The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu sana Jude Thaddaeus Ruwa'ichi OFMCap. amekanusha na kutolea ufafanuzi taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikionyesha kuwa warsha ya waamini jimboni humo itafanyika Oktoba 29, siku ambayo ni ya uchaguzi mkuu wa Tanzania, kuwa taarifa hiyo siyo ya kweli na haijatoka ofisi ya jimbo hivyo amesema ipuuzwe, bali warsha hiyo itafanyika Novemba 29, 2025.
Askofu Mkuu Ruwa'ichi amesema hayo wakati akihitimisha adhimisho la misa takatifu ya jubilei ya mapadre wa jimbo hilo, iliyofanyika katika parokia ya Bikira Maria wa Fatima msimbazi.
Askofu Mkuu Ruwa'ichi amesema hayo wakati akihitimisha adhimisho la misa takatifu ya jubilei ya mapadre wa jimbo hilo, iliyofanyika katika parokia ya Bikira Maria wa Fatima msimbazi.