mtwa mkulu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2013
- 8,586
- 11,227
Sulbakheri Tehrani...Shkamooni Dar es salaam......Asalam aleykum Tehran, Baghdad na Syria...
Mpaka jioni hii Kwa majira ya Africa Mashariki hakuna tunachoweza kuficha kuhusu athari zilizojitokeza kuhusiana na makombora yaliyofurushwa na iran.
Iran ilirusha takribani makombora 180 kuelekea Israel, jeshi la Israel lilisema. Hilo lingelifanya kuwa shambulizi kubwa kidogo kuliko mashambulizi ya Aprili, ambayo yalishuhudia takribani makombora 110 ya balistiki na makombora 30 ya baharini yakirushwa kuelekea Israel.
Picha za video zilizobebwa na TV ya Israel zilionekana kuonesha baadhi ya makombora yakiruka juu ya eneo la Tel Aviv muda mfupi kabla ya 19:45 saa za ndani (16:45 GMT).
Makombora mengi yaliangushwa na mifumo ya ulinzi ya anga ya Israel, afisa wa usalama wa Israel alisema, huku mwandishi wa BBC mjini Jerusalem akisema baadhi ya kambi za kijeshi zilipigwa, pia migahawa na shule zilipigwa.
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) lilisema kuwa asilimia 90 ya makombora yalifikia maeneo yao, likisema makombora ya hypersonic yametumiwa kwa mara ya kwanza. Duru za IRGC zilisema kuwa kambi tatu za kijeshi za Israel zililengwa.
Ayatollah khominei kiongozi wa mamlaka ya Iran
Mamlaka ya ulinzi wa kiraia ya Palestina katika mji unaokaliwa wa Ukingo wa Magharibi wa Jeriko ilisema mtu mmoja alikufa wakati wa shambulio la kombora la Iran.
Kulingana na shirika la habari la AFP, ambalo lilizungumza na gavana wa jiji Hussein Hamayel, mwathiriwa aliuawa na vifusi vya roketi vilivyoanguka.
Maafisa wa Israel hawajaripoti majeraha yoyote mabaya kutokana na mashambulizi ya anga ya Jumanne, lakini madaktari wa Israel walisema watu wawili wamejeruhiwa kidogo na milipuko.
Tunaweza kujumuisha athari hizo Kwa kusema yafuatayo
- Majeruhi wawili tuu.
Soma Pia: Makombora ya Iran yametua Israel bila kipingamizi cha mitambo ya Iron Dome. Je, Israel imefanya makusudi ili ipate backup nzito ya Kuitindua Iran?

- Kifo Cha mpalestina mmoja
- Uharibifu wa majengo na