Athlete Crown sio gari la kubishana nalo ukiwa barabarani acha liende

Athlete Crown sio gari la kubishana nalo ukiwa barabarani acha liende

Mkuu tupia picha ya hiyo cresta new model tuione.
Daah labda itakua hii jombaa,hahah.
EkkQq3-XgAAaO8n.jpg
 
crown mjin kero sasa
Mimi nataka kwenye kushindanisha wanipe Toyota Chaser Gr80( Chaser Mayai) yenye injini ya 1G ambayo ni manual.

Kisha mwingine awe na CROWN yenye 2500cc na hii isiwe drag race maana Crown kwenye drag race atanipita bila ubishi sababu ya uwezo wake wa ku take off.

Nataka tupewe walau km 100 na njia nzuri ni kipande cha Kahama-Runzewe-Nyakanazi huyo wa Crown hapo atasoma namba kwa Chaser Mayai mwendo wa kucheza na pedal 3.
 
Unajua kuna watu wanajisemea mambo tu.

Ameona Speedometer inasema 240 na nyengine 180 basi anaona kuwa ya 240 iko fasta. Crown inavuka 180, hii michoro tu ujue unaendaje. Chukua gari yoyote ya Uingereza mfano tuseme Toyota avensis utaona kuwa ina 240km/hr ila toyota avensis hio hio lakini kutoka Japan utakuta ina 180 na engine sawasawa.
Engine sawa sawa lakini gear box zinatofautishwa kwenye suala la speed mzee baba...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Boti imekula engine ya 109 hahaha 😂😂😂
Mkuu kuna project nyingine hapa Bongo kuna mzungu anataka afunge injini ya Discovery V8 petrol kwenye Reinforced Fiber Boat na inafanyiwa modification Kwa kuwekewa gearbox ya marine ya ZF na mfumo wa jet propulsion.

Huyo mzungu ni muumini mkubwa wa high speed kwake suala la mafuta sio Tatizo. Hii project nami nimekaribishwa kama mualikwa ikianza nitasogeza video humu.
 
DAR-moro ni kipande cha hovyo, madereva wengi wanachukia hicho kipande kutokana na usumbufu wake hata ukitembea usiku wa manane bado utapata shida Tu...
Hizi speed za 150km/h zinatumika sehemu chache mno
Kwahiyo hakuna jinsi mtu atakaeanzia dar afike singida sawa na yule atakaeanzia moro.

Hata ukienda kaskazini kupitia bagamoyo, kile kipande cha kuanzia mwenge mpaka bagamoyo kinaudhi sana.
 
Hata kutoka Moro hadi Singida hiyo 150kph FLAT, huwez kuipata kote. Kwa maana Gairo,Kibaigwa,Dumila,Pandambili,Mbande,Chalinze ya Kongwa jct,Bahi,Dodoma yote hadi Mizani, humo kote lazima upunguze speed.
Sawa.

Ila hatasumbuka sana kama atakaeanzia dar.

Kukuta foleni hata kibaha ni kitu cha kawaida sana.
 
Mbaya zaidi vijiji vyenyewe havijasajiliwa ni wale wakimbia mji.Barabara ya segera chalinze ndio vimejaa viingi halafu vibao vinaanzia nyuma sana ni kama vile mtaji wa trafick kwenye hivi vibao,
Napendekeza spidi limit iwe 80Km/h kwa vijiji na 30 Km/h kwa mashule.
Shule inakaaje pemebeni ya high way?

Hiyo ni ya kuihamisha haraka sana.
 
Back
Top Bottom