Askofu Nyaisonga avishangaa Vyama vya Upinzani kususia uchaguzi. Ahimiza waumini kujitokeza kupiga kura na kuchagua viongozi

Baba Askofu mkuu amepotoka sana! Jamani hilo taahira lina dalili za madigiteta ndiyo maana linafanya kila juhudi kujipendekeza kwa kabisa ili wasilikemee! Yaani askofu anaanza.kukemea katikati badala ya kuanzia kule walikoanza.kuchafua mchakato!
 
Hadi kanisa lifafanue na kuhimaza. Hilo peke yake ni kuonesha kuna shida. Lakini kanisa linazungumzia kukaa meza moja, hivi ni kweli kanisa hilo halikupata kuona mwenendo usio sawa?
 
Hili jambo linanitatiza kidogo unamsoma mleta mada anasema Paroko nae kahubiri alichotumwa . Ahsante kwa kunikumbusha sio waraka au tamko la TEC.
Hapa kama ndivyo ulivyosema basi kanisa si la kubebeshwa lawama kama alivyochangia barafu na Malcom Lumumba
Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Peter O'bay naye amehubiri kile alichotumwa na wakubwa zake, kuhimiza watu wajitokeze kwa wingi katika uchaguzi
 
TEC na Bakwata ni vitengo vya CCM
 
Huyu Askofu hajielewi,Ni meza ipi ya mazungumzo iliyoandaliwa?

Kama haya ni maamuzi ya baraza,hii ni aibu kwa kanisa Katoliki ambalo tulitegemea likemee uovu lakini limeamua kushirikiana na watesi wetu.
 
Hakuna cha intelijensia wala upuuzi mwingine wowote. Huyu amesukumwa na urafiki wake binafsi na mtawala. Na hili tamko kwa vyovyote ni lake yeye binafsi na syndicate yake.

Huyu Askofu, analinajisi Kanisa Katoliki.

Uko sahihi, haiwezekani zoezi lililoendeshwa kwa uhuni wa kitoto kiasi hiki, kisha kanisa katoliki wasione na kutoa tamko la huyo askofu. Kanisa la RC kwa kauli hii linapaswa kujitathmini kwa kutoka kwenye haki na kuamua kuwa sehemu ya siasa chafu.
 
Kumbe ndo maana wanatuambia usiangalie matendo yangu ila iman ya kanisa lako,hapa nmenotise kitu na kwa hali hii watapoteza waumini wengi sana ikiwemo mm,bora hata kua kkkt kule atleast wana misimamo iliyonyooka
 
Safisana askofu hakika uliyoyasema ni mfano wa kuigwa kwa viongozi wa vyama vya siasa!kuliko kususa wangekaa meza moja na serikali! Ubarikiwe Sana baba askofu

How realistic is this proposition ya vyama shindani kukaa meza moja na serikali? Mimi sidhani inawezekana. Ingawa vingozi wetu wa sasa kila siku wanatenda kinyume na kauli zao tukumbuke kuwa Rais alishapata kudai kuwa hawezi kukutana na washindani wake kwa sababu anahofia wanamtuma Bahraini! Ukweli ni kwambà sababu zinazofanya asikutane nao ni zile zile zinazofanya vyama vya upinzani kufunguliwa kufanya siasa na vyombo vya habari kudhibitiwa.
 
Wakatoriki tuliyo wengi tunapenda kutii uongozi uliyowekwa madarakani kwa ridhaa ya wananchi bila kutumia nguvu, ghiliba ,wanataka haki itendeke kwa chaguzi zote.Hakuna mwananchi anayetaka abaguliwe,na kunyimwa haki zake za msingi kulingana na katiba.Viongozi wangeshauri tuwe na mazingira mazuri ya uchaguzi yaliyo sawa kama vyama vyote vilivyosajiriwa wakae kwanza waelewane maana sisi sote tumeumbwa kwa sura ya Mwenyezi Mungu ,waunde tume iliyo huru ya uchaguzi.Kama hakuna impartiality there is no need for election
 
Usituletee ujinga wewe askofu nyaisonga, sisi si wajinga, sisi ambao tuko katika vyama vya upizani sio wote ambao ni wakatoliki, na pia najua sio wakatoliki wote wanakuunga mkono, sikiza kwa maakiini wewe askofu, kama umekula hela ya ccm na mungu wa kina wanaccm magufuli sisi wengine hatujakula hela ya ccm na hatutaki hela iliyoimbiwa kota kwa walipa kodi,hatutaki hela ya magufuli na ccm yake, hujui vile wananchi wanaumia , wewe uko na hela ya kutosha, huna mke au watoto(hata kaa maaskofu wengine na mapadre wa katoliki wako na wasichana kibao wanaolala nao kwa siri)sisi ndio tunaumia huko kwa kukosa ajira, misharaha haijaongezwa kwa miaka 4,wapizani kubadikiwa kesi, wengine kupigwa risasi, waandishi wa habari kutekwa na kuuawa huko mto ruvuma, na wakati hii nyote inajili wewe mkuu wa katoliki na maaskofu wenza munapiga makofi tu, sababu? hamna shinda yeyote hela iko kibao ya sadaka, ikiisha munaitisha hela huko roma na mambo mengi, baba askofu LEAVE US ALONE WE OPPOSITION PLS, achana na sisi, endelea kuabundu mungu wako magufuli na binguni yake inayoitwa ccm, freedom will came one day, wewe askofu umekuwa kibaraka wa magufuli na wauaji wake wa uvccm
 
Binafsi Roha Mtakatifu ananielekeza kutopiga kura..!
 
 
Haya ni maoni ya Baba Askofu, naamini wote mmeyasikia na mtayaheshimu. Msimkashifu wala kumsemea yaliyo mabaya mtumishi wa Mungu kwa kutoa maoni yake ambayo kwake yeye anaamini yapo sahihi. Kutofautiana ni kawaida sana, tusiwe kama wale ambao watumishi wa Mungu wakinena yanayowafurahisha wanawasifu ila wakinena yasiyowafurahishi wanawakejeli na kuwaambia waache kuchanganya dini na siasa.

Katika kusimamia haki usiamini nguvu ya mtu mwingine yeyote bali nguvu yako tu. Baba hata Mama yako wanaweza kukuacha pamoja na kuwa wewe ndio unawatafutia chakula. Ni vipi kwa mtu mwingine anayejitegemea mwenyewe kwa kila kitu?
 
fumbo la mfumo ndani ya mfumo imejionyesha kama jua

na hii similarity inashangaza..

ameondoka Pengo ,watu wakashukuru alipokuja Ruwaichi..

Kutanabahi amekuja Askofu Nyaisonga...na mtazamo wake huku ukichagizwa na dhana ya mfumo...usioonekana lakini upo

*akili kumkichwa ndio hii ya Askofu nyaisonga
 
Kama na Kanisa Katoliki linalamba soli ya Jiwe basi halina maana. Nami nawatupia lawama maaakofu wote walio compromise na Serikali kwa sababu ya mahusiano mabaya. Hebu waenda DRC wakaona RC ilivyo shamiri
 
Hadi kanisa lifafanue na kuhimaza. Hilo peke yake ni kuonesha kuna shida. Lakini kanisa linazungumzia kukaa meza moja, hivi ni kweli kanisa hilo halikupata kuona mwenendo usio sawa?
Na halitakuja kuona kamwe ndani ya awamu hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…