Askofu Shoo: Siasa ni mchezo mchafu hivyo viongozi wa dini hawapaswi kuwa sehemu ya uovu huo

Askofu Shoo: Siasa ni mchezo mchafu hivyo viongozi wa dini hawapaswi kuwa sehemu ya uovu huo

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,639
Askofu mkuu wa Kanisa la KKKT Dr Shoo amewaasa viongozi wa dini kutojifungamanisha na siasa kwani siasa ni mvhezo mchafu na viongozi wa dini hawapaswi kuwa sehemu ya uovu huo.

Askofu Shoo amefafanua kuwa hata hivyo hiyo haimaanishi viongozi wa dini wakae mbali sana na siasa bali wawe washauri wa kweli na haki.

Askofu Shoo amewataka Watanzania wawasikilize wagombea wote kwa makini na kisha waamue kwa usahihi wanayemchagua.

Naye RC Anna Mghwira wa Kilimanjaro amesema vyombo vya dola vinawatafuta wale wote waliomfanyia vurugu mgombea mmoja huko wilayani Hai na kusema anaamini askofu Shoo amelisikia tukio hilo kwa sababu huko ni eneo lake.

Chanzo: EATV habari!

Maendeleo hayana vyama!
 
Ninachoshukuru katika habari hizi za siasa dhehebu langu huwa ni nadra sana kukuta likijitokeza sana kujipambanua maana linafahamu mipaka ya dini na mambo ya serikali achilia mbali siasa maana kwa kufanya hivyo lazima utacompromise mambo na hutakuwa huru.

Kwa hiyo Dr yupo sahihi kabisa ingawa sidhani kama ataeleweka.
 
johnthebaptist,

Namheshimu sana Mama Mgwira, RC mstaarabu kuliko wote kwa mtazamo wangu. Ila kwa leo amenivunja moyo.

Hivi kweli wale vijana ni wakutafuta na aliewaleta mnamjua? RC badili kauli, maana tulitegemea uwe umeshajiuzulu kwa kudharauliwa na wasaidizi wako hadi mkoa wako ukaingia doa.
 
Ninachoshukuru ktk habari hizi za siasa dhehebu langu huwa ni nadra sana kukuta likijitokeza sana kujipambanua maana linafahamu mipaka ya dini na mambo ya serikali achilia mbali siasa maana kwa kufanya hivyo lazima utacompromise mambo na hutakuwa huru

Kwa hiyo Dr yupo sahihi kabisa ingawa sidhani kama ataeleweka
Wewe ni KKKT kumbe!
 
Namheshimu sana Mama Mgwira, RC mstaarabu kuliko wote kwa mtazamo wangu.
Ila kwa leo amenivunja moyo.
Hivi kweli wale vijana ninwakutafuta na alie waleta mna mjua.?? Rc badili kauli, maana tulitegemea uwe umesha jiuzulu kw a kudharauliwa na wasaidizi wako hadi mkoa wako ukaingia doa..
Tumbo mkuu.
 
Watanzania Wengi Wetu hatujitambui, Kunyimwa Elimu stahiki kumetugharimu saana, Pili Kuna Changamoto saana na Matatizo ya Njaa na Tatu Uoga kwavile tumezoea Maisha ya Ujanja ujanja ndiyo gharama ya yote haya. Akili huwa zinakaa pembeni!
 
Nasubiri tamko la viongozi wangu wa TEC..naamini ipo misingi na misimamo yao wanayoiamini kuhusu kutoridhika na uongozi wa Jiwe
 
Ninachoshukuru katika habari hizi za siasa dhehebu langu huwa ni nadra sana kukuta likijitokeza sana kujipambanua maana linafahamu mipaka ya dini na mambo ya serikali achilia mbali siasa maana kwa kufanya hivyo lazima utacompromise mambo na hutakuwa huru.

Kwa hiyo Dr yupo sahihi kabisa ingawa sidhani kama ataeleweka.
Shoo ni mnafiki! Anajulikana yeye ni chadema!

Kama ana misimamo hiyo kwanini asimkemee Bagonza yule wa Karagwe?
 
johnthebaptist,

Namheshimu sana Mama Mgwira, RC mstaarabu kuliko wote kwa mtazamo wangu. Ila kwa leo amenivunja moyo.

Hivi kweli wale vijana ni wakutafuta na aliewaleta mnamjua? RC badili kauli, maana tulitegemea uwe umeshajiuzulu kwa kudharauliwa na wasaidizi wako hadi mkoa wako ukaingia doa.
Mmojawapo huyu hapa
JamiiForums-2079067986.jpg
 
1. Mh Askofu Sho, kuna watu kama majini sheikh, sasa na huyo ni kiongozi wa dini? Hao si ni wezi tu?
2. Waliobaki wote ni Wajasilia dini, wasikuhangaishe!
 
1. Mh Askofu Sho, kuna watu kama majini sheikh, sasa na huyo ni kiongozi wa dini? Hao si ni wezi tu?
2. Waliobaki wote ni Wajasilia dini, wasikuhangaishe!
Kumbe askofu Shoo ni mwenyeji wa Hai!
 
Back
Top Bottom