Askofu Nyaisonga avishangaa Vyama vya Upinzani kususia uchaguzi. Ahimiza waumini kujitokeza kupiga kura na kuchagua viongozi

Askofu Nyaisonga avishangaa Vyama vya Upinzani kususia uchaguzi. Ahimiza waumini kujitokeza kupiga kura na kuchagua viongozi

"Madicteta Bwana!!! ujipenyeza kila sehemu.

Miskitini, Makanisani, Jeshini na idara zote za kiserikali na kijamii na vyombo vya habari

Ila uwa sio popular kwa wananchi na dawa ya madicteta uwa ni maandamano yasiyo na kikomo." Mimi ni mkatoliki pure but toka aingie Magufuli madarakani kanisa linafanya mambo mengi ya aibu na ya kipumbavu niwaambie tu viongozi misimamo yao sio misimamo ya sisi wananchi wakatoliki tunataka haki itendeke uyu itakuwa kahongwa sio bure.

Acha kuaminisha watu uongo. Yule Shoo wa KKKT yeye anayeongelea siasa na kuandika waraka mbona hamzunguzii.

Safari hii mtapata tabu sana. Hakuna kumbelezena ni mwendo wa kwenda mbele
 
Binafsi nachukulia kwamba mjadala wa uhalali wa uchaguzi wa serikali za mitaa umefungwa rasmi kufuatia tamko la Baba Askofu Nyaisonga wa Kanisa kubwa kabisa nchini.

Awali wakati wa Baraza la Maulidi viongozi wa Bakwata wakiongozwa na Mufti Abubakar waliwataka Waislamu wote nchini kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa bila ya kuwa na visingizio vyovyote.

Naye Baba Askofu Nyaisonga ametoa wito kama huo wa kuwataka Wakristo wote na wale wenye mapenzi mema kushiriki uchaguzi huo kwa 100%.

Mjadala umefungwa, shime Watanzania tujitokeze kwa wingi 24/11/2019 kuchagua viongozi wetu wa serikali za mitaa.

Amen!

Maendeleo hayana vyama!

Uzuri ni kuwa hao viongozi wa dini wote tunakutana kwenye kusaka Malaya hivyo tunajua hamna lolote watatambua. Huko kwenye dini wako kwenye utafutaji kama utafutaji mwingine.
 
Wengi wa viongozi wa dini wanapata habari za vyombo vya habari kama TBC, RADIO TANZANIA hawajui lolote nje ya hapo
 
Huo ni mtazamo wako!

Amen!
It is not a matter of mtizamo. kama jitu na eti uaskofu halioni attrocities wanazofanyiwa waumini eti kwa vile linachangiwa sadaka linakula, then hilo ni jihuni kama wahuni wengine!
 
Nimesikiliza mahubiri ya Askofu Mkuu na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tz,Mhashamu Askofu Nyaisonga, ameelekeza lawama zake katika vyama vya upinzani,akijenga hoja kuwa havikutumia busara na elimu katika kufikiri na kujitoa katika uchaguzi.

Amehimiza kuwa kujitoa sio suluhu,wanapaswa kukaa meza moja na serikali kutatua hiyo changamoto,amesisitiza kuwa waliojitoa wamekosea,hivyo kasema msimamo wa maaskofu Wakatoliki ni kutokubaliana na kusisia uchaguzi,na wamehimiza waumini kujitokeza wa wingi jumapili kupiga kura.

Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Peter O'bay naye amehubiri kile alichotumwa na wakubwa zake, kuhimiza watu wajitokeze kwa wingi katika uchaguzi, hii ni kusema, kanisa katoliki linaungana na Polepole, Jafo na TAMISEMI kuubariki uchaguzi wa serikali za mitaa ambao mchakato wake umejaa utata mtupu,utata ambao hata makada wazoefu wa CCM wanaona aibu kwa yaliyotokea. Hili ndio kanisa Katoliki na msimamo wake umetangazwa na Rais wa TEC. Kanisa limeridhika na mchakato, halitaki kugombana na serikali, limewakana waumini wake waliogoma toka mwanzo kujiandikisha kwa kuona ubovu wa demokrasia kwa sasa.

