Hapa unasema maswali umeyajibu
Hapa unakiri kuwa maswali niliyokuuliza Mungu ndio anayajua majibu yake.
Kwa maana kwamba ulichokisema hapo juu kuwa umejibu, ni uongo.
Kama maswali unayoulizwa yamekuzidi uwezo ukisema tu hujui mi nitakuelewa, ila uki spin swali kwa lengo la kujirahisishia utaonekana unakwepa hoja ambazo zina reveal uongo kwenye dhana ya uwepo wa Mungu
Hapa sasa kwa kukubali kuwa hujui ndio umefanya uungwana
Na sasa naondoka eneo hilo nakuuliza swali lingine.
Una amini Mungu katika msingi wa dini?
Kama ndio niambie dini gani?
Kwa hiyo ujuzi wa Mungu umeu-set katika single room ya uumbaji tu, nje na hapo Mungu sio mjuzi wa yote sio?
Umesema Mungu ni mjuzi wa uumbaji, kwa maana hiyo kabla ya uumbaji Mungu wako hakuwa na ujuzi.
Maswali yako ni yaleyale, awali nilikujubu .
Nakunukuu:
"Hapa unakiri kuwa maswali niliyokuuliza Mungu ndio anayajua majibu yake.
Kwa maana kwamba ulichokisema hapo juu kuwa umejibu, ni uongo."
Hapana, sio uongo. Shida ipo kwako.Kwa makusudi, umejizima data za ufahamu. Hivyo huwezi kuelewa.
Nakunukuu:
"Kama maswali unayoulizwa yamekuzidi uwezo ukisema tu hujui mi nitakuelewa, ila uki spin swali kwa lengo la kujirahisishia utaonekana unakwepa hoja ambazo zina reveal uongo kwenye dhana ya uwepo wa Mungu"
Sio kwamba yamenizidi uwezo, bali akili zangu hazina ufunuo wa majibu yake.
Nakunukuu:
"Hapa sasa kwa kukubali kuwa hujui ndio umefanya uungwana.
Na sasa naondoka eneo hilo nakuuliza swali lingine. Una amini Mungu katika msingi wa dini?
Kama ndio niambie dini gani?"
Uungwana hutendwa na muungwana, na majibu yake ni ya kiungwana pia.
Naamini Mungu katika msingi wa imani. Elewa kwamba, Mungu hatokani na dini. Hivyo sioni umhimu wa kujibu swali hilo.
Nakunukuu:
"Kwa hiyo ujuzi wa Mungu umeu-set katika single room ya uumbaji tu, nje na hapo Mungu sio mjuzi wa yote sio?
Umesema Mungu ni mjuzi wa uumbaji, kwa maana hiyo kabla ya uumbaji Mungu wako hakuwa na ujuzi."
Nilikujibu kuwa sijui dimensions za ujuzi wa Mungu. Ni mojawapo ya maswali ambayo sina majawabu yake.