The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Askofu Dkt. Fredrick Shoo amewataka wananchi kutokuwa tayari kuona yaliyofanyika katika chaguzi zilizopita yakijirudia katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu 2025.
Askofu Shoo ametoa kauli hiyo Machi 16,2025 katika ibada ya kufungua jengo jipya la Kanisa Usharika wa Kirua, Jimbo la Kilimanjaro Mashariki na kueleza kuwa kila mtu apewe haki yake ya kushiriki kwa uhuru na amani katika uchaguzi wa mwaka huu.
Pia soma Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Uhuru wa kuchagua na uhuru na haki katika kuchaguliwa, wananchi waweze kuchagua wale wanaowapenda ,wale wanao wafahamu kuwa watakuwa watumishi kweli na kuwawakilisha kweli ili haki na amani ambayo ndio Msingi wa maendeleo uweze kuwepo katika nchi yetu" Askofu Dkt.Shoo.
Aliongeza kusema kuwa, "Nitoe wito kwa washirika na wananchi wote wa Tanzania hebu tutumie nafasi yetu vizuri na tusiingie katika vurugu,mapigano na matukano,mambo yote yatendeke kwa amani na utaratibu" alisema Askofu Dkt.Shoo
Akipongeza jitihada zilizofanyika za ujenzi wa Kanisa hilo jipya Askofu Dkt. Shoo amewataka washarika wanao abudu nje ya sharika zao,waliosafarini kuelendelea kushirikiana na sharika zao katika shughuli za maendeleo katika kumtumikia Mungu aliyewapa vipawa na mali ili Mungu ajitwalie Utukufu peke yake.
"Niwaombe washarika waliopo nje ya Usharika huu na hata sharika nyingine (Diaspora) kuendelea kutumika katika kazi ya Mungu ili mema na baraka za Mungu ziwe juu yetu wakati wote"
Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa Kanisa hilo Mchungaji Kiongozi wa Usharika huo James Sambo amesema kuwa ujenzi huo umefanyika kwa miaka 22 kwa gharama ya zaidi ya Shilingi Milioni 121.
"Baba Askofu Dkt.Shoo wapo wengi walioshirikiana nasi katika ujenzi wa nyumba hii ya kuabudia wengine nikutoka katika madhehebu mengine ikiwemo Katoliki, Amani na ushirikiano ulipo baina yetu umetuwezesha kufanikisha kazi hii ya Bwana." Mch.Sambo