Katika maandishi ya kitabu cha "How The Church and Government Got The Same Bed", mwandishi alijaribu kuelezea kwa undani jinsi kanisa, na hasa kanisa la Vatican wakati mwingi lilivyoshiriki kuungana na serikali katika kuisaidia kufikia adhma yake, mwandishi ameeleza nafasi ya wamisionari katika kuitawala Afrika, jinsi walivyotangulia na kuwatengenezea njia wakoloni, kuanzia Congo ya DR mpaka Afrika ya Kusini,Kaskazini na Mashariki ya Afrika. Mwandishi anasema kanisa huangalia kwanza maslahi ya viongozi wake kabla ya waumini wake.

Inaelezwa kuwa wakati wa utawala wa Kifashisti kule Italia, Mussolini aliona tishio la Kanisa Katoliki ktk kufikia malengo yake. Maana kwa wakati ule, kanisa lilikuwa na ushawishi wa kila sekta ya maisha ya kiroho na kimwili na serikali ilikuwa na ushawishi mdogo tu ya maisha ya kisiasa.

Alichokifanya Mussolin ni kujipendekeza kwa kanisa na kutoa "rushwa" ili yote atakayoyafanya kanisa katoliki lililokuwa na nguvu sana Italia libaki kimyaa.Na Alifanikiwa...

Kwanza aliamua kumbatiza mwanae wa kiume, ambaye hapo awali hakuwa amebatizwa.Hapa akaliteka kanisa kwa karata ya kwanza.

Pili alimua kufunga ndoa ya kikanisa,baada ya kuwa amekaa miaka 11 na ndoa ya bomani na mkewe Rachele.Hii ikawa karata ya pili ya kujisogeza na kujiweka karibu na kanisa ili kutimiza malengo yake ya ufashisti.

Karata nyingine;aliamuru kufungwa kwa maduka yote ya vileo(wine shops) na kufuta leseni za clubs zote za usiku ili kuendana na kauli ya kanisa ya kupunguza uovu mitaani kwa ulevi na anasa za usiku.Hapa kanisa katoliki likanasa mtegoni.

Alienda mbali mpaka akatangaza kuwa "Public Swearing",yaani kujiapiza hadharani jina la Mungu kama "Public Crime"...Yaani mwananchi ukiwa mtaani mnabishana,mtu akikwambia sema Haki ya Mungu...Ukisema tu "Haki ya Mungu sijaenda nyumba ndogo mwezi wa pili sasa".Basi ujue wewe una kesi ya jinai ya kujibu.Hapa alitaka kulifurahisha kanisa kwa amri ile isemayo "Usitaje bure jina la bwana Mungu wako"

Mussolini akaamuru kupigwa marufuku vidonge vya majira na kampeni zote za matumizi ya uzazi wa mpango kama ulivyo msimamo wa kanisa.Wakati huo kanisa lilitaka wanawake wabaki nyumbani ili kulea watoto na kukuza familia vyema.Mussolini akalipigia chapuo hili na kulitungia sheria ili kuwafurahisha wazee wa kanisa.

Akatunga sheria ambayo ilifutilia mbali talaka kwa ndoa hata za bomani.Hii ilikuwa ni njia ya kuungana na kanisa ktk ndoa ya mke mmoja na isiyo na talaka mpaka Mungu awatenganishe.Ndoano hii ikanasa vizuri kwa kanisa.Hawakupepesuka wala kutikisika.Mambo yote ya ndoa yakaondolewa serikalini na kubaki kuwa in "Full Control of the Catholic Church".Wale wapenda mteremko wa ndoa za bomani wakakosa pa kwenda.

