonga avishangaa Vyama vya Upinzani kususia uchaguzi. Ahimiza waumini kujitokeza kupiga kura na kuchagua viongozi

Askofu ni kula kulala mnufaika wa sadaka zetu hivo ajui chochote wala hana uchungu wowote,angekuwa anabeba zege asingetamka hayo
Kazi anayofanya askofu, au kiongozi yeyote wa dini mkweli, anayetambua kwamba Mungu ni Mungu wa haki, kazi yake ni kubwa hata kuliko kubeba zege. Hapa Siongelei wachumia tumbo.
 
Mkuu umelikuza sana hili jambo, Tanzania haina mfanano wowote na Italy ya Musolin.

Sijui ni kwanini huwa hamtaki kuwafanya wapinzani wawe responsible kwa makosa yao??

Yaani kulialia tu kwa almost kila kitu.

Sijui tunajenga jamii ya aina gani??

Ambayo kuna ka kikundi ka watu hakataki kufuata utaratibu wowote ila kana haki ya kupata kila kitu.

Upinzani wetu na ufananisha na madereve boda boda barabarani.
 
Askofu wa TEC si mungu ni mwanadamu, Askofu wa TEC hawezi kuamua wananchi wamchague nani? Kiongozi wa dini mwenye hofu ya mungu atasema kweli daima hatapindisha ,Askofu mwenye hofu ya mungu huonya aonapo pindi serikali inapofanya sivyo ndivyo,

Askofu wa kweli yuko tayari kuwatetea wanyonge wapate haki zao.
 
Kwa Bwana Magu Kila Goti Litapigwa..

somo kutoka katika Waraka wa kwanza wa Nyaisonga kwa Wakatoliki

(1 Nya 2019 :18-8)
 
Daaahhh................yaaaani Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume.
 
Jana uzi huu niliupuuza sikutaka hata kuusoma nikafikiri tu kuna mkichaa mmoja kaja na yake, leo nimekuta thread nyingi kuhusu hili. Basi ni wazi kama aliesema hili ndio bossi wa TEC, kanisa katoliki limeamua kumkumbatia kaisari na kuacha watu wake wakione chochote kinachofikiriwa na wakubwa. Tuseme yaliyo moyoni nao hupita humu na kuyasoma nakila mwenye uwezo au sauti aseme yake kuhusu hili. Makanisa wakati wa UKUTA walikwenda kwa JIWE kujaribu kumkutanisha na WAPINZANI hadi leo JIWE amekataa, leo askofu anasema WAPINZANI wakae na kuongea na JIWE. Hivi wanafikiri yaliyotokea ni bahati mbaya serikali hii inaweza kuyabadilisha? Inasikitisha lakini ndiyo hivyo tena KONDOO wametelekezwa na mchungaji. Kanisa Katoliki lijitafakari tena.
 
Kuna baadhi ya viongozi wetu wa dini hakika kuna wakati wanajivunjia heshima wenyewe, sijui ni kwa nini wanashindwa kuiga mfano wa wenzao waliokuwepo wakati ule wa awamu ya kwanza ambapo serikali ilkuwa inawaheshimu sana na kila wakati serikali ilikuwa ikikumbana na changamoto yeyote ilikuwa ikiwaita kuwaomba ushauri, sasa hivi maswala ya imani za dini eti yanapelekwa serikalini kuomba ushauri, na matokeo yake serikali imewadharau viongozi wa dini nao wanahaha kujikomba kwake ili wapendwe, sasa hivi hata mkuu wa wilaya anaweza kutoa vitisho, kejeli, matamko na au maagizo kwa viongozi wakuu wa dini ?.
 
Binafsi nachukulia kwamba mjadala wa uhalali wa uchaguzi wa serikali za mitaa umefungwa rasmi kufuatia tamko la Baba Askofu Nyaisonga wa Kanisa kubwa kabisa nchini.

Awali wakati wa Baraza la Maulidi viongozi wa Bakwata wakiongozwa na Mufti Abubakar waliwataka Waislamu wote nchini kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa bila ya kuwa na visingizio vyovyote.

Naye Baba Askofu Nyaisonga ametoa wito kama huo wa kuwataka Wakristo wote na wale wenye mapenzi mema kushiriki uchaguzi huo kwa 100%.

Mjadala umefungwa, shime Watanzania tujitokeze kwa wingi 24/11/2019 kuchagua viongozi wetu wa serikali za mitaa.

Amen!

Maendeleo hayana vyama!
 
Tatizo la huyu askofu ni la kisaikolojia zaidi.
Huyu ni mtu anaeishi kambini bila familia. Hana mke , hana watoto na hajui uchungu wa mwana kama isemwavyo uchungu wa mwana aujuae ni mzazi.

Sasa mtu wa namna hii kumkabidhi jukumu la kuzisimamia familia ili hali yeye hana familia yake mwenyewe aliye iweza kwa kuisimamia ndio hivyo maumivu, maudhi, uonevu, ukandamizaji, ubabe na mengi ya namna hiyo hayata isha katika jamii inayosimamiwa na mtu wa aina ya askofu Nyaisonga.
 

Mkuu haya ni kama utani lakini ndio hivyo yanatokea. Tutarajie mabaya ya kutisha huko mbeleni.
 
Kanisa katoliki limeingia kwenye uporaji wa Democracy Ngoja tusubiri matokeo coz naona wamekubali kumsujudia Mungu MTU kiongozi wa Malaika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…