Unaushaid kwel wa kuthibisha Kuwa wapinzan hawataki kusikiliza Mawazo tofaut na udikteta wao Uko wap...!!? Eb Sema kat ya wapinzan na utawala nan hataki kusikiliza hoja za mwenzake...!!? Na kwann wasiskilizwe yanayowezkana kutatuliwa yatatuliwe kwa mjib wa sheria na katiba...!!!? Mfano
1) Wanahoji kuhusu mauaji ya kinyemela yanayoendelea japo wawe wanayatolea msistizo Ktk ufatiliaj... (Mfalme) kimya hasem lolote unadhan tutamuelewaj (dikteta asiye skia upande mwngne)
2) uchaguz Uko waz umechakachuliwa wako tu wanatoa porojo bila ya kufata taratb na sheria kusikiliza malalamiko ya wenzao... Japo kupunguza vinavyowezkana na waliofanya Hvyo iko dhahili Ila utawala Uko kimy nn hii (udikteta)
3) udikteta au unauelewaje wew?
4)wapinzan skuwa hawaung hoja za maendeleo lakin wanachokipinga ni kitumia mgongo na maneno ya maendeleo kwa wanyonge hku watu wenyew Ugum wa life unaendelea...!!! ( maendeleo Nkwa watu na sio vitu) na mtu akiulza hapew maelezo yenye fact na kueleweka,, ukihoj zaid umemkashifu Mkuu?? (udikteta)
Sasa na Dini ndio hvo hata Yale yanayoonekana kwel wanataka kugeuza Kuwa uongo na hawakosoi penye kosa hypoc...
Juzi nilimsikia mbunge mmoja wa Upinzani akishauri Bungeni kuwa Serikali inunue ndege ya mizigo.
Nilicheka sana.
Hawa ndio wapinzani tulio nao.
Wapinzani tangu Lipumba na Slaa walipoasi vyama vyao mpaka sasa hakuna wanasiasa wa upinzani wenye uwezo wa kujenga vyma vyao na falsafa zao kwa mbinu mbadala zinazoendana na wakati tulio nao.
Siasa za Kibabe kwa sasa zimekua kama siasa za dunia nzima.
Zinatofautiana tu kwa mazingira na aina ya upinzani uliopo.
Hata Marekani kuna mbabe trump lakini amebanwa na Katiba.
Wapinzani wa Tanzania in wasanii kuliko sanaa. Watawala nao wameshagundua udhaifu wa wapinzani wanaamua kuwatokomeza kabisa.
Hivi kuna tatizao gani kwa Wapinzani kuwatoa madarakani vibaraka wanaojiita wenyeviti wa maisha ili kujenga upya vyama vyao kwa kasi zaidi na kwa kujenga taifa lenye siasa safi.
Wakati Wa JK wapinzani walibanwa kidogo lakini kutokana na akili kubwa za za Dr. Slaa na Lipumba waliimba Mara moja kukutana na JK. Wakamueleza walichotaka kumweleza na matokeo yake Demokrasia ikazidi Kushamiri.
Hivi unafikiri Wapinzani wangeomba kukutana na JPM ili wamweleze kwa kina makusudio yao , nini wa wanamuunga mkono na nini wanapingana naye na nini ushauri wao ili nchi isonge mbele kidemokrasia na kimaendeleo angekataa??
Sidhani kama angekataa . Na kama angekataa hapo ndipo viongozi wote wa Dini wangewaunga mkono mana kila MTU angeshangaa Rais kukukataa kukutana na wapinzani wake wenye nia ya kujenga nchi na sio kubomoa.
Ni wazi kuwa upinzani unakufa kutokana na kubinywa na CCM na serikali yake lakini pia viongozi wana uwezo mdogo na mbinu ndogo sana kisiasa labda kidogo Zito Kabwe ndiye mwenye mbinu za kisiasa lakini anazidiwa na udogo wa Chama chake na kuwa na ruzuku ndogo.
Laiti Zito angekua anaongoza Chama chenye wapiga kura milioni 6 zilizotangazwa achilia mbali kuchakachuliwa Leo hii CCM wangeomba pooo.
Wapinzani bila kuwang'oa viongozi wanaojali maslahi na kutafuna ruzuku tu bila kujenga Chama hakika 2021 Tanzania itakua haina Chama cha upinzani chenye ruzuku.
Wapinzani wasitunishiana misuli na serikali kwa kutukana tu kwenye mitandao. Mbinu hii haina tija zaidi ya kujikuta wakiwa mahakamani na magerezani. Pesa zote za ruzuku zinaishia kwenye Kesi mahakamani.
Chagueni viongozi wenye uwezo ama wa kidiplomasia au walioko tayari kwa lolote bila kujali vyeo vyao na maslahi yao.
Sio unatangaza Ukuta halafu unapotea siku ya ukuta huonekani.
Unatangaza kusoma albadiri halafu siku ya kusoma unaingia mitini. CCM wanapita mitaani wanachana bendera wanapiga wapinzani halafu hakuna tamko LA maana zaidi ya kulia lia. Wakurugenzi wanaharibu chaguzi makusudi halafu wao wanapandishwa vyeo walioonewa wanaishia gerezani tena kwa sababu ya kulialia mitandaoani wanaambiwa wamechochea .
Ukiona una viongozi wasio na uwezo wa kuivuta jamii ikawaunga mkono kwenye maandamano basi ujue unapoteza muda.
Hivyo ni bora kubadili mbinu na kuendesha siasa za kidiplomasia.
Kuomba kukutana na Polepole, Bashiru Ally na mwaisho kuomba kukutana na Mkuu wa nchi ili waendeshe siasa za kusikilizana na kistarabu kwa pande zote.
JPM akielezwa kwa umakini na wa Tanzania wote tukaona jinsi viongozi wanajadili utaifa wetu na umoja wetu hakika asingeweza kukataa mapendekezo yao. Ila wao nao wawe tayari kupokea mapendekezo yake.
Nakumbuka alipoingia madarakani aliwashauri kuwa tuachane na mambo ya vyama na mikutano na maandamano ili tujenge kwanza nchi.
Akamshauri Mbowe kuwa ajenge makao makuu ya ChADEMA jijini DODOMA ,na aliahidi kuwapa eneo.
Badala ya Mbowe na wenzake kujadili hili zuri LA kujenga Makao makuu wakakimbila suala la kupigwa marufuku kwa maandamano.
Kuandamani ni haki ya watu lakini haina tija kama hakuna hoja za msingi za kuandamana.
Shule zinajengwa ,mabarabara ,madaraja, ufisadi unadhibitiwa,ndege zinanunuliwa ,ujambazi na ugaidi umedhibitiwa n.k. unataka maandamano yaruhusiwe ili nini?
Nafikiri tumekosa wapinzani makini wala sio serikali . Serikali inabadilika kulingana na mipango ya kidunia.
JPM ni Rais sahihi kwa mazingira ya sasa na yaliyokuwepo. Muda wake ukiisha basi atakua amepiga hatua kufikia malengo mapana ya muda mrefu.