Akatoa 109 acres ktk mji wa Roma ili yajengwe makao makuu ya Papa(Vatican) baada ya kuwa yalipokonywa wakati wa "Unification of Italy" ya miaka ya 1870's,na akatoa amri kanisa lilipwe zaidi ya £130 milioni kwa wakati ule.Hii ilikuwa ni ndoano iliyoingia sawasawa kwa kanisa,na kanisa halikusema lolote juu ya "ufashisti" wa Mussolini hadharani;japo liliouona na kuuhisi kwake na kwa waumini wake.

Vatican ikawa nchi ndani ya mji,wakapewa mamlaka juu ya Post Office,jeshi dogo,polisi na "Rail station".Baada ya hapo,ugomvi ukawa ni nani anatakiwa ku-control Elimu?Mussolini alihitaji sekta ya elimu ili apandikize "ufashist" kwa watoto,na kanisa lilitaka elimu ili kupandikiza imani ya kikatoliki kwa watoto.

Mambo haya yote ambayo baadae,waumini wasio rasharasha waliona ni kama rushwa kwa kanisa ili liweze kusifia na kukaa kimya juu ya serikali ya kifashisti ya Mussolin yalifanikiwa.

Si ajabu Papa John Paul II alikuja kuiomba jumuiya ya waumini na wasio waumini ktk jubilei ya miaka 2000 ya Ukristo kwa yale yote kanisa iliyoyakosea ktk kukuwa kwake.Hili la kuukumbatia uonevu wa serikali isiyojali usawa ya Mussolini lilikuwa ni moja ya kosa la Kanisa.

Hakukuwa na Kardinali,askofu wala kasisi(padre) aliyeikemea serikali isiyo ya kidemokarasia ya Utawala wa Mussolini.Mengi yalitokea na kanisa lilikaa kimyaaa.Waumini waliteseka,waliumia na walipata machungu ya maisha...Lakini kanisa lilisema hewalaaa,huu ni utawala mzuri tu,maana umerudisha heshima ya Papa katika nchi ya Italia.

Hatumaanishi kuwa sasa Tanzania tuna ufashisti,lakini tunakubaliana kuwa kwa sasa Tanzania maisha ya chuki za kisiasa,mienendo ya kidemokrasia na ushiriki wa watu katika siasa huru umekengeuka sana.

Kuwa baba wa kiroho na kuongea kinyume cha yale waumini wako ambao ni sehemu ya wananchi wa Tanzania wanalalamika,ni kuwa upande wa pili badala ya ule wa waumini wako.

Ndio maana wale wanafunzi wa historia ya kale,wanaweza kustuka na kuona kuwa kanisa linaendelea kuwa upande tofauti na wanaoonewa.Kanisa libaki kuwa mali ya waumini wanyonge,liachane na urafiki wa mashaka kama ule wa Mussolini na Vatican enzi hizo za zama za giza za Ulaya.

Kama kanisa la wakati huo lilibaki kimya juu ya ufashisti wa Benitho Mussolini,hili la kwetu la Tanzania,lisibaki kimya juu ya uonevu wa kidemokrasia,vurugu za kuinajisi demokrasia unaonekana kufanywa waziwazi kabisa na serikali.Kutoa kauli za aina hii hadharani,mbele ya mimbari na katika altare takatifu,inatupa mashaka na tutaamua kurudi na kupekua kurasa za kitabu cha "How The Church and Government Got The Same Bed"

Tukizifunua kurasa hizi;Tutahitimisha kwa kusema,Rais wa TEC amesimama upande wa serikali,amesimama na wanaodhaniwa kuminya demokrasia na mizizi yake,taswira ya waumini ambao ndio raia wenyewe kutokupendezwa na haya yanayoendelea haujaletwa na vyama vya upinzani,maana waumini walianza kugoma kujiandikisha mpaka pale walipohimizwa kwa lazima.

