Naona umekuja napo pataka, thibitisha hili na umejuaje ? Naam a anapanga yatokee na yote yapo katika milki yake.Haya yanatokea pasi na chochote ila bahati mbaya, haiitaji hata akili kubwa kufikiria hili... kwani kuna anaepanga mvua inyeshe au isinyeshe? Kuna anaepanga matetemeko au vimbunga? Ivo ni vitu vinatokea venyewe na ni nature...
Sent using Jamii Forums mobile app
Allah anapanga mvua inyeshe na wpai inyeshe na wapi isinyeshe.
Anasema Allah aliye juu :
65. Na Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Kwa hakika katika hayo imo Ishara kwa watu wanao sikia. (an-Nahl : 65)
Akasema tena Allah :
28. Naye ndiye anaye iteremsha mvua baada ya wao kwisha kata tamaa, na hueneza rehema yake. Naye ndiye Mlinzi Mwenye kuhimidiwa. (ash-Shuura : 28)
Akasema Allah mtukufu :
43. Je! Huoni ya kwamba Mwenyezi Mungu huyasukuma mawingu, kisha huyaambatisha, kisha huyafanya mirundi? Basi utaona mvua ikitoka kati yake. Na huteremsha kutoka juu kwenye milima ya mawingu mvua ya mawe, akamsibu nayo amtakaye na akamuepusha nayo amtakaye. Hukurubia mmetuko wa umeme wake kupofua macho. (an-Nuur :43)
Angalizo tunapowawekea hizi aya mnatakiwa mzisome Kisha mtafakari, sababu Allah anapenda watu wanao fikiri na kuzingatia.
Sasa wewe tuthibitishie ya kuwa yanatokea tu pasi na chochote.