ATCL vipi flights za Dar - Chato zitaendelea baada ya kifo cha Dkt. Magufuli?

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Nauliza tu vipi ATCL zile trips za Dar -Chato, Chato-Dar zitaendelea kama mlivyokuwa mkitangaza au ndio basi tena?
Kama zitaendelea good.

Kama hazitaendelea basi unafiki uliwatawala na hakika mtafilisika soon maana hamna vision. You are like wind, you have no specific direction or goals.
 
Mimi nawaomba atcl waendelee kutoza nauli viongozi na familia zao maana ile atcl ya zamani ndege zilikuwa zinajaa lakini waliolipa nauli ni wawili tu, nakumbuka mwakyembe alienda airport akakagua abiria walikuwa wanasubiri kupanda ndege ya atcl akakuta wote hawana tiketi akawaambia atakaeingia kwenye ndege ni yule atakaeenda kulipia tu, walirudi wote shenzi zao, Marehemu Magu kipindi yupo rais alikuwa analipana nauli.
 
"Kama hazitaendelea basi unafiki uliwatawala na hakika mtafilisika soon maana hamna vision. You are like wind, you have no specific direction or goals''. MSG DELIVERY
 

Hili swali lipo trick sana...
Joyce enheee naomba bia nyengine afu niitie na mtu wa jikoni
 
Safari za ndege za Chato- Dar, Chato - Mwz zitaendelea Sana labda dhahabu ya Geita iishe, kwa wafanyabiashara wa dhahabu ni risk Sana kusafirisha mzigo kutoka Geita kwenda Mwanza! Ila kutoka Geita kuja Chato ambapo ni karibu Sana na usalama ni wa uhakika!
Mleta mada Mkoa wa Geita umebarikiwa Sana kwa vivutio vya utalii, Burigi- Chato, Kisiwa cha Rubondo, mazalio makuu ya samaki wa aina zote ziwa victoria, nk
Kile kimtokacho kinywani(mawazoni) mwanadamu ndio humtia najisi na sio alacho! Mleta mada mawazo yako yamejaa najisi!
 
So, vision ya kujenga ule uwanja wa chato Airport ilikuja kwasababu ya Dhahabu ya GGM?
Kwanini haukujengwa Geita mjini palipo na mgodi mkubwa?
Nimefanya kazi GGM na Bulyanhulu, jiografia ya Ile migodi mikubwa haina undugu na Chato Airport
 
Duuuuuuhhh hiyo nilikuwa sijaipata.
Kweli umri wangu mdogo
 
Wanaendelea. ATCL wamekuwa smart. Trip ni Mwanza via Chato.

So hata kama kuna travellers wawili, poa tu, afterall, trip mwisho wa siku inapita Mwanza then Dar
 
Wanaendelea. ATCL wamekuwa smart. Trip ni Mwanza via Chato.

So hata kama kuna travellers wawili, poa tu, afterall, trip mwisho wa siku inapita Mwabza then Dar
Gharama za kutua ndege na kuruka chato kuelekea mwanza unazifahamu?? Kama ni ndio je huko ndo kuwa smart??

Ujue ndege usifikiri ni kama basi linavyosimama msamvu na kuendelea ndugu yangu
 
Naomba nikuulize. Umbali wa Geita mjini mpaka Chato Airport na Geita Mjini mpaka mwanza airport ni km ngapi mtawalia?
 
Mbona mapema. Si msuburi muone mambo yanaenda aje? Na sio mambo ya atcl tu, ni serikali nzima na mwenendo wa nchi baada ya Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…