ATCL yatolea ufafanuzi kuhusu simtofahamu ya msanii Diamond Platnumz

Hivi hili suala ATCL wangeamua kukaa kimya wangepata tabu gani? Kuzingua wamezingua ila naona kama wamelipa uzito saaaana kupitiliza katika harakati za kujisafisha. . . .hadi tuite press aiseee. Basi sawa
 
Nimekutana nayo hii mwananchi eti! Mpaka nimeshangaaa
 
  • lemutuz_superbrand
    LIVE HARD TALK: Naomba kutoa mchango wangu kuhusu you guys Shirika la Ndege Air Tanzania ...YOU ARE HORRIBLE and SUPER NIGHTMARE ...mambo mnayoyafanya ni Aibu tupu I mean Jumamosi nimeruka na ndege yenu Drimlaina to Mwanza na nimerudi nayo jana Usiku ...Rais Magufuli kwa nia njema kabisa kainunulia Taifa hii ndege ili isaidie kumaliza tatizo la Usafiri ...Ndege ni Kubwa nzuri na Safi lakini tatizo nyingi handlers aidha hamna uzoefu au ni WAZEMBE WA AJABU SANA ....Marubani wapo vizuri na kukata tiketi hapa Dar hakuna tatizo ....Tatizo linaanzia Uwanja wa Ndege Dar kwenye kusafiri hakuna mpangilio mizuri yaani kuanzia mistari ya ku Check in ni kama unapanda Dala dala yaani kweli mnashindwa hata kuwapanga Abiria kistaarabu kama mashirika mengine? ...hapo mpo jirani na Emirates hamuwaoni wao wanayoyafanya? ....kuanzia Check in ni usumbufu mtupu Joto watoto wanalia hakuna Air Conditons Abiria 262 mnagombea ku Check in bila utaratibu maalum ...sasa ukifika juu ndio kabisa Tangazo linasema sasa ndege ipo tayari kuondoka boom abiria wote 262 mnaanza kugombea kuingia kupitia kamlango kadogo sana Kina Mama wenye watoto, Vilema, Wazee, kama daladala ....ok mashirika yote ya ndege Duniani watu wa Business na First Class wanaingia kwa mpango tofauti lakini sio hii ndege yaani jana na juzi niliona Wazungu Watalii wanavyolalamika ...jana tulipokuwa tunatoka Mwanza tukaambiwa abiria wote ni lazima tupitie Mlango mmoja wa Nyuma Horrible halafu ndege ndani Chafu tayari hata usafi unawapa taabu ....na hata mkiwauliza Crew wenu jana niliwapa maneno mazito sana kuhusu huu uzembe wa ajabu sana ...Rais alisema anataka Watalii watumie ndege zetu naomba niwaambie kwa hizo tabia zenu Watalii watakodi magari hata mimi nikiwa Mtalii siwezi nikarudia kupitia bughudha kama zile za Jana na Juzi ....Juhudi zote za Mheshimiwa Rais mnazivuruga kwa Uzembe tu hakuna lolote ni INCOMPETENCE na UZEMBE ....ni Wakati muafaka Rais akawaondoa wote au mrudi kwenye Training ...ok guys NIMEANDIKA NILIYOYAONA KWA MACHO YANGU so ambayo sijayaandika SIKUYAONA! ...MUNGU AIBARIKI TANZANIA! AMEN! - @lemutuz_superbrand
Sitoshangaa kama wiki itaisha bila Mkurugenzi wa ATCL kutenguliwa maana uenda huu mchezo anaujua! Haiwezekani watu wanalalamika namna hii dizaini kama wakisubiri nani aanze tu! alafu hapohapo Mkurugenzi amemjibu Mond kuwa kachelewa wakati mwenyewe kaeleza kuwa walikutwa siti zimeuzwa na zimebaki 2
 

Le Mutuz analalamika kupitishwa kwenye kamlango kadogo.

Atakuwa alihangaika sana kupita.
 
HapaKazi Tu!
Timue wazembe! Lakini inline to labour law! Wengine watajifunza. Customer care ni sawa na Meza na Sahani plus msosi wenyewe.
 
