ATCL YAZINDUA SAFARI ZA MWANZA - DODOMA, ABIRIA 1300 KWA SIKU
Shirika la Ndege Tanzania(ATCL), limezindua safari zake za utoaji huduma kati ya Mwanza -Dodoma ikiwa ni kurahisisha safari kwa watumiaji kwa njia ya anga.
Safari hizo zilianza Juni 5,2026, ikitajwa kusaidia wafanyabiashara na wananchi kusafiri kwa urahisi,haraka na salama kati ya miji hiyo miwili.
Meneja wa ATCL kituo cha Mwanza, Paskas Samwel amesema,hadi kufikia Juni,wameshuhudia ongezeko la safari tatu mpya kupitia mkoa huo ikiwemo ya kupitia Geita, Kilimanjaro na hiyo ya Dodoma.
Amesema,ongezeko la safari hizo mpya linafanya jumla ya miruko katika ukanda huo kufikia 160 kwa mwezi,kukiwa na wastani wa ndege tano mpaka saba kwa siku.Hivyo kuongezeka kwa miruko hapa Mwanza ni uthibitisho wa ukuaji wa uchumi wa Kanda ya Ziwa.
Amesema kuanza kituo cha Mwanza kinahudumia abiria 1,000 hadi 1,300 kwa siku na kwamba ongezeko la safari ya Mwanza-Dodoma ambayo inafanyika kwa siku mbili Ijumaa na Jumapili imeiwezesha ATCL kufikia miruko zaidi ya 32 kwa siku katika vituo vyake mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Akizindua safari hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Amir Mkalipa,amesema Mkoa wa Mwanza ni wa pili katika kuchangia pato la taifa na idadi ya watu huku ukiwa ni kitovu cha mikoa ya Kanda ya Ziwa na unafikika kihurahisi hivyo usafiri wa anga ni muhimu.
Mkalipa amesema,safari hiyo itarahisisha usafiri na kuchochea uchumi kwani awali watu walikuwa wakitaka kusafiri kutoka Dodoma kuja Mwanza,iliwalazimu kuunganisha mpaka jijini Dar-es-Salaam.Huku akisisitiza kuwa safari hizi zikifanya vizuri wanaweza kushauri kuongezwa nyingine.
Mbunge wa Bariadi Vijijini Masanja Kadogosa, amesema Serikali imetekeleza ahadi ya kuanzisha safari hiyo pamoja na kuendelea na mipango ya kuupanua uwanja wa ndege wa Mwanza ili uwe na hadhi ya kimataifa.
Kadogosa amesema mpaka kufikia hatua kulifanyika mijadala mikubwa bungeni kuhusu maendeleo ya uwanja huo hatua ambayo imesaidia serikali kutoa ahadi kwamba maboresho na upanuzi zimetekelezwa.