mfianchi
Platinum Member
- Jul 1, 2009
- 11,904
- 8,371
Mkuu hapo umenena hawa jamaa walewa sifa kwa kuwa hawana mshindani na hapo ndio tunakumbuka air daladala yetu Fastjet ambayo ilituwezesha wazazi wetu vikongwe kuwapandisha ndege kwenda Muhimbili kutibiwa hadi mbeki 3 pia tuliwapandisha FJ kwa nauli ya laki moja sasa hawa wanataka kupata faida asilimia 100, naamini bila ya mwendazake hili shirika litakuwa ICU kama hawajabadili hizo nauli,weka nauli nafuu sababu hii ni budget airline ujaze hata mbuzi kwenye cabin, ndio maana akina Lusinde Kibajaji,Musukuma wanawadharau hawa wasomi wetu,wanashindwa kufikiri na kuangalia mazingira.Ni suala la kitalaamu kiuchumi ambalo lipo katika maisha ya kila siku. Kwamba bei ikiwa ndogo uwezo wa kulipia huduma huwa mkubwa na kuongeza soko. Kwa hiyo ili kuruhusu soko kubwa lipanuke na kuweza kupata wateja wengi ni vyema Atcl wakashusha bei kama ilivyokuwa kwa fastjet. Mfano kama ikiwezekana mtu kusafiri kwa laki na nusu toka Mwanza mpaka Dar Atcl wanaweza kuwa na trip zaidi ya nne kwa siku Dar to Mwanza.