Atakayetoa taarifa sahihi ya kupatikana Mzee Michael Juma, zawadi Tsh 500,000/ au zaidi

Atakayetoa taarifa sahihi ya kupatikana Mzee Michael Juma, zawadi Tsh 500,000/ au zaidi

Kwani mama Anna na Anna wanasemaJe ?!. Na wako wapi ?
Mama Ana na Ana(mwanao wa kwanza)pia hatuna taarifa juu yao Ndo maana swala linakuja gumu maana aliondoka aliondoka nao kurudi masasi.Na toka apo hatujui taarifa zao kabisa Ndo maana pia nimemtaja Ana Kama yupo umu Ana watoto wake wanawezakuwa umu wakasoma. Na kupata A,B,C
 
🤣🤣ko sababu wajukuu wanamtaka babu ahaha daa yaani kama tuu baba yao hamjui baba yake ila watoto wanataka babu hao watoto inaonekana wamedekezwa saaan
Wewe unasema tena, hujui maumivu ya kuwa na historia iliyokatika.... HILO SWALI LA WATOTO LINAMUUMIZA SANA BABA YAO NDIYO MAANA YUPO RADHI KUTOA HELA ILI KUUNGANISHA NASABA....

KAMA SIYO MUISLAM ni sawa kwake kufanya hivyo maana kwa WAISLAM WATOTO WALIOZALIWA OUT OF WEDLOCK nsaba yao inafuata kwa mama yao....
 
Nendeni hapo Gerezani mchukue Check no ya Mshahara wake mwende Pensheni mkaangalie kama bado anapokea Kiinuwa Mgongo chake! Mtapata Acc na Tawi la Benk anapochukuwa pesa za penshen Simple
Kwa miaka inyaozungumziwa sidhani kama watumishi walikuwa wanalipwa kwa cheque number!
 
brother punguza makasiriko niliposema aweke dau nilimaanisha niache baadhi ya shughuli zangu ili nimsaidie yeye kwani kazi yake inaweza chukua mpaka siku 3, na hapo kote ninapotafuta hizo taarifa lazma watu niwapoze jpo najuana nao wengi tu sababu ukienda kisheria kuna mlolongo mrefu.

pia nikampa hatua za kufanya endapo hyo hela hana au ana mda wa kufatilia na kumaambia kabisa kama atashindwa ani dm ili nijue amefika wapi na nimuunge na nani free bila charge.

hapo kosa langu liko wapi?
Huna baya !! Binafsi nimekuelewa sana ushauri ulompa ! Spot on.
 
Kosa lako ni kuanza kutoka maelezo kwake badala ya kupanga namna utakavyomsaidia. Mimi nilitarajia ungemwambia njoo tukutane au tuwasiliane kwa mipango zaidi. Hilo la kuweka dau hata mimi nimeelwa kwa sababu shughuli kama hiyo ni lazima utaacha kazi zako na itabidi uzunguke sana. Kama unaweza ni vizuri mzungumze kwa kina ili mpange na kujua kukadiria gharama hasa ikizingatiwa kuwa zinaweza kuwa kubwa kuliko unavyodhani. Au basi uongozane naye angalau kwa hatua za mwanzoni.
Ushakuwa ubabaishaji huu,yeye kuna njia aliiwaza ambayo nadhani kwa sasa haifanyi kazi

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Hapa kama una mganga mkali dk tu ana mwona kwenye kioo anakuambia alipo. Wale ambao huwa mnajifanya wataalam haya leteni utaalamu wenu hapa. Siyo mnakaa kuwafunga kamba tu vijana humu kuwa mna huo utaalamu na kuwadanganya danganya.
 
Mtakumbuka mwaka 2018,April niliweka hapa jukwaani mada isemayo Anatafutwa Mzee Michael JUma Mkazi wa Mtwara na Masasi.

Kiufupi kwa wale ambao hawakupitia uzi huu mda ule Ni kuwa huyu Michael Juma alikuwa Ni Askari magereza katika gereza la musoma miaka ya 80S.Alikwa na Mke anaitwa Mama Ana(bahati mbaya hatukupata jina la huyu mama maana huyu ANA Ndo mtoto wao wa kwanza kuzaliwa)Huyu mzee alikuwa Ni mmakonde wa Mtwara na alikuwa anasema wazazi wake baade waliamia mtwara mjini kutokea Masasi.Mke wake huyu alikuwa Ni mnyiramba kwao singida na inavyoonekana aliamia musoma toka gereza la singida na huyu Mama ANA.Lakini pia kwa mjibu wa mtoa taarifa wetu Ni kuwa kwenye miaka ya 1989 au 1990S aliacha kazi na kurudi kwao mtwara na kujishugulisha na kazi ya fundi seremala maana yeye kazini kwake alikuwa kwenye section hiyo.Bahati mbaya pia hatukuweza kupata jina lake la ukoo au Kijiji alipokuwa akitokea either Cha masasi au mtwara.

KWA NINI ATAFUTWE?Anatafutwa ili kijana wake apate kumjua na pia Kama Yuko hai amuhudumie maana kwa Miaka hiyo huyu ndugu yangu hakuwahi kumwona na hamjui mpaka sasa Ni mtu mzima mwenye maisha yake binafsi na kinachomtesa Ni watoto wake wanasumbua juu ya babu yao.

Tumeshafanya jitihada kubwa kumsaka bila mafanikio Mara ya mwisho tukipata taarifa toka kwa mtu alikuwa anafanya nae kazi mwaka huu apo tabora alitueleza alikaa mda baadae yeye akahamishia tanga kumbe hapakuwa Tena na mawasiliano na kipindi hicho mawasiliano yalikuwa Ni shida adi muonanapo Ana kwa ana tofauti na sasa.Kwa sasa huyu aliyepata kufanya nae kazi Ni mstaafu anachokumbuka tu Ni jina.Pia tulifika alipokuwa anafanyia kazi bila mafanikio kutokana na mda kwenda na mfumo wa utunzaji kumbukumbu wa mda huo.

Tunaomba kama Kuna mtu ana A,B,C juu ya andiko hili au ata Ana,ndugu wa karibu ,au watoto wa Ana Kama Mungu alimjalia na watu wote wenye mapenzi mema watujulishe na Zawadi itatoka siyo ya kusubilia Ni papo kwa papo cha msingi utupe uhakika wa taarifa sahihi. Najua JF Kila siku wanaongezeka members wapya na hii inatufanya tuje apa Mara kwa Mara.

Naomba tu matapeli wakae pembeni maana Kuna mda nililipoti apa juu ya mmoja wao akitaka kutuchezea(nafsi hiyo haipo Tena)tunafanya analysis Hadi tujiridhishe Ndo unapewa pesa yako bila shida.Asanteni,Tutafute kupitia 0789443404/0762364740
Anyway. Lazima sana awe yeye mwenyewe asilimia 100? Je kama kuna mzee wanafanana majina anaweza pia kufaa?
 
[emoji1787][emoji1787]ko sababu wajukuu wanamtaka babu ahaha daa yaani kama tuu baba yao hamjui baba yake ila watoto wanataka babu hao watoto inaonekana wamedekezwa saaan
Kina Junior wanamtaka Babu... Ila hawa watoto hawajui Lolote kuhusu baba yao hata Ndugu wa upande wa babaaa..??? Mama yao alikuwa kauzuuu...
 
Naelewa sana unachikitaka ni kheri kubwa pia hata kwa watoto kujua asili yao. Nakutakia baraka umpate mzee. .
 
Back
Top Bottom