Atheists wana mtindio wa ubongo

Atheists wana mtindio wa ubongo

Mungu ni mjuzi wa umbaji wa viumbe vyote. Pia alitoa dira na mwelekeo wa uwiano wa maisha katika mazingira aliyoishi, anayoishi na atakayoishi.
Unavyosema mjuzi wa uumbaji unakusudia kusema ujuzi wake upo limited?

Yani kuna vitu vinafanyika by surprised?
 
Binafsi nadhani unaua nzi kwa gobole! Swali ni jepesi mno na halihitaji maelezo mengi namna hii!

Kiumbe kinaweza kujiumba pasipo muumbaji? Yaani mfano, je, peni unayoandikia inaweza kujiunda yenyewe? Kikombe kinaweza kujiumba???? Kama jibu lako ni HAPANA basi hata wewe HUKUTOKEA tu! Yupo aliyekuumba!

Yaani, kama mifumo rahisi kabisa iliyofanyika kwa mikono na akili ndogo ya mwanadamu haikutokeatokea tu sembuse complicated system iliyofanyika kwa akili nyingi sana????

Nawashauri mtoke kwenye ulevi wenu na mkubali kuwa yupo MUNGU muumba wa vyote!!
Ngoja tuendelee kuua nzi kwa gobole

Huyo muumbaji alijiumba?
 
Unavyosema mjuzi wa uumbaji unakusudia kusema ujuzi wake upo limited?

Yani kuna vitu vinafanyika by surprised?
Kwa nini unadhani nakusudia kusema ujuzi wake upo limited?
Kitu gani hakijaeleweka katika post # 1261?
 
Ni kwasababu haupo specific

Labda nikuulize tena kwa namna nyepesi

Mungu wako unayemuamini kuwa yupo ana sifa ya ujuzi wote wa kujua yaliyopita, yajayo na ya sasa?

Au hana ujuzi wote yani kuna vitu vinafanyika bila yeye kujua?
 
Binafsi nadhani unaua nzi kwa gobole! Swali ni jepesi mno na halihitaji maelezo mengi namna hii!

Kiumbe kinaweza kujiumba pasipo muumbaji? Yaani mfano, je, peni unayoandikia inaweza kujiunda yenyewe? Kikombe kinaweza kujiumba???? Kama jibu lako ni HAPANA basi hata wewe HUKUTOKEA tu! Yupo aliyekuumba!

Yaani, kama mifumo rahisi kabisa iliyofanyika kwa mikono na akili ndogo ya mwanadamu haikutokeatokea tu sembuse complicated system iliyofanyika kwa akili nyingi sana????

Nawashauri mtoke kwenye ulevi wenu na mkubali kuwa yupo MUNGU muumba wa vyote!!
Kiumbe kutoweza kujiumba maana yake sio kwamba ni lazima kiwe kimeumbwa na Mungu.

Kama vile wewe kutoweza kujizaa maana yake sio kwamba baba yako ni James Bond 007.

Usilazimishe kwamba, kwa kuwa kiumbe hakiwezi kujiumba, basi ni lazima kimeumbwa na Mungu.

Ukilazimisha hivyo, utakuwa umefanya logical non sequitur.

Ni sawa na kusema wewe baba yako ni James Bond 007, kwa sababu haiwezekani uwe umejizaa mwenyewe.

Ni lazima uthibitishe huyo Mungu yupo kwanza.

Ni lazima uthibitishe huyo James Bond 007 yupo kwanza.
 
Kwa mantiki hio basi Mungu nae aliumbwa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninachosema hapa, kama kiumbe haliwezi kujiumba basi lazima yupo aliyekiumba! Huyo ni mwenye akili na maarifa yote! Kama hutaki kumwita Mungu tafuta jina lako utakaloona linafaa! Wapo waliomwita Jehova, wapo waliomwita God, wapo waliomwita Yahwe, wapo waliomwita Murungu nk.

Siwezi kukuchagulia jina la kumwita ila wewe angalia makuu aliyokutendea angalia utakavyomwita!
 
Yeye kaumbwa na nani basi? Maana "hakuna kitu kinachojiumba"
Na kwamba "anatenda makuu"?... makuu yapi hayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninachosema hapa, kama kiumbe haliwezi kujiumba basi lazima yupo aliyekiumba! Huyo ni mwenye akili na maarifa yote! Kama hutaki kumwita Mungu tafuta jina lako utakaloona linafaa! Wapo waliomwita Jehova, wapo waliomwita God, wapo waliomwita Yahwe, wapo waliomwita Murungu nk.

