Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Siyo kila asimamaye madhabahuni ni mtumishi wa Mungu. Mtawajua kwa matendo yao na kauli zao.
Haya ni maoni ya Baba Askofu, naamini wote mmeyasikia na mtayaheshimu. Msimkashifu wala kumsemea yaliyo mabaya mtumishi wa Mungu kwa kutoa maoni yake ambayo kwake yeye anaamini yapo sahihi. Kutofautiana ni kawaida sana, tusiwe kama wale ambao watumishi wa Mungu wakinena yanayowafurahisha wanawasifu ila wakinena yasiyowafurahishi wanawakejeli na kuwaambia waache kuchanganya dini na siasa.
Katika kusimamia haki usiamini nguvu ya mtu mwingine yeyote bali nguvu yako tu. Baba hata Mama yako wanaweza kukuacha pamoja na kuwa wewe ndio unawatafutia chakula. Ni vipi kwa mtu mwingine anayejitegemea mwenyewe kwa kila kitu?
Nauliza hivii...ongezeni sauti!.... Nauliza hivii....hapa kanisa halijachanganya dini na siasa!?!?!? Kwanini hawasikii!?!? So walishaonywa na aliyewaonya alikuwepo moja ya kanisa na wakatangaza waumini wasisahau kwenda kupiga kura!Akiwa katika Jimbo Katoliki la Shinyanga kuhudhuria Misa ya Jubilei ya kutimiza miaka 25 ya Upadre wa Padre Sangu Rais wa Baraza la Maaskofu (TEC) amewataka wakatoliki kuwapuuza baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaohubiri mgomo wa kugomea zoezi la uchaguzi wa viongozi ngazi ya serikali za mitaa utarajiwao kufanyika hivi karibuni.
Rais huyo wa TEC amekemea tabia ya Wanasiasa wasio na nia njema kwa taifa kwa kuhubiri uovu wa kugomea chaguzi zinazoandaliwa na serikali.
My take: Haya sasa wenye yao dunia wamenena!
Siyo kila asimamaye madhabahuni ni mtumishi wa Mungu. Mtawajua kwa matendo yao na kauli zao.
Wanadai siku ya hukumu wote tutapimwa kwa usawa,hakuna cha Askofu wala mhubiri wa neno la Mungu,itafahamika huko. Kama anaweza kutoka tu na kuwalaumu wapinzani kwa kujitoa kwenye uchaguzi bila kuhoji na kujua sababu za wao kujitoa sisi kama kondoo wake tumuelewe vipi Baba yetu wa kiroho? Wapinzani wanawezaje kujitoa kwenye uchaguzi bila sabubu na wakati uchaguzi ndio chakula chao? |
Mwenye yake dunia Ni Mungu Muumba wa Mbingu na Dunia, askofu Nyaisonga ni tope tu linalojipendekeza kwa serikali hii dhalimu eti tu kwa sababu inaongozwa na mkatoliki aliyekengeuka!!!Akiwa katika Jimbo Katoliki la Shinyanga kuhudhuria Misa ya Jubilei ya kutimiza miaka 25 ya Upadre wa Padre Sangu Rais wa Baraza la Maaskofu (TEC) amewataka wakatoliki kuwapuuza baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaohubiri mgomo wa kugomea zoezi la uchaguzi wa viongozi ngazi ya serikali za mitaa utarajiwao kufanyika hivi karibuni.
Rais huyo wa TEC amekemea tabia ya Wanasiasa wasio na nia njema kwa taifa kwa kuhubiri uovu wa kugomea chaguzi zinazoandaliwa na serikali.
My take: Haya sasa wenye yao dunia wamenena!
Sasa ngoja na sisi waumini tujenge uadui na kanisa letu tuone kama watawasalisha hao viongozi pekeeNiliwahi kueleza hapa jukwaani taarifa kutoka kwa Askofu mmoja kutoka inner circle ya Kanisa Katoliki. Mimi pia ni mkatoliki halisi wa imani aliyewahi kuhudumu ndani ya kanisa.
