Aslay na Nandy kupelekwa Mahakamani

Hivi ile kesi ya Dayamondi ha Saida Kalori iliishaje??


Tusubiri na hii
 
Wasanii wanalilia sana hati miliki lakini wao ndio wezi wa kwanza wa kazi za wenzao
 
Laki 8 tu me nawalipia hacheni roho mbaya
Umehelwa post hao wakina Asley wamewapa icho kikundi laki 8 wakati ukiiangalia kwa makadirio Asley na Nandi washaiingiza zaidi ya million 50
 
Kesi yao hao viongozi wa kikundi (Culture Music Club)itakua tu na mashiko kama kikundi kilikua kina haki miliki juu ya wimbo huu.Hao waimbaji waliochukua hiyo 800,000 itawatokea puani na Aslay na Nandi watapaswa kuwalipa hao wanakikundi.Ishu ya wimbo chambua kama karanga wa Saida Karoli mwenye haki miliki ni Mzee Mutta na sio Saida Karoli.
Sema hao wazee wangekua wajanja wangewapa bure tu huo wimbo ila royalties zote zinakua za wanakikundi ila Aslay na Nandy watanufaika na show tu za wimbo husika,mauzo ya wimbo na matangazo yanakua ni mali ya kikundi.Mfano wimbo wa I will Always Love you aliouimba Whitney Houston ulikua wa Dolly Parton.Whitney alimuomba Dolly amuuzie huo wimbo but Dolly Parton alikataa kata kata na alimpa wimbo ule bure ila royalties zote zikawa ni za Dolly Parton.Whitney alivyokufa wimbo huu uliuza sana na mapato yote yalienda kwa Dolly na sio kwa Whitney ambaye aliufanya wimbo huu uwe maarufu sana,kumbuka Whitney amekufa akiwa kafilisika kama ungekua ni wimbo wake basi angeiacha familia yake ikiwa pazuri kimapato.
Wazee hawa wakae chini wafikie muafaka ila ikishindikana basi waende mahakaman na wang'anganie wimbo uwe mali yao au wagawane nusu kwa nusu kwa kila kitakachofanyika kuhusu wimbo huo wasikubali kupewa hela hata ikiwa milioni kumi kwan mpaka sasa huo wimbo umewapa Nandy na Aslay mkataba mnono wa brand ammbassodor achilia mbali show yao ya Valentine Day!
 
Hayo yameibuka baada ya mmiliki wa wimbo huo, Kikundi cha Tarab Asilia visiwani Zanzibar (Culture Music Club) kudai pesa zilizotolewa jumla ya Tsh. 800,000 kama fidia za kutumia kazi hiyo hawazitambui hivyo wanajipanga kuwapeleka mbele ya Mahakama
Nashawishika kuwa Devils Advocate - Itakuaje kama hio laki nane ndio ilikua makubaliano yao na hao waliopokea? Biashara ni issue nzito sana, pale unapomuuzia mtu gari kwa milioni 5 halafu yeye akafanikiwa kuliuza kwa milioni nane!! ..
Just thinking out aloud...
 
Nadhanii waliwapaa mpaka pesa..Na jamaa wakakubalii maana kiukweli nyimbo zao zishapitwa na wakati na hata shoo kupitia hizo nyimbo hawampati mtu.. Semaa tamaa imewajaa baada ya kuona imekuwa Hit kalii sana
Kasome tena vizuri utaelewa, tofautisha kati ya msanii na uongozi wa kundi.
Ishu ya kusema nyimbo ilikuwa haina umaarufu sio hoja ya msingi
 
Njaa kitu kibaya sana sana..wanavyoona inahit basi wanaingia tamaa.
Wakina Aslay na Nandy walienda kuwaona wahusija kuomba ruhusa kabla ya kuirudia hii track.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…