Siwezi kukuchagulia jina la kumwita ila wewe angalia makuu aliyokutendea angalia utakavyomwita!
Unajuaje "yupo aliyekiumba" ?

Nikikwambia mtu kaumbwa na baba na mama yake, utasema hao baba na mama ndiyo Mungu?
 
Uwepo wake hauthibitishiki sasa...

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mtoto mmoja siku moja aliposikia mwalimu wake anasema hakuna Mungu eti kwa sababu tu hamwoni aliwaambia wenzake "niliwaambia, hana akili huyu"!!! Mwalimu wake alipohamaki na kuja juu, aliwauliza wenzake, je, mkimuangalia kichwani mnaona akili? Wenzake wakasema hatuoni! Walitumia kigezo cha kutoona furushi la akili kichwani kwa mwalimu wao kama kigezo cha kuamua kwamba mwalimu wao hamnazo!

Mi Nadhani, si kila kisichoonekana hakipo! Kuna vitu ambavyo havionekani kwa macho ya mwilini lakini vipo! Utajua kwamba vipo kwa kuona madhala yake maishani!
 
Tatizo mnam describe Mungu katika namna tofauti ambazo zinakuja kuwabana mbeleni

Mungu mnadai ni roho asiyeonekana, at the same time mafundisho yenu katika uumbaji yanasema Mungu alifinyanga udongo kwa mikono na kumuumba Adam kisha kumpulizia pumzi.

Mtu anajiuliza kumbe Mungu naye ana mikono kama sisi na anaweza kufinyanga udongo kama wahunzi

Sasa kwa scenario hiyo unakuwa umetoka kwenye invisible God kwenda kwenye visible God na hapo ushahidi wa kuona lazima uwe na mashiko

Ukitoka hapo tena kuna sehemu katika mafundisho yenu yameelezea muonekano wake wa kimaumbile kuwa ni mwanaume ambaye ameketi kwenye kiti cha enzi kisha mkono wa kuume ameshika upanga ukatao kote na kote

Mtu anakuwa anajiuliza, huyu Mungu ambaye haonekani imekuwaje ahitaji kiti kwa ajili ya kukaa? So ina maana ana makalio?

Sasa hayo maelezo ndio yanayokuja kuwabana kwa watu ambao wanahoji ushahidi wa kuona kwa macho.
 
Kuna mtoto mmoja siku moja aliposikia mwalimu wake anasema hakuna Mungu eti kwa sababu tu hamwoni aliwaambia wenzake "niliwaambia, hana akili huyu"!!! Mwalimu wake alipohamaki na kuja juu, aliwauliza wenzake, je, mkimuangalia kichwani mnaona akili? Wenzake wakasema hatuoni! Walitumia kigezo cha kutoona furushi la akili kichwani kwa mwalimu wao kama kigezo cha kuamua kwamba mwalimu wao hamnazo!

Mi Nadhani, si kila kisichoonekana hakipo! Kuna vitu ambavyo havionekani kwa macho ya mwilini lakini vipo! Utajua kwamba vipo kwa kuona madhala yake maishani!

Kitu kama hakionekani kama kipo lazima hua kuna namna ya kuthibitisha uwepo wake. Tunataka tu namna ya kumthibitisha mungu, Mungu yeyote yule kati ya maelfu ya miungu wanaoabudiwa dunian kote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo mnam describe Mungu katika namna tofauti ambazo zinakuja kuwabana mbeleni

Mungu mnadai ni roho asiyeonekana, at the same time mafundisho yenu katika uumbaji yanasema Mungu alifinyanga udongo kwa mikono na kumuumba Adam kisha kumpulizia pumzi.

Mtu anajiuliza kumbe Mungu naye ana mikono kama sisi na anaweza kufinyanga udongo kama wahunzi

Sasa kwa scenario hiyo unakuwa umetoka kwenye invisible God kwenda kwenye visible God na hapo ushahidi wa kuona lazima uwe na mashiko

Ukitoka hapo tena kuna sehemu katika mafundisho yenu yameelezea muonekano wake wa kimaumbile kuwa ni mwanaume ambaye ameketi kwenye kiti cha enzi kisha mkono wa kuume ameshika upanga ukatao kote na kote

Mtu anakuwa anajiuliza, huyu Mungu ambaye haonekani imekuwaje ahitaji kiti kwa ajili ya kuka? So ina maana ana makalio?