Huyo dogo anatoa wapi uthubutu wa kulichafua shirika letu la ndege kwa uzembe wake mwenyewe wa kuchelewa mda?!

Kuna nani nyuma yake hadi anakuwa na UTHUBUTU WA KIWANGO KILE KULITUHUMU /KULICHAFUA SHIRIKA ILHALI POPOTE DUNIANI MTU ANAYE CHELEWA NDEGE huwa haimusubiri?!

Huyo dogo/jipu lileeni tu.Ipo siku kwa PAPARA zale na MAJIVUNO yake atakuja kuichafua zaidi nchi kwa matamanio ya KIJINGA!

Kwa kitendo kile SHIRIKA LA NDEGE WAMPELEKE MAHAKAMANI HARAKA KWA KULICHAFUA SHIRIKA KWA UZEMBE WAKE!
 
WAFANYAKAZI WA ATCL NA TEAM KIBA TULIZENI VISHUNDU KWANZA SERIKALI IPO KWENYE UCHUNGUZI

NI LAZIMA MSHIKISHWE ADABU, MMESHAZOEA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA SAFARI HII MTAISOMA NAMBA
 
WAFANYAKAZI WA ATCL NA TEAM KIBA TULIZENI VISHUNDU KWANZA SERIKALI IPO KWENYE UCHUNGUZI

NI LAZIMA MSHIKISHWE ADABU, MMESHAZOEA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA SAFARI HII MTAISOMA NAMBA
Ficha ujinga wako na nimekustahi kwa mda!
 
Acha ujinga, huenda hata ndege hujawahi kupanda. Tayari unamchukulia kama mwanamuziku maarufu Africa, ndio unapokosea. Mchukulie kama abiria tu, ndio analalamika huduma alizofanyiwa sio stahiki. Sasa wewe unasema analichafua shirika la ndege, kwani lini likikukwa safi?
 
Na wewe unakera na mpira kwenye thread za watu. Fungua thread yako special ndo uweke haya mambo maana kama ni issue za mpira trust me watu hapa tupo vizuri na latest news, huhitaji kutukumbushia.
 
Hivi hili suala ATCL wangeamua kukaa kimya wangepata tabu gani? Kuzingua wamezingua ila naona kama wamelipa uzito saaaana kupitiliza katika harakati za kujisafisha. . . .hadi tuite press aiseee. Basi sawa
nguvu ya mtandao vs brand boss!!
 
Mbona huyo wa Mwanza 2014 alihamishiwa Arusha airport.
 
Yaa kumbuka huyu ni msanii nje ya kwamba ni mwananchi kama wengne but fikiria kama alikuwa anaenda kuperforrm mkoa mmja impact yake ingekuwaje nk
Msanii wenu mshamba tu kwani hajui muda wa kufika airport. Local flight unatakiwa saa moja kabla ya kuruka. International flights ni masaa 2 kabla. Yeye anadhani muda huu umewekwa na wasanii wen zake. Na safari zote za nje hajaelimika tu. Kweli mtu wa Mbagala huyu.
 
Kuna jukwaa la sports, walioliweka sio kwamba hawakuwa na akli timamu...unatia waswas uwezo wako wa akli kwa kuleta taarifa sahihi kwnye jukwaa lisilo sahihi na thread isiyo sahihi.....
 
Unamuombea uhamisho mama wa watu jamani
 
1. Kama kweli ni abiria mwenyewe ndiye aliyechelewa kwa kuomba kutumia ticket hiyo na kusafiri kesho yake kwa utaratibu wa ndege si kuna hela zaidi anatakiwa kuongeza? Kama hakuongeza ina maana hapo ni kampuni ya ndege imekiri kosa? Kama ameongeza ni abiria kukiri kosa?

2. CCTV cameras zilizopo hapo uwanjani haziwezi kutumika kuthibitisha kuwahi au kuchelewa kwa hao abiria ili hatua stahiki zichukuliwe kwa watendaji wabovu au abiria kama itathibitika kwamba ni wao walichelewa na wakaharibu kwa makusudi taswira ya shirika kwa kutoa taarifa ya kupotosha umma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…