Athlete Crown sio gari la kubishana nalo ukiwa barabarani acha liende

Athlete Crown sio gari la kubishana nalo ukiwa barabarani acha liende

Dereva wenu alikuwa mwoga sidhani kama voksiwagen anaweza kumuacha kabisa crown
acha utani ww crown level za mark x sio VW..
CROWN hata kiteza cha 4cylinder kinamtoroka vizuri tu kina rpm kubwa speed 180 ila ukikamua kina pitiliza kurudi kwenye 0..
 
Gari yoyote yenye injini ya GX100 ogopa sana.likifungua hata uwe na range rover v8 na uko spidi 200 itakupita kama umesimama na huku yenyewe imeandikwa spidi 180
acha ushamba ww
1G injini ya kizamani unaijua 1jz
tubishane kitaalam 1g ambayo we unaiita ya gx100 inachelewa kuchanganya hp ndogo..huwezi fananisha hata brevis
 
niambieni na hii gari yetu landcruiser prado SKZ ENGINE DIESEL, alafu ni TURBO, niliifungua speed 140 hadi gari inapiga mluzi, na tyre zikitanuka kwenda nje,, nilivipita visubaru na vialtezza, kama napita baiskeli tu. sijui hiyo athlete crown kama ingenikamata kwa kweli.
ingekuws ligi usingezikamata hata ingekuwa rav 4 1AZ
 
hiyo crown ina spidi ya kawaida sana mkuu,mwenye brevis hapa aje aweke ushuhuda,kuna jamaa yangu ana hiyo crown nishafanya nae sana ligi na brevis hajawahi kunikamata....nashangaa brevis mmeiweka kando,bado hamjakutana na gari zenye kasi eeh?
waambie hawaijui injini ya 1jz
 
Sasa mkuu ulikuwa unataka kufa au? Toka lini nisani na toyota vikafukuzana?
Hiyo Fuga habari yake sio nzuri kabisa, na usirudie tena kufukuzana na gari ya Nissan kama upo na Toyota labda uweumeizidi cc mf. ww uwe na gx100 ufukuzane na Nissan duet labda utashinda lakini sio una ki-vits chako upange ligi na duet lazima uambulie kusoma plate number tu.
duet na vits mbona zote ni toyota na zote ni cc990
 
Humu wengi mdebwedo kisa mnaendesha gari za kike automatic ukipewa manual hata kuwasha tu huwezi!
 
Speed kasi hutegemea ukubwa wa engine na piston

Gari hata iwe na speedometer inayosoma 260 ila ni 2500 cc v6 haiwezi ifikia 3600cc v6 yenye 200
njoo prado yako mi nikae na brevis tuweke km 20 nani anawahi kufika...mbona utatengua kauli
 
Sikuwai Kusafiri safari ya mbali basi bwana nikapata safari ya kwenda mkoa(bukoba),nikamchukua Sista na mshikaji wangu Mmoja hivi, saa kumi alfajiri nikaanza safari,njiani baada ya kibaha,kikajitokeza hicho kicrown bwana,tulihangaishana kinatembea hatari, uzuri asubuhi kunakua hakuna magari mengi,mwisho wa siku Jamaa alinipigia honi kukubali yaishe nikampungia mkono sikuwai kumuona tena..nilikua naendesha harrier(Lexus 300) 6 cylinder..
harrier hio hata mark 2 110 anakuchapa fimbo
..
 
Back
Top Bottom