Askofu yile alieleza kuwa Kanisa Katoliki, baada ya waraka wa kwaresma, ulioeleza mapungufu mengi ya watawala wa awamu hii, uhusiano wake na mtawala mkuu ulififia sana kufikia hatua ya kujenga uadui. Inner circle ya Kanisa waliazimia kuurudisha uhusiano huo uliokuwa umezoeleka.
Hatua ya kwanza ilikuwa kumpata Rais wa TEC ambaye ana mahusiano binafsi ya karibu na mtawala, na huyo hakuwa mwingine bali huyu Rais wa TEC wa sasa. Hilo lilifanikiwa.
Na ninarudia tena, chini ya uongozi wa sasa wa TEC, msitegemee kauli yoyote ile kutoka TEC itakayokuwa kinyume na matakwa ya watawala. Kanisa, kama lilivyo bunge na mahakama, wamejumuishwa. Mark my words.
Mimi niliyasikia haya wakati wa kipindi cha kumpata Rais mpya wa TEC. Jambo la kujiuliza, hivi hizi dini zetu zipo kwaajili ya imani au maslahi fulani? Ni dini au watu fulani ndio wanaozifanya dini kuwa syndicate ya matakwa binafsi ya watu fulani?
Hatupangiwi ya mungu wampe mungu ya kaisari wamuachie kaisari.
Kujenga umoja wa kitaifa kama walivyofanya wakina Padre Athanase Seromba kwenye mauaji ya watutsi laki nane kule Rwanda, si ndiyo ???Nijuavyo mimi:
• Kanisa Katoliki huwa halifanyi mambo ili kumfurahisha mtu au kikundi cha watu.
• Kanisa Katoliki huwa halifanyi mambo kwa kufuata mkumbo wa watu.
• Kanisa Katoliki halifungamani na chama chochote cha siasa.
• Kanisa Katoliki halifanyi mambo ili kuongezea tatizo zaidi, bali huangalia namna nzuri ya kuleta umoja na mshikamano.
• Kanisa Katoliki halijawahi kuwa la kidemokrasia hata siku moja. Sikumbuki kama nilishalishuhudia au hata kusoma sehemu juu ya hili.
• Kanisa Katoliki hufanya mambo yake likizingatia misingi ya Ukristu likiamini hakuna mwanadamu mkamilifu.
Ninajaribu kujiuliza:
• Kuna sababu gani ya msingi ya kulifanya Kanisa Katoliki liunge mkono ususiaji wa uchaguzi?
• Sisi Watanzania, tukisusia uchaguzi, then what will be our next plan? What will we benefit from doing so? Will that change anything?
• Je, kususia uchaguzi ndio suluhusho pekee lililopo? Ndio CCM wata-retreat? Ndio kusema kuwa wataacha uonevu?
• Je, tukisusia uchaguzi, tutaleta umoja na mshikamano kama taifa, au ndio tutazidi kugawanyika?
Ninafikiri tunapaswa kutafuta suluhisho jingine. Hatuwezi kususia tu bila kuwa na reasonable plan nyingine.
Kanisa Katoliki lipo sahihi, kwa mtazamo wangu.
Hapana, kama lilivyofanya kumuunga mkono Benito Musolini katika mambo mazuri kama vile kupinga matumizi ya contraceptives, kutaja bure jina la Mungu, kuvunja ndoa kwa talaka, na mambo mengine kama hayo.Kujenga umoja wa kitaifa kama walivyofanya wakina Padre Athanase Seromba kwenye mauji ya watutsi laki nane kule Rwanda, si ndiyo ???
Kabisa, usisahau mambo mema kama kumuunga mkono kuchinja na kupora mali za Wayahudi zaidi ya elfu nane na kuwapeleka Borgo San Dalmazzo Camp na Fossoli ili Kanisa lipewe mji wa Vatican.Hapana, kama lilivyofanya kumuunga mkono Benito Musolini katika mambo mazuri kama vile kupinga matumizi ya contraceptives, kutaja bure jina la Mungu, kuvunja ndoa kwa talaka, na mambo mengine kama hayo.