Athlete Crown sio gari la kubishana nalo ukiwa barabarani acha liende

crown mjin kero sasa
Mimi nataka kwenye kushindanisha wanipe Toyota Chaser Gr80( Chaser Mayai) yenye injini ya 1G ambayo ni manual.

Kisha mwingine awe na CROWN yenye 2500cc na hii isiwe drag race maana Crown kwenye drag race atanipita bila ubishi sababu ya uwezo wake wa ku take off.

Nataka tupewe walau km 100 na njia nzuri ni kipande cha Kahama-Runzewe-Nyakanazi huyo wa Crown hapo atasoma namba kwa Chaser Mayai mwendo wa kucheza na pedal 3.
 
Engine sawa sawa lakini gear box zinatofautishwa kwenye suala la speed mzee baba...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Boti imekula engine ya 109 hahaha πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Mkuu kuna project nyingine hapa Bongo kuna mzungu anataka afunge injini ya Discovery V8 petrol kwenye Reinforced Fiber Boat na inafanyiwa modification Kwa kuwekewa gearbox ya marine ya ZF na mfumo wa jet propulsion.

Huyo mzungu ni muumini mkubwa wa high speed kwake suala la mafuta sio Tatizo. Hii project nami nimekaribishwa kama mualikwa ikianza nitasogeza video humu.
 
DAR-moro ni kipande cha hovyo, madereva wengi wanachukia hicho kipande kutokana na usumbufu wake hata ukitembea usiku wa manane bado utapata shida Tu...
Hizi speed za 150km/h zinatumika sehemu chache mno
Kwahiyo hakuna jinsi mtu atakaeanzia dar afike singida sawa na yule atakaeanzia moro.

Hata ukienda kaskazini kupitia bagamoyo, kile kipande cha kuanzia mwenge mpaka bagamoyo kinaudhi sana.
 
Hata kutoka Moro hadi Singida hiyo 150kph FLAT, huwez kuipata kote. Kwa maana Gairo,Kibaigwa,Dumila,Pandambili,Mbande,Chalinze ya Kongwa jct,Bahi,Dodoma yote hadi Mizani, humo kote lazima upunguze speed.
Sawa.

Ila hatasumbuka sana kama atakaeanzia dar.

Kukuta foleni hata kibaha ni kitu cha kawaida sana.
 
Shule inakaaje pemebeni ya high way?

Hiyo ni ya kuihamisha haraka sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…