Hujaelewa! Nadhani mtoa mada alitaka kutufundisha kuwa hakuna kitu chenye uwezo wa kujiumba! Atheist ameona gari zuri akasema aliyelibuni alituliza akili kweli kweli! Kama akiambiwa hilo gari halikubuniwa wala kuundwa na mtu huja juu! Madai yake, gari haliwezi kujiunda lazima yupo aliyeliunda!
Kama hivyo ndivyo! Tunawaomba ma'atheist' kukubali pia, mwanadamu hakujiumba!!! Lazima yupo aliyemuumba! Na kama yupo, hawezi kuwa mwingine zaidi ya MUNGU!
Wewe ndio hujaelewa
Unaposema nyumba ina muundaji maana yake ni kitu ambacho una ushahidi nacho, ni kitu ambacho umeki experience kupitia mazingira uliyotoka, ni kitu ambacho kina fahamika na kila mtu na hata wewe unaishi kwenye nyumba. So kufikiria nyumba imeumbwa ni fact based on personal experience.
Sasa Ulimwengu umeumbwa, una experience yeyote kusapoti madai yako? Wapi uliwahi kuona ulimwengu ukiumbwa ili tuone ni sawa kufikiria huu ulimwengu umeumnwa?
Nisome vizuri hapa
Kiufupi mleta mada kaja na analogy ya watchmaker ya William Paley ambayo katika teleological arguments hii ni moja ya analogy ya kijinga sana
Hii ni teleological argument inayojaribu Kuonesha uwepo wa Mungu kupitia mfano wa msanifu wa saa.
Hoja hii ilianzishwa na Paley miaka ya 1770s, Paley alidai kuwa ukienda beach katika matembezi yako fukwe ya bahari ukakuta saa chini lazima utajua tu kuwa ile saa imetengenezwa.
Alichokuwa anajaribu kusema Paley ni kuwa saa inalazimika kuwa na mtengenezaji, sasa na ulimwengu nao utahitaji mtengenezaji?
Sasa jaribu kufikiria katika mfano huo kwa kutanua wigo mpana wa mawazo, yani baada ya kutoka hapo kwenye saa ukaendelea na matembezi zaidi kwenye fukwe za beach halafu ukakuta mwamvuli, je utafikiria kuwa mtengeneza saa ndio aliye tengeneza na huo mwamvuli?
Hapana huwezi kufikiria namna hiyo, utafikiria kuwa umetengenezwa na mtengeneza miamvuli
Na tukisema tutembee tuizunguke hiyo beach tukakutana na toy la watoto, mtoa mada atafikiria kuwa ni mtengeneza saa au mtengeneza miamvuli ndio aliyetengeneza hilo toy la watoto?
Je hii haiwezi kuwahusisha watengenezaji wengi tofauti tofauti wa ulimwengu, kuwa responsible kwa kila kilichoumbwa?
The fact ni kwamba hii lazima ihusishe creators wengi wa ulimwengu na kila kitu kilichomo ndani yake.
Ukitika hapo utajiuliza maswali haya
Nani alimfundisha mtengeneza saa, mtengeneza miamvuli na mtengeneza toy?
Na nani aliwafundisha walimu wao?
After all hata ukimsoma mgunduzi wa saa ya kwanza Peter Henlein alijifunza akiwa kijana mdogo jinsi ya kuwa locksmith (katika hizo nyakati locksmith ilikuwa ni moja ya craftsmen wachache wenye uwezo na vifaa vya kuingia kwenye field ya clock making)
Alisaidiwa na craftsmen wengi pamoja na wasomi wa waliokuwa jirani na monk Friedrich Krafft ambaye alitengeneza Astrologium ambayo ni very complicated na alikuwa ni msomi wa vitu vigumu kama mathematics na astronomers ambaye alimsaidia kumpa new techniques na vifaa ambavyo vilimsaidia kutengeneza saa ya kwanza.
Kwa hiyo saa haina muundaji, ina waundaji.
Kama Paley aliangalia saa iliyopo chini na kujiuliza kuwa saa hii lazima iwe na muundaji, basi ni wazi alikuwa mjinga.
Kwasababu kama alijua kuwa ni saa lakini hakuwa na hakika kama imeundwa basi hakuwa na akili sio?
Na kama hakuweza kuelewa utofauti wa saa na vilivyomzunguka basi hakuwa mtu mwenye akili timamu.