Kampuni ya Ndege ya Air Tanzania (ATCL) inapenda kuwajulisha wateja wake na umma kwa ujumla kuwa safari za ndege
TC422 na TC423 kati ya
Dar es Salaam na Moscow zimesitishwa kwa muda kuanzia
4 Septemba 2026.
Uamuzi huo umefuatia tathmini ya kawaida ya hatari zinazohusiana na mazingira ya uendeshaji wa safari hiyo. ATCL hufanya tathmini hizo mara kwa mara katika mtandao wake mzima wa safari, na pale ambapo matokeo ya tathmini yanaonyesha umuhimu wa kusitisha safari kwa muda, hatua hiyo huchukuliwa.
Usalama daima hupewa kipaumbele kuliko masuala ya kibiashara.
Abiria wenye tiketi za safari zilizoathiriwa watapewa
marejesho kamili ya fedha au watapewa nafasi ya
kubadilisha tarehe ya safari au kutumia njia nyingine ya usafiri bila gharama ya ziada. Tafadhali wasiliana nasi kupitia
[email protected] au
+255748773900, au wasiliana na wakala wako wa usafiri.
Tunaendelea kufuatilia hali hiyo kwa kushirikiana na mamlaka husika, na tutatangaza kuanza tena kwa huduma hizo mara tu tathmini itakapoonyesha kuwa safari zinaweza kuendelea.
Soma Pia: ATCL Yaanza Safari za Moja kwa Moja Dar-Moscow 2026
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliosababishwa na tunawashukuru wateja wetu kwa
imani na kuendelea kutuunga mkono.
View attachment 3662863