Hizi ni dalili kuwa si tu hatua ya kugomea uchaguzi imeasisiwa na vyama pinzani,bali ilishaanza kutendwa na waumini ambao ndio wapiga kira wenyewe.

Tutamkumbusha RAIS WA TEC na Askofu Mkuu wa Mbeya Nyaisonga kuwa kuutumikia mwili ni gharama zaidi ya kuitumikia roho.Ndio maana Lugha Mama ya Kanisa ya Kilatini ikasema "Nemo Liber Est Qui Corpori Servit"(No One is Free who is a slave of his body)

Tuitumikie Roho inayodumu milele,kuliko mwili unaooza na kuliwa na nyenyere.
View attachment 1265377
View attachment 1265378
Hawa wote ni wahuni, wana watoto mitaani!
 
Hakuna mwenye clip ya huyo Askofu? Tunaomba tuipate ili iwe kielelezo katika malalamiko yetu. Msimamo wa Papa upo wazi - hataki kulifungamanisha Kanisa na watawala dhidi ya watu wa kawaida/maskini.

Kama Wakatoliki au mtu yeyote ana uwezo wa kufikisha malalamiko yake kwa Papa. Naye kwa kutumia watu wake atachunguza ukweli wa malalamiko yaliyotolewa.
 
Mungu wangu mbona naona uchungu kuendelea!!! kuwa kondoooHHH,
Baba hata sababu za kususia huzitaji tupige kura tuuuuhhh aaahhhh waaapiiii!!????
 
Hakuna mwenye clip ya huyo Askofu? Tunaomba tuipate ili iwe kielelezo katika malalamiko yetu. Msimamo wa Papa upo wazi - hataki kulifungamanisha Kanisa na watawala dhidi ya watu wa kawaida/maskini.

Kama Wakatoliki au mtu yeyote ana uwezo wa kufikisha malalamiko yake kwa Papa. Naye kwa kutumia watu wake atachunguza ukweli wa malalamiko yaliyotolewa.
mbona imeambatanishwa hapo juu kwenye uzi?Au hujaiona?
 
Kiongozi wa dini..vs...kiongozi wa kanisa...apo pananipa tabu sana...mim mkristo lakini jamaa sio kiongozi wangu
 