Sasa hayo maelezo ndio yanayokuja kuwabana kwa watu ambao wanahoji ushahidi wa kuona kwa macho.
Tofauti za description ya Mungu inatokana na uwezo wetu mdogo tulionao juu ya kumuelezea huyu Mungu!

Kuna kajitabu niliwahi soma miaka ya nyuma kidogo, sikumbuki title yake! Kuna vipofu wawili walikuwa wanampapasa tembo kwa mikono yao na kumuelezea kulingana na kiungo walichoshika wakati wakimpapasa!

Aliyeshika na kupapasa sikio alisema tembo ni kama ungo fulani mkubwa sana! Aliyeshika ubavu alipinga sana na kusema hapana!, kwa mujibu wake yeye alidai tembo ni kama ukuta mkubwa sana! Yupo aliyeshika mkonga....., yupo aliyeshika mguu! na kadhalika! Wote walimuelezea kulingana na namna tembo huyo alivyojifunua kwake!

Ndivyo ilivyo kwa Mungu! Hakuna aliyemuona kwa macho ya nyama! Wote tunadonoadonoa tu kidogo tunachojua kuhusu Mungu!

Udhaifu wetu katika kumfafanua huyu Mungu si kigezo kwamba hakuna Mungu! Mungu yupo na ndiye aliyetuumba sisi sote! Na alituumba kwa makusudi maalumu! Kama ambavyo aliyeumba gari alivyokuwa na makusudi maalumu ya kuumba gari ndivyo na Mungu alivyotuumba sisi!
 
Kitu kama hakionekani kama kipo lazima hua kuna namna ya kuthibitisha uwepo wake. Tunataka tu namna ya kumthibitisha mungu, Mungu yeyote yule kati ya maelfu ya miungu wanaoabudiwa dunian kote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo kwenye kumthibitisha nitaomba nikusumbue uingie kwenye ulimwengu wa kiroho kwa njia ya maombi naamini atajifunua kwako!

Mfano, binafsi nimewahi kumuomba Mungu ajidhihirishe kwangu katika changamoto mbalimbali nilizopitia na alitenda yasiyowezekana kutendeka kwa uwezo wangu wa kibinadamu!

Wapo walimuomba awaponye magonjwa na walipona! Wapo waliomwomba awape hiki na kile na ikawa! Hata wewe kwa uaminifu ukimwomba Mungu ajifunue kwako kwa namna unayotaka naamini atatenda! Lakini kwamba nikwambie twende nikuoneshe Mungu yupo Tabata nadhani nitakuwa nakudanganya!
 
Tofauti za description ya Mungu inatokana na uwezo wetu mdogo tulionao juu ya kumuelezea huyu Mungu!

Kuna kajitabu niliwahi soma miaka ya nyuma kidogo, sikumbuki title yake! Kuna vipofu wawili walikuwa wanampapasa tembo kwa mikono yao na kumuelezea kulingana na kiungo walichoshika wakati wakimpapasa!

Aliyeshika na kupapasa sikio alisema tembo ni kama ungo fulani mkubwa sana! Aliyeshika ubavu alipinga sana na kusema hapana!, kwa mujibu wake yeye alidai tembo ni kama ukuta mkubwa sana! Yupo aliyeshika mkonga....., yupo aliyeshika mguu! na kadhalika! Wote walimuelezea kulingana na namna tembo huyo alivyojifunua kwake!

Ndivyo ilivyo kwa Mungu! Hakuna aliyemuona kwa macho ya nyama! Wote tunadonoadonoa tu kidogo tunachojua kuhusu Mungu!

Udhaifu wetu katika kumfafanua huyu Mungu si kigezo kwamba hakuna Mungu! Mungu yupo na ndiye aliyetuumba sisi sote! Na alituumba kwa makusudi maalumu! Kama ambavyo aliyeumba gari alivyokuwa na makusudi maalumu ya kuumba gari ndivyo na Mungu alivyotuumba sisi!
Utajuaje kwamba uwezo wenu mdogo si pamoja na kuelezea sifa kwenye kitu ambacho hakipo?
 
Back
Top Bottom