ATCL Kwenda India ni ukatili kwa Watanzania

sinzahome

New Member
Joined
Apr 25, 2019
Posts
2
Reaction score
5
Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kutumia ndege yake ya Boeing 787 Dreamliner inataraji kwenda nchini India kuwachukua watanzania 255 waliokuwa wagonjwa wakipatiwa matibabu nchini humo. Suala hili ukiliangalia juu juu unaweza kusema ni upendo wa Serikali ya Tanzania kwa wananchi wake kwa kuwachukua watanzania hao baada ya kunasa huko kwa sakata la LOCKDOWN la Ugonjwa wa CORONA ulioathiri Dunia Nzima.

Lakini laghasha, Watanzania hawa wanaoenda kuchukuliwa wameingia gharama kubwa saaaaaana za kulipia nauli ya ndege na kuwa mara 2 au 3 zaidi ya ile waliotumia awali kwenda India kutibiwa, kiasi ambacho wengi wao walioko huko wenye kipato kidogo kushindwa kulipia nauli hiyo ya kurudi nyumbani. Kama kweli Serikali inania ya dhati ya kuwasaidia wananchi wake kurudi nyumbani wafanye “COST SHARING” kwa hao wagonjwa ili kuwasaidia kurejea nyumbani. Ikumbukwe kwamba hao wagonjwa walikwenda India kutibiwa huko kwa gharama zao wenyewe na walishaingia gharama kubwa za kutibiwa wakiwa huko sasa sidhani kuwasaidia kurudi nyumbani napo waingie gharama nyingine kubwa zaidi.

Hili kwa maoni yangu naona sio kuwasaidia wananchi bali ATCL kuendelea kuingiza mapato licha ya Janga la CORONA kuendelea kuwepo. Hii inaitwa kufa kufaana kuwepo kwa janga la CORONA imekuwa ni manufaa kwa ATCL kuendelea kuingiza mapato na sio kuwasaidia wananchi wake. wakati huo ikumbukwe kuwa ndege hizi zimenunuliwa kwa Kodi za wananchi ambao ni watanzania wenyewe kati yao ndio hao walionasa huko India.

Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi alisema “Sisi ni wafanya biashara, ndege yetu gharama yake ni hizi kwahiyo tunahitaji utupe kiasi hiki, hata wakiwa watu wawili wakiwa na uwezo wa kuichukua ndege tunawapa” Kwa kusema hivi inaonesha kuwa ATCL wako kimaslahi zaidi na sio kuwasaidia watanzania.

ATCL na Serikali kwa ujumla kwa hili hata siwasifu eti mnawajali au kuwasaidia watanzania bali nawapongeza kwa kuendele kuwaumiza wananchi hali ya kuwa ndege hizo ni Kodi zao.
ndege1.jpg
 
Sasa wewe unalalamika vipi wakati wao ndiyo wameomba msaada wa ndege kwa gharama hiyo? Pia wao ndiyo waliamua kwenda huko wakati huduma zote za afya zinapatikana hapa TZ. Kumbuka pia wengine walipeleka watoto wao shule ila wakanasa huko. Hivyo huo ni msaada tosha kabisa la sivyo waendelee kukaa huko mpaka ndege sitakapoanza safari duniani kote. Wapo wamarekani wamekwama hapa TZ mpaka sasa hivi wakisubiri ndege zianze safari.
 
Hao wanaenda kuchukuliwa hawajalalamika ila we kiherehere unalalamika
Upo sahihi mdau.....Watu wanasahau shirika la ndege linatakiwa lifanye kitu kwa kuangalia faida pasipo kuumiza mtu wala kujiumiza lenyewe! Lazima wakumbuke inaenda ikiwa tupu kuwafuta huko tofauti na ile ambayo inakwenda kibiashara ambapo inakwenda na abiria na inarudi na abiria

Njia pekee ni Watanzania waliopo kule ni kuilipa ATCL kwa kuwa wao waliomba ama SERIKALI kuwalipia wananchi wake na si ATCL kubeba hizo gharama hata kama ni shirika la ndege la serikali
 
Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kutumia ndege yake ya Boeing 787 Dreamliner inataraji kwenda nchini India kuwachukua watanzania 255 waliokuwa wagonjwa wakipatiwa matibabu nchini humo. Suala hili ukiliangalia juu juu unaweza kusema ni upendo wa Serikali ya Tanzania kwa wananchi wake kwa kuwachukua watanzania hao baada ya kunasa huko kwa sakata la LOCKDOWN la Ugonjwa wa CORONA ulioathiri Dunia Nzima.

Lakini laghasha, Watanzania hawa wanaoenda kuchukuliwa wameingia gharama kubwa saaaaaana za kulipia nauli ya ndege na kuwa mara 2 au 3 zaidi ya ile waliotumia awali kwenda India kutibiwa, kiasi ambacho wengi wao walioko huko wenye kipato kidogo kushindwa kulipia nauli hiyo ya kurudi nyumbani. Kama kweli Serikali inania ya dhati ya kuwasaidia wananchi wake kurudi nyumbani wafanye “COST SHARING” kwa hao wagonjwa ili kuwasaidia kurejea nyumbani. Ikumbukwe kwamba hao wagonjwa walikwenda India kutibiwa huko kwa gharama zao wenyewe na walishaingia gharama kubwa za kutibiwa wakiwa huko sasa sidhani kuwasaidia kurudi nyumbani napo waingie gharama nyingine kubwa zaidi.

Hili kwa maoni yangu naona sio kuwasaidia wananchi bali ATCL kuendelea kuingiza mapato licha ya Janga la CORONA kuendelea kuwepo. Hii inaitwa kufa kufaana kuwepo kwa janga la CORONA imekuwa ni manufaa kwa ATCL kuendelea kuingiza mapato na sio kuwasaidia wananchi wake. wakati huo ikumbukwe kuwa ndege hizi zimenunuliwa kwa Kodi za wananchi ambao ni watanzania wenyewe kati yao ndio hao walionasa huko India.

Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi alisema “Sisi ni wafanya biashara, ndege yetu gharama yake ni hizi kwahiyo tunahitaji utupe kiasi hiki, hata wakiwa watu wawili wakiwa na uwezo wa kuichukua ndege tunawapa” Kwa kusema hivi inaonesha kuwa ATCL wako kimaslahi zaidi na sio kuwasaidia watanzania.

ATCL na Serikali kwa ujumla kwa hili hata siwasifu eti mnawajali au kuwasaidia watanzania bali nawapongeza kwa kuendele kuwaumiza wananchi hali ya kuwa ndege hizo ni Kodi zao.
Ungeweka ushahidi wa malipo hayo ingependeza sana,vinginevyo ni takataka tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona tumeingia gharama kwenye vingi visivyo tija mfano kununua wapinzani,marudio ya chaguzi,nk
 
Back
Top Bottom