Kesi yao hao viongozi wa kikundi (Culture Music Club)itakua tu na mashiko kama kikundi kilikua kina haki miliki juu ya wimbo huu.Hao waimbaji waliochukua hiyo 800,000 itawatokea puani na Aslay na Nandi watapaswa kuwalipa hao wanakikundi.Ishu ya wimbo chambua kama karanga wa Saida Karoli mwenye haki miliki ni Mzee Mutta na sio Saida Karoli.
Sema hao wazee wangekua wajanja wangewapa bure tu huo wimbo ila royalties zote zinakua za wanakikundi ila Aslay na Nandy watanufaika na show tu za wimbo husika,mauzo ya wimbo na matangazo yanakua ni mali ya kikundi.Mfano wimbo wa I will Always Love you aliouimba Whitney Houston ulikua wa Dolly Parton.Whitney alimuomba Dolly amuuzie huo wimbo but Dolly Parton alikataa kata kata na alimpa wimbo ule bure ila royalties zote zikawa ni za Dolly Parton.Whitney alivyokufa wimbo huu uliuza sana na mapato yote yalienda kwa Dolly na sio kwa Whitney ambaye aliufanya wimbo huu uwe maarufu sana,kumbuka Whitney amekufa akiwa kafilisika kama ungekua ni wimbo wake basi angeiacha familia yake ikiwa pazuri kimapato.
Wazee hawa wakae chini wafikie muafaka ila ikishindikana basi waende mahakaman na wang'anganie wimbo uwe mali yao au wagawane nusu kwa nusu kwa kila kitakachofanyika kuhusu wimbo huo wasikubali kupewa hela hata ikiwa milioni kumi kwan mpaka sasa huo wimbo umewapa Nandy na Aslay mkataba mnono wa brand ammbassodor achilia mbali show yao ya Valentine Day!