Yaani wanajukwaa mie nalisema Hili Ila Kama lilikuwepo bas ndio Hvyo....!!! Tangu uhuru Mpk sasa Dini zote kubwa hapa Nchini zilichangamana si Uislam au Ukristo(Roma) zingatia haya....!!!
Wakati wa Muungano Tanganyika na Zanzibar, Tanganyika iliongozwa na mtawala ambaye ni Mkristo(Roma) ambao asingeweza kuunganisha Zanzibar iliyotawaliwa na mwalabu (Muislam) bila makubaliano yoyote.....!!!
Ili kukamilisha azima ya Muungano uwe na USAWA na kuepusha vita kuwepo Kati ya Mzanzibar na Mtanganyika ilibid JK kupata ridhaa ya Kidini ili kupenyeza Swala la siasa...!!!
Wakaingia makubaliano ya kubadilishana Swala la Utawala ndipo ikawa Kwa Kuwa yeye ndio chocheo la Muungano huo akaruhusiwa Kuwa mtawala wa kwanza wa Muungano....!!!! Akawa Raisi wa kwanza (Mkatoliki) Ila Ikumbukwe Kati ya makubaliano ilikuwa Utawala wa kupokezana Yaani Akitoka Mkristo anafata Muislam.... (Mark hilo neno) Ndipo uongozi ulivyokubaliana ili Muungano uwe SAWA...!!
Hii ilichukuliwa Kidini zaid Ila Kuwa na SURA ya KISIASA ndipo waliposema "Serikali haifungamani na upande wowote wa Dini" lakin Kumbuka utawala wa kupokezana ndio utaratib na SERA za chama japo ""Sio wazi katika vitabu vya SERA zao za chama"" Ebu tujikumbushe mfano wa Utawala wa kupokezana
(1)JK NYERERE(mkatoliki) (2)HASSAN MWINYI(muislam)(3)MKAPA(mkatoliki) (4)JK KIKWETE(muislam) (5)MFALME(mkatoliki) na atakaekuja LAZIMA(Msisitizo) lazima awe (6).....(Muislam) mark my word.....Niweke chumvi hapa (WAZIL MKUU)....hahahaaa 😡
N. B..!! Dini nyingi haziwez kuhamasisha maandamano na kuiongelea vibaya serikali Kwa maana wengi viongozi wao (WAKUBWA WA DINI NA MATHEHEBU) ndio washauri wa Raisi na huwa tunapewa miongozo ili kuzungushwa Kwa wachungaji wote KUTOWAHAMISIWA WATU (WAUMINI) kufanya Hvyo Kwa kisingizio wakae Makanisani ili KULIOMBEA TAIFA AMANI... (Kumbuken kipindi maandamano yalipotaka kushamili mwaka ule) wachungaji,maaskofu na mashekhe waliitwa IKULU Kabla ya kufika kwa tarehe ile ya maandamano (Tarehe ile ilipofika wachungaji weng walipewa barua na siku ile lilitolewa Tangazo Kuwa MUDA ule wa maandamano watu wote (WAUMINI) wanatakiwa kuhudhuria Ibada ya jioni Saa 9..mchana ili KULIOMBEA TAIFA AMANI (hii ilikuwa mbinu ya kupunguza wingi na ukubwa wa maandamano maana weng wangekuwa KANISAN...!!!!
Hivyo usishangae kuona Dini na mathehebu yake wako kimya juu ya mambo haya ya serikali eti hawayaoni....!!!! Wanajua vizur kabisa wakuu wa Mathehebu na Dini ndio wanajua vyema na hawawez kulizungumzia na ndio maana mchungaj yeyote ambaye hayuko kweny mfumo wa serikali akiinuka na kuzungumza anazimwa na Wenzake hao hao wa Dini husika...!!
Watanzania wenzangu kila mmoja anayohaki ya kuchagua na anayohaki ya kuhoji ili kupata chimbuko na kazi husika za Dini na dhehebu lake...!!! Na kuulzia hivyo sio dhambi unatafuta japo sehem sahih yako wew na Mungu wako....!!! Sio kila uambiwacho ni sahih Ila changanya na zako ili upate original source ya unachosikia...!!!
ISAYA 56:10-11 na YEREMIA 50:6
KUMWAMINI MUNGU NA KUTANGAZA YAKE MEMA SI LELEMAMA NDUGU ZANGU ""Tangu baada ya yona ufalme umeshikiliwa na wenye nguvu"" Et kuamini Mungu Mpk uone Muujiza (Tomaso eeh) na kila Tangazo ni kupata Muujiza tu Daah kwel
""Amini unochokiamini na chenye uhakika sio upelekwe tu Na unachokiaminishwa pasipo kujua chanzo na kinalenga nini""

Cc. KWAKHERI UKORONI KARIBU UHURU
 
"Madicteta Bwana!!! ujipenyeza kila sehemu.

Miskitini, Makanisani, Jeshini na idara zote za kiserikali na kijamii na vyombo vya habari

Ila uwa sio popular kwa wananchi na dawa ya madicteta uwa ni maandamano yasiyo na kikomo." Mimi ni mkatoliki pure but toka aingie Magufuli madarakani kanisa linafanya mambo mengi ya aibu na ya kipumbavu niwaambie tu viongozi misimamo yao sio misimamo ya sisi wananchi wakatoliki tunataka haki itendeke uyu itakuwa kahongwa sio bure.
Umeona eeehh
 

Attachments

  • IMG_20191116_225309.jpg
    IMG_20191116_225309.jpg
    854 KB · Views: 1
Back
Top Bottom